Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Uhai ulikuwepo kabla ya binadamu kugundua pesa na nyumba,Mimi nitauza kila kitu kupigania uhai was mmpendwa wangu!

Haya mavitu niyakutafuta Ila uhai haununuliwi haijalishi nitabaki kwenye wakati gani nitanyanyuka na kupambana tena
Hakika una moyo kama wa mwanajeshi
 
Usikate tamaa,, huwezi kuacha mtu afe kisa kulinda mali, uhai unatoka kwa Mungu ma sio mwanadamu, why ukate tamaa? Huko mbeleni bila shaka utaomba wagonjwa mahututi ama walio ugua muda mrefu, wapigwe sindano za sumu wafe...weka utu mbele..
 
Wengine tumeshapita huko, na shida ilikuwa maDr walikuwa wanadanganya kuwa mzee ana tatizo flani linalotibika lakini kwa pembeni wanawaambia watu baki kwamba huyu mzee hana muda mrefu, kansa imesambaa kila mahali.
Doctor mbaya sana huyo aisee...
 
Hii Mada yako iko sawa; Labda ila nadhani inategemeana na Potential ya Mtu; Mfano mtu alikuwa ni mpambanaji (potential) hili lazima liangaliwe kwanza kupambana kuhakikisha anatoboa,
Sasa unakuta watu wanapambana na Mtu wa 90, of which kama Busara alishawaachia wenye umri mdogo, lakini hela inatumika nyingi sana tena kwa kuchangishana binafsi sionagi umuhimu wake.

Kama Hela ya Matibabu ya muda mrefu ipo na si tatizo miongoni mwa wanafamilia, then atibiwe tu mpaka umauti utakapomfiika.
Umefafanua vema sana mkuu
 
Kuna kipindi ni muhimu kukubali kwamba kifo kwa ujuzi wetu wa sasa hakiepukiki, na kuna watu wataendelea kuishi baada ya mtu kufariki, hivyo, inaweza kuwa busara kuweka mbele interests za watakaobaki.

Hususan kama mgonjwa anaumwa ugonjwa chronic na kashakuwa mtu mzima.

Mimi siwezi kubariki wazo la kuuza nyumba zangu nilizohangaikia maisha yangu yote, zije kuwa nguzo ya kusaidia uchumi wa kizazi changu na ndugu zangu wa karibu, ili tu niongeze miaka michache katika maisha yangu.

Kitu cha muhimu kabisa ni kujiweka katika mazingira ambayo hatuhitaji kuchagua kimoja kati ya mawili haya, na tunaweza kufanya yote. Kujihudumia matibabu bila kufikia hatua ya kufanya kitu kama kuuza nyumba.
Umenena vema hapa
 
Wengine tumeshapita huko, na shida ilikuwa maDr walikuwa wanadanganya kuwa mzee ana tatizo flani linalotibika lakini kwa pembeni wanawaambia watu baki kwamba huyu mzee hana muda mrefu, kansa imesambaa kila mahali. Kukawa na plan ya kwenda India, wakataka vipimo flani ambavyo ilibidi kwenda Muhimbili baada ya kama wiki nikawa na wasiwasi na hali ya mgonjwa maana alikuwa katika hali ambayo hawezi safiri mwenyewe, kumbana Dr mmoja akawa mkweli akasema huyu mzee ana prostate cancer na imeshakula organs zote na cha kufanya sasa nawapa dawa za kupunguza maumivu mrudisheni nyumbani akapumzike. Hakumaliza week 2 mzee akapumzika.
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom