Kuna Jamaa ananidhulumu hela yangu. Nikienda Polisi nitapata haki?

Kuna Jamaa ananidhulumu hela yangu. Nikienda Polisi nitapata haki?

Mkuu, pole. Dawa ya deni ni kulipa. Atakulipaje? Fanya hivi. Endelea kumsumbua kwa kumpigia simu na sms za kutosha. Kwenye sms tumia lugha za kuonyesha ni kwa namna gani amekudissapoint. Kila baada ya saa tuma ujumbe au beep.
Atasikia kero kubwa na nakuhakikishia atakulipa.
Kuwa mvumilivu.
 
Wewe uliona wapi mtu anafundishwa kwanza ndo anakuja kutoa ADA?
yaani hata Mimi sikulipi.
 
Mkuu, pole. Dawa ya deni ni kulipa. Atakulipaje? Fanya hivi. Endelea kumsumbua kwa kumpigia simu na sms za kutosha. Kwenye sms tumia lugha za kuonyesha ni kwa namna gani amekudissapoint. Kila baada ya saa tuma ujumbe au beep.
Atasikia kero kubwa na nakuhakikishia atakulipa.
Kuwa mvumilivu.
Mnampa matumaini hewa.hivi shule au tuisheni zingekuwa zinafanya hivi si wangefirisika?
 
Wewe jamaa hauna uvumilivu kabisa,nimejibana subiri nitakulipa usaze,sasa kuanikana humu jf ndo unaona utapata msaada? Ukienda police hauinusi hata mia yangu jichanganye uone.
 
Wewe ni mtu wa haki, umekutana tu na mtu mwovu ndo maana anakutesa na hela yako kiasi hichi.

Nakushauri mpotezee usimdai
jamaa baada ya kupata mtu wa kumpigisha pindi akaona ametoka tayari kimaisha,akaanza kutegemea hiyo hela kuwa nitamlipa,kila saa boss boss boss inakera,mara shem hajambo,uko wapi,vipi una muda nije nikufundishe, yaani ilikuwa kero,alitegemea hiyo laki4 ndo maisha yasonge,kazi yake ya ukinyozi aliiacha kisa atapata hela,nikwambie tu ndugu, acha wenge,hela nakupa na siku nyingine ujifunze usitegemee kitu kimoja kuendesha maisha yako,na kwa wakati mwingine nikikuhtaji uje unifundishe usiwe unanisumbua kwa sms zako,unabeep sana hata salio huna, sasa nakupa kanuni,nyoa watu saloon kwako asubuh mpaka saa10 jion kisha ndo unakuja ofsini au nyumbani kwangu, staki simu zako jamaa yangu.

Na maswala ya kuanikana hadharani mara ofsi zake zipo sehem fulani,nyumbani kwake wapi,ana gari koma mara moja. Pumbavu.
 
Ushatapeliwa na wala hauwezi shitaki mahali popote kwa sababu hauna mkataba wala ushahidi unaoweza kukutetea...

Ungekuwa na mkataba au makubaliano rasmi, moja kwa moja ungeenda mahakamani kuandikisha shauri maana ishu za madai ukipeleka polisi ni sawa na kujipotezea muda...

Kwa sasa fanya kama umetoa hisani au lipiza kisasi kisivhoacha traces zozote kukurejelea...
Kwa maelezo yake, kisheria mkataba upo.

Ushauri (sio wa kisheria), usimkabe sana give it a time, mfano usidai hata kwa mwezi hivi. Then muibukie ofisini kwake usipige sana simu Kila dakika, by the way kama hapokei makusudi hata ukipiga mara mia ndo atapokea? Au unataka kumkera? Mfuate ofisini.
 
Pole ila ukishakubali kukopesha huduma unatakiwa uwe mvumilivu. Polisi hawana msaada kwenye madai.
 
Mkuu, pole. Dawa ya deni ni kulipa. Atakulipaje? Fanya hivi. Endelea kumsumbua kwa kumpigia simu na sms za kutosha. Kwenye sms tumia lugha za kuonyesha ni kwa namna gani amekudissapoint. Kila baada ya saa tuma ujumbe au beep.
Atasikia kero kubwa na nakuhakikishia atakulipa.
Kuwa mvumilivu.
Hii sio njia nzuri, kwani hajui ofisini, kwanini asimfuate ofisini
 
Wakuu habarini za wakati huu.

Mnamo tarehe moja mwezi huu wa nane, kuna jamaa mmoja hivi, ni Agent wa kusafirisha mizigo. Ana kampuni (Clearing and forwarding agency) pale posta, TWIGA HOUSE, FLOOR YA 5, ROOM NAMBA(imehifadhiwa).

Katika harakati za hapa na pale ndani ya mji, tulikutana tukafahamiana. (Mimi nina ujuzi na mambo ya IT).

Sasa huyu jamaa alikuwa na nia ya kujua IT, (system development). Tuliingia kwenye makubaliano, japo yasiyo rasmi, tukakubaliana atanilipa laki 8 for the whole course. Mwanzo tulivyoanza alisema hana advance, tusome tu mwisho wa mwezi atanipa nusu (laki nne).

Kwa kuwa nulikuwa na mishe zingine pia za hapa na pale, nilikuwa najitahidi ku-balance muda wangu ili siku isiishe bila yeye kusoma. Nilikuwa namtembelea huko ofisini kwake nampigisha pindi kila siku, weekend namfuata nyumbani kwake pale magomeni mapipa, nampigisha pindi. Jamaa sasaivi Ana uelewa na anaweza kutengeneza static website, HTML, CSS, mpaka yeye mwenyewe ananiAppreicate.

