Kuna Jamaa ananidhulumu hela yangu. Nikienda Polisi nitapata haki?

Na ili kutengeneza mazingira ionekane kuwa una mdai laki nane,tulia kwa muda kidogo halafu uje umwandikie ujumbe,kwamba kaka sikutarajia kwamba shilingi laki nane ingeweza kuharibu urafiki wetu tuliyojijengea kwa muda mrefu,naomba leo kwa uwazi kabisa uniambie nikupe muda gani ambao unafikiri utakutosha ili uwezo kunilipa hiyo laki nane,atakachojibu itakuwa admission kwamba anadaiwa laki nane,labda apinge kuwa humdai hiyo hela.

Au kaa hata mwezi nenda ofisini kwake mwambie akuandikie kwenye karatasi na asaini ,aseme ni lini atakulipa hiyo hela,akikuandikia utaitumia hiyo memo kama sehemu ya ushahidi mahakamani.
Au kama wewe ni mtoto wa mjini na una muda wa kutosha uwe unamuibukia kazini kwake siku za kazi,akiona huu usumbufu mbele ya wateja wake atakulipa ili kulinda trust yake kwa wateja wake.
 
Mnampa matumaini hewa.hivi shule au tuisheni zingekuwa zinafanya hivi si wangefirisika?
Hiyo mbinu nilishawahi kuitumia. Nilipewa na dada m1 mlokole. Baada ta kumsumbua sana akaanza kunipigia yeye. Alipoonza kunipigia yeye nikawa sipokei. Namsumbua na sms na kumbeep hata kama ni saa 8 usiku. Mwisho akaomba kulipa kidogokidogo kupitia line yangu ya simu. Akipunguza tu namwacha siku tatu, shughuli inaanza tena. Mpaka akamaliza. Nikafuta na namba yake.
 
Mlipe tu yaishe, japo kweli amefanya makosa kukuanika. Inaonekana anapitia magumu, kwanini usifanye kama unamsaidia tu?
 
ALITAKIWA achukue hela kabla ya mafunzo kuanza.hakuna elimu ya usome uje ulipe baadae.
Kosa ni lake.mtu ATOE laki 8 na tayari umeshamfundisha na ameshajua?
Unatoa ndio, kwanini tuishi maisha ya kuviziana kiasi hicho?
 
Mna mkataba ?

Unafanyaje kazi kienyeji hivo ? Yani umpigishe pindi akulipe mwisho wa mwez tena hela nusu !

Ulitakiwa uingie nae mkataba wa kimaandishi !

Pole kwa ujinga wako, next time jifunze kuiheshimu taaluma yako ! Ona sasa unaonekana kero na msumbufu kudai hela yako !

Huna cha kumfanya, as hamkua na makubaliano ya kimaandishi ama mashahidi live,,,,

Sana sana hio text ya mke wake inaweza kutumika police wakaamini ni kweli undamdai huyo mtu, lakn anaweza kukugeuka akataja kiasi pungufu na makubaliano
 
Hakikisha unampigia simu mfululizo Kila siku alfajiri ya saa 11 hadi 12 asubuhi....
Utamkera na deni atalipa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…