Kuna janga linaandaliwa vivuko vya Kigamboni, TEMESA chukueni hatua

Kuna janga linaandaliwa vivuko vya Kigamboni, TEMESA chukueni hatua

Imekwama wapi?
Picha
Screenshot_20220902-190231.jpg
 
Mjini hapa bila Dili hakuendeki.

Tengeneza tatizo wanaume waje kulitatua.

Toka Mzee WA Chato kuondoka naona kivuko kimefululiza kuharibika.

Hapa mpaka mtu apewe Tenda. Hela zinatafutwa anyhow.
 
Wakuu, jana na leo! Nimeshuhudia kitu kisicho cha kawaida wakati navuka kati ya Feri na Kigamboni.

Sijui kivuko ni kibovu ama vipi.

Tumepanda kikagoma kabisa kwenda, nafikiri tulikuwa wengi kupita kiasi.

Tukapunguzwa at least kikatembea kwa shida.

Yaani kwa sasa Feri ni shida kweli kweli.

Wasipochukua hatua kwa siku hizi ambapo vivuko ni viwili tu, lolote linaweza kutokea hasa nyakati za Asubuhi na Jioni.

Nawasilisha

Kuna haja gani ya kuwa na vivuko visivyo vya uhakika na usalama wake ni mdogo ikiwa serikali inaweza kujenga daraja zuri tu hapo na maisha yatakuwa rahisi kwa wakazi wa kigamboni. Tanzania bhana ni nchi fulani ya hovyo sana serikali inawatesa tu wakatwa tozo.
 
Back
Top Bottom