Sidhani kama ni busara kuihusisha team ya mpira ya taifa na mambo ya kisiasa,
Hata sheria za FIFA zimekataza hilo,wanaoichukia team ya taifa kwa mrengo wa kisiasa na wanaoipenda team ya taifa kwa mrengo wa kisiasa,wote wanafanya makosa,
Team ya taifa itakumbukwa kwa record za FIFA kama team ya Tanzania na sio team ya chama chochote cha kisiasa,michezo huwaunganisha watu na sio kuwagawa watu,
Linapokuja suala la kitaifa kama team ya mpira ni vizuri watu kuweka tofauti zao pembeni,
mfano ukiangalia team ya taifa ya Iraq ina wachezaji kutoka different sects,notably Shia,Sunni and Kurdish,ila hua wanaungana kuishangilia team yao na wachezaji hucheza kwa kushirikiana na kusahau tofauti zao,2007 walifanikiwa kushinda kombe la Asian Cup na nchi nzima walishangilia ushindi ule,so michezo itumike kuwaunganisha watu coz hata sheria za FIFA zipo wazi kabisa kukataza siasa kuingilia Soka,
Haya ni maoni yangu kama mdau wa soka,sipo upande wowote ule Politically.