Kuna ile dhana watu wa vijijini wanaishi miaka mingi kuliko wa mijini, kuna uhalisia kwenye ili?

Kuna ile dhana watu wa vijijini wanaishi miaka mingi kuliko wa mijini, kuna uhalisia kwenye ili?

Analog

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2024
Posts
323
Reaction score
618
Kumejengeka dhania ya kwamba watu wa vijijini wanaishi kwa muda mrefu kuliko watu wa mijini kutokana na aina ya mifumo ya maisha wanayoishi.

Unakubaliana na hili na unafikiri ni kwa nin watu wanaweka fikra hzi?
 
Ni kweli, kwa sababu wanaishi maisha halisia ya binadamu kama Mwenyezi Mungu alivyotuumba wanadamu.

Kutoka kwenye hoja yako nayafikiria mambo yafuatayo kwanini wanaishi umri mrefu; kama ifuatavyo:-

1. Hewa Safi:
Wakazi wa vijijini hupumua hewa safi isiyo na uchafuzi ukilinganisha na miji mikubwa ambayo mara nyingi ina hewa chafu kutokana na moshi wa magari na viwanda. Mijini k.v. Dar au Beijing utaona ukungu fulani hivi majira ya mchana hasa mnaofanyia kazi magorofani mtakuwa mashahidi...ile ni hewa chafu. Hata unapoingia Dar kama unaishi mkoani utaona kuna hewa fulani nzito sana ambayo dhahiri ni hewa ukaa (CO2).

2. Mazoezi ya Asili: Maisha ya kijijini mara nyingi yanahusisha shughuli za kilimo na kazi za mikono ambazo zinasaidia kuimarisha afya ya mwili. Mkaazi wa kijijini anatokwa jasho, anakojoa muda wowote na popote sasa huku mjini hakuna vyoo na vichache vya kulipia watu wanabana haja....lakini pia hawafanyi mazoezi, wale wa maofisini anatoka kwenye kiyoyozi anaingia garini kwenye kiyoyozi, ukute na nyumbani nako kiyoyozi...hakuna evening walks wala jogging wala gym...wa mjini walifanya mazoezi kidoogo wakati wa UVIKO-19 tangu hapo wameacha.......watu wamenenepeana hadi unaogopa watapasuka!!!...Change is necessary!

3. Chakula safi na Asili: Wakazi wa vijijini mara kwa mara hula vyakula vya asili na vilivyotoka shambani moja kwa moja, ambavyo ni visafi na vina virutubisho vingi. Mjini vyakula vingi ni vya kiwandani na vyenye kemikali...

4. Maisha Tulivu: Vijijini kuna utulivu zaidi na msongo wa mawazo ni mdogo ikilinganishwa na miji ambayo mara nyingi ina kelele na harakati nyingi zinazoleta stress.

5. Jamii Zilizo na Mshikamano: Jamii za kijijini zina mshikamano wa karibu na mara nyingi zina mtandao mzuri wa kijamii unaosaidia kutoa msaada wa kihisia na kimwili, jambo linaloongeza ubora na urefu wa maisha.

Matajiri wanaojitambua kote duniani huwa wanaishi vijijini au maporini huko!

N'yadikwa
[Signed]
 
1718115264958.jpg
 
Je huduma za afya kati ya mjini na vijijini wap zinapatikana kirahisi ?

Sehemu ipi mama wajawazito hufa zaidi kwa huduma za afya kuwa mbali na makazi ?

Sehemu gani hupata maji safi na salama na chakula bora kwa wakati?

Sehemu gani kati ya hizo hukumbwa na magonjwa ya milipuko mara kwa mara ambayo hupelekea vifo vingi?

Sehemu gani hukumbwa zaidi na magonjwa yasiyo ambukiza kwa wingi ?


Pia tutaangalia population kati ya mijini na vijijini ipoje , pia kuna ile kasumba watu wengi wa mijini umri ukienda wengi wao hurudi vijijini .
 
Kumejengeka dhania ya kwamba watu wa vijijini wanaishi kwa muda mrefu kuliko watu wa mijini kutokana na aina ya mifumo ya maisha wanayoishi.