Ilivyofika tarehe 20 Jumatano mwezi huu wa nane, nilipata taarifa ya msiba wa kakaangu kutoka nyumbani. Nikamwambia "brother, sikia hichi na hichi, kuna msiba umetokea nyumbani, naomba ujitahidi ifikapo tarehe 30, unipatie chochote kitu niweze kwenda msibani. Akasema sawa.

Ndani ya hizo siku, from 20th, niliendelea kumtembelea ofisini kwake na kumpigisha pindi. Ilivofika tarehe 25. Akasema nimpe muda kidogo, tusitishe kusoma kwanza anitafutie hela ili ikifika tarehe 27, awe ameshanipatia hela, nikasema sawa brother hamna shida

Ipofika tarehe 27 hiyo, saa 12 jioni nikamtafuta, simu iliita haikupokelewa, nilipiga kama mara 5 hivi haikupokelewa, nikashtuka, "mbona sio kawaida yake kutokupokea simu?" Nikapotezea.

Tarehe 28, nimepiga simu siku nzima hakupokea, natuma text normal and whatsapp, zinakuwa delivered lakini ukimya uliendelea. Tarehe 29, nilijiskia vibaya sana maana safari ya kwenda kijijini ilifika, kulingana na assurance yake, nilitegemea hizo hela kama nauli, ikabidi nighairi safari.

Nilimtumia texts za kuchukizwa na hali ailyonionesha ya kutoipokea simu. Baada ya hizo texts, sms ikaingia iliyosomeka kama. ("Kaka Abari Mme wangu atakupa ela kama alikubalia namjua nimuaminifu nika changamoto kametokea popote ulipo utaletewa ela ntamkumbusha kama ulimtafuta na atakutimizia haki yako Kesho jumamosi ama jumapili ")

Baada ya kama nusu saa hivi nikapiga tena, kimya, nikajaribu kumpigia na namba ngeni, aka akapokea, alivyosikia Sauti yangu akasema nitakupe hela kesho "Jumamosi"

Wakuu jana saa 11 jioni nimepiga simu hadi nimechoka, hamna reply.

huyu jamaa napajua kwake (amejenga wala hajapanga, ofisi ni yake na yeye ndiye boss wa ile ofisi. Jamaa huyu Ana gari.

Swali langu; NIKIENDA POLISI NAWEZA NIKAPATA HAKI YANGU? au hili swala halina mashiko kwenye sheria?
Na nawezaje kupata haki yangu? Maana huyu jamaa baada ya kuwa na knowledge ya system development, ameanza kunigeuka kwa style hii. NIFANYEJE WAKUU. NAOMBENI USHAURI. POLISI INAWEZA KUNISAIDIA KUPATA HAKI YANGU?
Hapo twiga house kwenye lipicha la ndege?, kushoto? 5th floor?
-Jibu ndiyo au hapana! (nimepiga ramli tu)
 
jamaa baada ya kupata mtu wa kumpigisha pindi akaona ametoka tayari kimaisha,akaanza kutegemea hiyo hela kuwa nitamlipa,kila saa boss boss boss inakera,mara shem hajambo,uko wapi,vipi una muda nije nikufundishe, yaani ilikuwa kero,alitegemea hiyo laki4 ndo maisha yasonge,kazi yake ya ukinyozi aliiacha kisa atapata hela,nikwambie tu ndugu, acha wenge,hela nakupa na siku nyingine ujifunze usitegemee kitu kimoja kuendesha maisha yako,na kwa wakati mwingine nikikuhtaji uje unifundishe usiwe unanisumbua kwa sms zako,unabeep sana hata salio huna, sasa nakupa kanuni,nyoa watu saloon kwako asubuh mpaka saa10 jion kisha ndo unakuja ofsini au nyumbani kwangu, staki simu zako jamaa yangu.

Na maswala ya kuanikana hadharani mara ofsi zake zipo sehem fulani,nyumbani kwake wapi,ana gari koma mara moja. Pumbavu.
Mwanzoni alipoanza kuonyesha usumbufu ungevunja mkataba. Japo kuna watu wanadai kwa mtindo ambao mdaiwa anasema silipi sasa.
 
jamaa baada ya kupata mtu wa kumpigisha pindi akaona ametoka tayari kimaisha,akaanza kutegemea hiyo hela kuwa nitamlipa,kila saa boss boss boss inakera,mara shem hajambo,uko wapi,vipi una muda nije nikufundishe, yaani ilikuwa kero,alitegemea hiyo laki4 ndo maisha yasonge,kazi yake ya ukinyozi aliiacha kisa atapata hela,nikwambie tu ndugu, acha wenge,hela nakupa na siku nyingine ujifunze usitegemee kitu kimoja kuendesha maisha yako,na kwa wakati mwingine nikikuhtaji uje unifundishe usiwe unanisumbua kwa sms zako,unabeep sana hata salio huna, sasa nakupa kanuni,nyoa watu saloon kwako asubuh mpaka saa10 jion kisha ndo unakuja ofsini au nyumbani kwangu, staki simu zako jamaa yangu.

Na maswala ya kuanikana hadharani mara ofsi zake zipo sehem fulani,nyumbani kwake wapi,ana gari koma mara moja. Pumbavu.
Punguza ujuaji.
 
Akili mbovu sana eti "ana gari" kwahiyo gari likakuchanganya [emoji16][emoji16]
 
Kuna watu hawanaga huruma hapa duniani sijui wana moyo wa aina gani
 
Back
Top Bottom