Kuna janga linaandaliwa vivuko vya Kigamboni, TEMESA chukueni hatua

Hivi Kuna kina kiasi gani hapo,?
 
Watu wa Dar wanapenda wenyewe na wamezoeshwa kubanana hata kwenye daladala ni hivyo hivyo!
Lakini management nayo ni mbovu.
Hizi boats ziwekwe viti maeneo yote ili kupunguza nafasi za kusimama. Bila viti mnajenga tabia ya watu kuona wabanane tu potelea mbali.
Wengine ndiyo njia ya kuibia wenzao.
Watu wakishazoea kubanana huwezi kuwaambia boat imejaa!
Vinginevyo tuombe lisitokee la kutokea.
 
Nahisi serikali imetusomea albadiri na inatutoa kafara kimya kimya.

Nanutakuja kusikia kuwa TEMESA haiwezi kufanyia matengenezo ya mara kwa mara kwa sababu vivuko vinajiendesha kihasara.

Nchi hii hata aje malaika kuiongoza watamchakachua atake asitake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…