gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,312
- 3,345
Wandugu Salaam,
Juzi pale hospitali Msoga Madaktari wamepokea mgonjwa aliekuwa anatapika na kuharisha Damu sana na haraka walipomchukua maelezo wakabaini jambo.
Huyu mgonjwa alipata tatizo wakati anatafuna mfupa wa kuku na bahati mbaya kipande cha mfupa chanye ncha kali kilimkwama kooni. Alihangaika kukisukuma kwa kumeza ugali kikashuka tumboni lakini nako kilishuka na kuchoma tena tumboni.
Madaktari mara baada ya kupata hayo maelezo haraka wakamuingiza mgonjwa chumba cha XRAY ili wajiridhishe ndipo waanze upasuaji lakini kwa bahati mbaya umeme ukawa mdogo mashine za XRAY zikashindwa kufanya kazi.
Madaktari walihangaika kupiga simu Tanesco wakaambiwa tatizo lipo kwenye Gridi wao hawana chakufanya. Waliambiwa huwenda tatizo likachukua siku tatu kutengemaa maelezo yakawakatisha Tamaa.
Madaktari walianza kubishana pale wampasue tu bila XRAY kwani mgonjwa alihitaji msaada wa haraka lakini wengine waligoma kwani miongozo iliwataka wathibishe kwanza kwa vipimo.
Madaktari wakaamua wamkimbize Tumbi lakini mgonjwa huyu alipofika tu Tumbi akafia mapokezi hakuweza kupata huduma.
Mh Riziwani Kati ya zile taa za barabarani na STANDBY GENERATOR kipi kilipaswa kitangulie Kabla ya kingine?Mmefunga mataa kila kona mtaani yenye thamani kubwa ambayo ingetosha kabisa kununua ma generator hospitali lakini mmeona zile taa zitaonwa na wengi hivyo mtapata kura.hivi nikiwaita ninyi ni wauaji mtakataa?
Kati ya halmashauri na Msoga hospitali ni wapi hasa mlipaswa muanze kufunga standby generator? Yaani mmeanza kufunga generator kwenye maofisi mkaacha kufunga sehemu muhimu, nawaambia ninyi ni wauaji.
Nataka niwaambie acheni siasa pembeni, tendeni kwa kuwatizama wananchi sio kutafuta kura.
Kifo cha huyu mgonjwa kimeniuma sana kwani hakikuwa na sababu.
Ujumbe huu umfikie mbunge wa Chalinze kokote alipo. Wenye mawasiliano nae binafsi plz mwambieni kuna mwananchi anamuhusisha kwenye hii kadhia.
Asante.