Unakubaliana na hili na unafikiri ni kwa nin watu wanaweka fikra hzi?
KIJIJINI HAKUNA MWENDO KASI
HAKUNA CHIPSI
HAKUNA UZEMBE NI KAZI NGUMU
CHAKULA NI ASILI
MTOTO ANATOKA SHULE MPAKA KWAO KM 3 KWA MGUU AU BAISKELI
VITU VYA SUMU NI NADRA SANA
 
Chakula asili
Mazoezi
Pia kuna maisha ya amani na furaha kule kijijini.

Lakini hata mjini unaweza kuishi miaka mingi kama ukaachana na mambo ya hovyo hovyo.

Kama wazee wa tz na jf wengi ni hovyo hivo hata life expectancy yao ni less than 65.

Hovyo kabisa
 
Chakula asili
Mazoezi
Pia kuna maisha ya amani na furaha kule kijijini.

Lakini hata mjini unaweza kuishi miaka mingi kama ukaachana na mambo ya hovyo hovyo.

Kama wazee wa tz na jf wengi ni hovyo hivo hata life expectancy yao ni less than 65.

Hovyo kabisa
Pengine unaweza kuviepuka vyote, lakin unaweza vipi kuiepuka vipi hewa ya ukaa itokanayo na mkusanyiko wa viwanda vingi?
 
Kumejengeka dhania ya kwamba watu wa vijijini wanaishi kwa muda mrefu kuliko watu wa mijini kutokana na aina ya mifumo ya maisha wanayoishi.

Unakubaliana na hili na unafikiri ni kwa nin watu wanaweka fikra hzi?
Kaishi kijijini ushuhudie kwa macho yako na sii kuambiwa,unataka kudanja mapema endelea kung'ang'ania kuishi mjini😀
 
KIJIJINI HAKUNA MWENDO KASI
HAKUNA CHIPSI
HAKUNA UZEMBE NI KAZI NGUMU
CHAKULA NI ASILI
MTOTO ANATOKA SHULE MPAKA KWAO KM 3 KWA MGUU AU BAISKELI
VITU VYA SUMU NI NADRA SANA
Hapo kwenye chipsi nakataa
 
Vijijini wanazeeka haraka, sio kwamba wanaishi muda mrefu.
Kuhusu afya, uwepo wa hospitali zenye maabara nzuri na vifaa vya afya si suluhisho kwenye majibu ya hapa.
Mwaka jana Ilionyesha kwenye kila mimba 1000, watoto 56 wanakufa mijini, na 36 wanakufa vijijini. Na tuache story za kila siku kwamba vijijini umbali wa huduma za afya, na ukosefu wa vifaa tiba, sababu za kizamani sana tena zinazopendwa kutolewa na watu waishio mjini wasiopajua kabisa vijijini.

Point kubwa watu wa vijijini wanachoka miili haraka kuliko mjini. Sio kuishi muda mrefu.
Na ikumbukwe baada ya sensa, kuna only 3.4 % ya wazee Tanzania juu ya umri wa miaka 64.

Hapo hapo ni asilimia 63 tu ya watanzania wanaishi vijijini almost 40ml. (1-60 and above)
Piga hesabu zenu mtajua wapi wanaishi muda mrefu.
 
Watu wa vijijini wanawahi kuzeeka jambo linalotufanya tuhisi kwamba wanaishi muda mrefu ila uhalisia wa mambo Bado Ngoma inasoma droo
Nilitaka kusema hili.
Mtu wa vijana wa kijini menye 30yrs ni tofauti na wale wa mjini kwa mambo mengi.
Na ukiwaona wa mjini utasema ni mdogo kuliko wa kijijini.
Vijijini wanawahi kuoa/kuolewa mtu anawahi kua baba/mama akifika 40 tayari anaitwa babu/bibi.
 
Ni kweli maisha kijijini hayana stress kama mjini. Na stress zina punguza life span.
Ni kweli mkuu,hivi niambie umeingia kwenye mwendo kasi Posta,limeshona kisawasawa,umesimama mguu mmoja mpaka unafika Kimara hapo kuna usalama kweli...?
 
Back
Top Bottom