Kuna kidada cheupe pale TANESCO Mbezi Beach Afrikana nani anakipa jeuri namna ile?

Kuna haki ya kusikiliza upande wa pili na uchunguzi hivyo tumelipokea kwa kulifatilia wakati mwingine unakuta mtu katoa fedha kwa kishoka asiye mfanyakazi wa TANESCO ndio maana tunasisitiza kuchunguza
Mje na mrejesho sasa msisubir tuwaulizee
 
Kuna haki ya kusikiliza upande wa pili na uchunguzi hivyo tumelipokea kwa kulifatilia wakati mwingine unakuta mtu katoa fedha kwa kishoka asiye mfanyakazi wa TANESCO ndio maana tunasisitiza kuchunguza
Kishoka anakaa ndani ya ofisi ya umma,basi huyo kishoka ni mtumishi wenu
 
Acha kuharibia kazi watu wewe mjing.a.
 
Mkuu samehe tu,ungejua jinsi wanavyohangaika kuzipata hizo i phone series wacha nae alipize machungu kwa tozo ya picha.
 
Kweli vyuma vimekaza ,hela ya passport tu unampigia meneja?
Swali ambalo linahitaji Majibu kabla ya kukuunga mkono ama kukupinga ni je,
TANESCO wanatoa huduma ya kupiga picha wateja wapya iwe Kwa kulipia ama bure? Au ni mteja anatakiwa aje na picha zake?

Kama mteja anatakiwa aje na picha zake (Yani aambatanishe ktk fomu ya maombi) na huyo mdogo wako hakufanya hivyo ama aliambatanisha isiyotakiwa basi huyo mrembo Hawezi kumpa risiti kwasababu hiyo ni "kamradi"kake binafsi ka kusaidia wateja wasisumbuke kwenda studio na sio sera ya Ofisi
 
Wewe ulivyomjazia gallery ulitegemea nini? unataka picha ya bure simu ya babako?
hairuhusiwi mfanyakazi wa umma kutumia ofisi ya umma kufanya biashara binafsi. Nadhani ndiyo hoja ya mleta uzi... alikubali kupiga picha kwa kuwa alijua ni sehemu ya huduma ya ofisi na kwamba hata kama atalazimika kulipia inabidi apewe risiti ya malipo.
 
Taasisi zote za Umma ziwe na Account JF na kwingineko na ziwe Active Kwa kweli.Hongereni Sana Tanesco mnaupiga mwingi Sana kama Mama.Hamna jambo dogo.Na mpo karibu na Wananchi.Nimewapenda Sana na ninawapa hongera kitengo Cha mawasiliano.
 
Mkuu ungeniomba namba ya mtu flani tanesco. Huyo dada na meneja wake wangenyooka ndani ya dakika tano
Mkuu naomba hiyo namba PM maana TANESCO wanazingua nimeomba umeme mwezi wa tano huu unaelekea kuisha, nimejaza form lkn sijapewa control number kwa ajili ya malipo ya umeme ili waje kuniwekea kwangu
 
Hela ya picha bei gani? Mambo mengine sio yakulalamika, mbona leo nimetoa hela ya mipira hospital lakini sijapewa risit na mgonjwa kahudumiwa saizi tupo home. Sometimes usicomplicate Mambo jitahidi kuishi kadili ya mazingira.
Kupuuzia mambo madogo kama haya ndiko kumetufikisha hapa tulipo, mimi pia huwa napotezea lakini ukweli ni kwamba tunailea rushwa ndogo inayozaa rushwa kubwa zaidi.

Yesu akasema " mtu wa mshahara na aridhike na mshahara wake"

Watu waliotembea nje ya nchi za wenzetu wataniunga mkono kuwa...wenzetu wawapo ofisi za umma akikuhudumia vizuri na ukataka kumpa asante...hawezi kupokea hadi amuulize boss wake na akikatazwa anskurudia na kukwambia...no, thank you.
 
Hata mm nimesikitika sana, kibaya zaidi pale nilipoambiwa boss wake kashamkanya lakini ni jeuri!
 
Tunaendelea kuwasihi wateja wetu kujenga tabia ya kufata taratibu haswa za kufanya malipo yote ya Serikali kupitia namba ya kumbukumbu ya malopo yaani control number, malipo yote unayofanya nje ya mfumo sahihi ni uvunjifu wa sheria na taratibu
Je Tanesco mna utaratibu wa kupiga picha pps na kusafisha maofisi mwenu? Uchunguzi tuanzie hapa ili tujue nn na nn tunahitaji tofauti na hapo ni majungu ya mtoa taarifa
 
Je Tanesco mna utaratibu wa kupiga picha pps na kusafisha maofisi mwenu? Uchunguzi tuanzie hapa ili tujue nn na nn tunahitaji tofauti na hapo ni majungu ya mtoa taarifa
Tena ilinisikitisha sana, na nitahakikisha nafuatilia ili nipate na jina ikiwezekana na picha ya hicho kidada #TANESCO
 
Msikulupuke kuchukua maamuzi! Kama amefanya kosa kweli aonywe na kazi iendelee
Usiwafundishe TANESCO kazi. Wanajua wanachokifanya!

Wao ndio wanalo file la huyo dada. Je kama ameshapewa maonyo kadhaa?? Bado waendelee kumuonya tu??
 
Usiwafundishe TANESCO kazi. Wanajua wanachokifanya!

Wao ndio wanalo file la huyo dada. Je kama ameshapewa maonyo kadhaa?? Bado waendelee kumuonya tu??
Njia rahisi zaidi nikuwabana staff wenzake waliojilani naye! Kuwahoji kwa siri waeleze huyo dada ameanza lini hiyo biashara ya kusafisha picha, na anatumia mashine gani! # TANESCO
 
Yote kwa yote, sidhani kama ni sahihi kumuita mwanadamu mwenzio "Kile Kidada Cheupe nani anakipa jeuri"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…