Kuna Jamaa ananidhulumu hela yangu. Nikienda Polisi nitapata haki?

Kuna Jamaa ananidhulumu hela yangu. Nikienda Polisi nitapata haki?

Hiyo ni kesi ya madai (kuvunjwa kwa mkataba) huwezi kwenda police ,unachotakiwa ni kwenda mahakama ya mwanzo iliyopo karibu na wewe.

Pia inaweza kuwa kesi ya fraud endapo ukienda police,wanaweza wakaitwist ikawa jinai ya kujipatia huduma kwa njia ya uongo,yani alikulaghai iliapate ujuzi huku akiijua kwamba hawezi kukulipa.

Ushauri wangu ni kwamba nenda mahakamani direct ukafungue shauri la madai ikiwa ni uvunjifu wa mkataba ( oral contract)
_ Ushahidi ukiwa ni ujumbe alizikuwa anakutumia ikionesha appreciation ya mafunzo uliyompatia na kama kuna kazi zake alizokutumia kama assignment uliyompa afanye kama sehemu ya mafunzo .

_jumbe za kukuahidi kukulipa fedha zako alizokuwa anakutumia.

_ watu waliokuwa wanakuona ukienda ofisini kwake kumpatia hayo mafunzo,ingawaje hapa itabidi utumie wale ambao ni wa ofisi jirani kama wapo,maana hakuna mfanyakazi ataweza kutoa ushahidi dhidi ya Boss wake.

Pia utaonesha madhara uliyopata baada ya kushindwa kulipwa hela yako kwa wakati,na utaomba mahakama iamuru ulipwe fidia.

Kwa kifupi hiyo ni kesi ya madai,kuvunjwa kwa mkataba,ambapo wewe umeshatimiza wajibu wako ,ushahidi ukiwa mdaiwa ameonesha appreciation kwa kujua kufanya baadhi ya mambo kupitia mafunzo uliyotoa,na kwa upande mwingine mdaawa ameshindwa kutimiza wajibu wake kwa kushindwa kufanya malipo ndani ya muda uliokubaliwa,na ushahidi ukiwa ni ujumbe wake akisema atakulipa fedha zako nje kabisa ya tarehe mlizokubaliana na kwa bahati mbaya hata nje ya hiyo tarehe ya makubaliano hajakulipa hadi leo.

NB:Hicho ni kiasi kidogo cha fedha kulingana na wasifu wa jamaa ulioutoa hapa,naimani akiona WITO wa mahakama atakulipa fedha zako,sidhani kama atakubali kupoteza muda wake kwenda mahakama mara kwa mara nakuacha shughuli zake,sema amekuona mnyonge na anajaribu kukutikisa auone reaction yako,ukikaa kimya imeisha hiyo.

Anyways ni hayo tu,nimeandika sana😀
Na ili kutengeneza mazingira ionekane kuwa una mdai laki nane,tulia kwa muda kidogo halafu uje umwandikie ujumbe,kwamba kaka sikutarajia kwamba shilingi laki nane ingeweza kuharibu urafiki wetu tuliyojijengea kwa muda mrefu,naomba leo kwa uwazi kabisa uniambie nikupe muda gani ambao unafikiri utakutosha ili uwezo kunilipa hiyo laki nane,atakachojibu itakuwa admission kwamba anadaiwa laki nane,labda apinge kuwa humdai hiyo hela.

Au kaa hata mwezi nenda ofisini kwake mwambie akuandikie kwenye karatasi na asaini ,aseme ni lini atakulipa hiyo hela,akikuandikia utaitumia hiyo memo kama sehemu ya ushahidi mahakamani.
Au kama wewe ni mtoto wa mjini na una muda wa kutosha uwe unamuibukia kazini kwake siku za kazi,akiona huu usumbufu mbele ya wateja wake atakulipa ili kulinda trust yake kwa wateja wake.
 
Mnampa matumaini hewa.hivi shule au tuisheni zingekuwa zinafanya hivi si wangefirisika?
Hiyo mbinu nilishawahi kuitumia. Nilipewa na dada m1 mlokole. Baada ta kumsumbua sana akaanza kunipigia yeye. Alipoonza kunipigia yeye nikawa sipokei. Namsumbua na sms na kumbeep hata kama ni saa 8 usiku. Mwisho akaomba kulipa kidogokidogo kupitia line yangu ya simu. Akipunguza tu namwacha siku tatu, shughuli inaanza tena. Mpaka akamaliza. Nikafuta na namba yake.
 
jamaa baada ya kupata mtu wa kumpigisha pindi akaona ametoka tayari kimaisha,akaanza kutegemea hiyo hela kuwa nitamlipa,kila saa boss boss boss inakera,mara shem hajambo,uko wapi,vipi una muda nije nikufundishe, yaani ilikuwa kero,alitegemea hiyo laki4 ndo maisha yasonge,kazi yake ya ukinyozi aliiacha kisa atapata hela,nikwambie tu ndugu, acha wenge,hela nakupa na siku nyingine ujifunze usitegemee kitu kimoja kuendesha maisha yako,na kwa wakati mwingine nikikuhtaji uje unifundishe usiwe unanisumbua kwa sms zako,unabeep sana hata salio huna, sasa nakupa kanuni,nyoa watu saloon kwako asubuh mpaka saa10 jion kisha ndo unakuja ofsini au nyumbani kwangu, staki simu zako jamaa yangu.

Na maswala ya kuanikana hadharani mara ofsi zake zipo sehem fulani,nyumbani kwake wapi,ana gari koma mara moja. Pumbavu.
Mlipe tu yaishe, japo kweli amefanya makosa kukuanika. Inaonekana anapitia magumu, kwanini usifanye kama unamsaidia tu?
 
Mna mkataba ?

Unafanyaje kazi kienyeji hivo ? Yani umpigishe pindi akulipe mwisho wa mwez tena hela nusu !

Ulitakiwa uingie nae mkataba wa kimaandishi !

Pole kwa ujinga wako, next time jifunze kuiheshimu taaluma yako ! Ona sasa unaonekana kero na msumbufu kudai hela yako !

Huna cha kumfanya, as hamkua na makubaliano ya kimaandishi ama mashahidi live,,,,

Sana sana hio text ya mke wake inaweza kutumika police wakaamini ni kweli undamdai huyo mtu, lakn anaweza kukugeuka akataja kiasi pungufu na makubaliano
 
Hakikisha unampigia simu mfululizo Kila siku alfajiri ya saa 11 hadi 12 asubuhi....
Utamkera na deni atalipa..
 
Back
Top Bottom