Kuna kipindi ni muhimu kukubali kwamba kifo kwa ujuzi wetu wa sasa hakiepukiki, na kuna watu wataendelea kuishi baada ya mtu kufariki, hivyo, inaweza kuwa busara kuweka mbele interests za watakaobaki.
Hususan kama mgonjwa anaumwa ugonjwa chronic na kashakuwa mtu mzima.
Mimi siwezi kubariki wazo la kuuza nyumba zangu nilizohangaikia maisha yangu yote, zije kuwa nguzo ya kusaidia uchumi wa kizazi changu na ndugu zangu wa karibu, ili tu niongeze miaka michache katika maisha yangu.
Kitu cha muhimu kabisa ni kujiweka katika mazingira ambayo hatuhitaji kuchagua kimoja kati ya mawili haya, na tunaweza kufanya yote. Kujihudumia matibabu bila kufikia hatua ya kufanya kitu kama kuuza nyumba.