KUNA HUU WIZI UNAFANYWA KUPITIA TAASISI ZA AFYA ZA UMMA

tekman

Member
Joined
Aug 13, 2026
Posts
17
Reaction score
59
Habari wadau,
Uzi wa leo tunashona sekta ya afya hapa nchini malawi.
Wengi mnatambua kuwa kuna mfumo huu wa taasisi za afya za malawi.
Ambapo unapofika hospital inaenda kwa mlolongo ufuatao;
1. Unasajiliwa ambapo baadhi ya hospitali za serikali ya malawi hukichaji mpaka zaidi ya 10,000
2 unaenda kumuona daktari anakuandikia vipimo lakini anaandika kwenye mfumo na hakwambii anakupima nini
3.Anakutaka uende dirishani ukalipie, huko utaambiwa tu lipia 35,000.
4. Then utaenda maabara kupimwa na hapa ndio utastaajabu. Mtu wa maabara takupima Malari, Mkojo UTI na labda akuombe choo. Na hapo 35,000 yako itakuwa imeliwa 🤣🤣.
Vipimo hivyo hivyo ukienda maabara za private zenye vifaa bora zaidi haiwezi kugharimu zaidi ya 15,000.

MY TAKE ni kama hii familia ya kifalme imetoa maagizo watu walete pesa kwa kila namna. Maana haimake sense kabisa.
 
Ukirudi daktari anaandika dawa, ukifika famasi unaambiwa hii inauzwa 27,000 lakini mtaani ni 23,000.
 
Toa na pendekezo mlolongo unavyopaswa kuwa
 
Ushawahi kwenda duka la vifaa tiba ikiwa unatumia bima ukapewa mfuko umejaa ila ukifika kwa dokta anatumia bomba moja la sindano, gloves na pamba tu. Mzigo unaobaki ni halali yao kuja kumuuzia maskini mwingine.
 
Shida na nyie hamuumwi mara kwa mara alafu hamji hospital mpaka mshikwe haswaa
Hospital zitajiendesha vipi na so called viongozi wanataka tutunishe mifuko ya hospitali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…