1. Kutokuwa na hoja makini na jadidi. Wamebaki na vijembe kejeli na majigambo
2. Mafunuo ya Polepole yanawabagaza vibaya sana na kuwaacha uchi.. Anaamsha hasira ya watanganyika
3. Wasombwaji kwa maroli kukaidi
4. Zomeazomea.. Ikifanikiwa kwenye kampeni moja tu huko kwingine itakuwa ndio ada!
5. Kufarakana kati yao.. Timu ya kampeni! Na hili litahusisha pakubwa kwenye mambo ya pesa! Mgao kutoaminiana
6. Uasi wa kizalendo toka kwa wananchi kama Polepole ataendelea kupasua majipu yasiyo na tiba
7. Tuhuma za kudhuriana kati yao
Kwa bahati mbaya mkuu 'Mshana Jr.', kwa mara nyingine chache sana sikubaliani na mada yako hii hapa leo.
Najuwa ni ya "kujipa moyo sisi sote" tunaokuwa na matumaini ya lolote litokee kwa hawa majambazi ili nchi yetu ipone.
Sababu zote ulizo zitaja hapo juu, hakuna hata moja inayo karibia kuwastua na kuacha uhuni wao huu wanaolitendea taifa hili.
Hawa ni watu walio pania kweli kweli; walio jipanga kwa lolote lile ili waendelee kubaki madarakani.
Hawa wapo tayari kutoa roho za waTanzania mradi wafanikiwe kuendelea na mipango yao.
'As long as', mitutu inayoshikiliwa na akina Jumanne Mulilo na wengine bado wameishikilia upande wao, hakuna lingine linaloweza kusitisha mipango yao. Hii ipo wazi kabisa.
Sasa hivi wanatumia mbinu zote: kuhonga, kutumia malori, kuhadaa; kutisha watu, n.k.; na yote haya yakishindikana, bado watajitangazia ushindi..., dalili zote zinatuelekeza huko na siyo "kusitisha kampeni"!
Kwa hiyo hili la kusitisha ondokana nalo kabisa akilini mwako.
Jambo pekee ambalo linaweza kuvuruga mipango yao ni uasi wa waTanzania moja kwa moja. Kukataa kila hatua wanayo ifanya hadi siku waliyopanga kujitangazia ushindi.
Litakuwa jambo jema sana kama sote tunaokataa upumbavu huu tukihamishia akili zetu kwenye kubuni mikakati ya kuwasaidia waTanzania namna ya kukataa kila hatua ya hawa majambazi kuendelea kuitawala nchi hii kwa nguvu.
Zipo njia nyingi sana za waTanzania kukataa, baadhi tayari umezitaja kwenye orodha yako hapo juu.
NO REFORM NO ELECTION, bado ni hai sana. Tusiipuuze.