Kuna kila dalili kuwa Tanzania waovu wameshashinda

Kuna kila dalili kuwa Tanzania waovu wameshashinda

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,503
Reaction score
15,858
1 Watu wanapochochewa kuchukiana kwa misingi ya makundi, maeneo, itikadi au maslahi badala ya kuunganishwa na haki na uzalendo.
2. Umaskini na mateso kutumiwa kuwatawala watu.
Huduma muhimu zinapokosekana, fursa zinapopatikana kwa upendeleo, au wananchi wanapolazimika kutoa rushwa ili kupata huduma wanazostahili.
3. Ukweli kuzamishwa na propaganda.
Uongo unaporudiwa mpaka kuaminika, ushahidi unapopuuzwa na watu wanaohoji mamlaka wanaposhambuliwa badala ya kujibiwa hoja zao.
4. Wananchi kukata tamaa na kuacha kudai haki.
Hii ni dalili inayostahili kuangaliwa kwa makini: watu wanapoamini kwamba kupinga ufisadi, kutetea haki au kushiriki katika masuala ya umma hakutabadilisha chochote.
 
Kwanini mkuu?
Mkuu, ukiwa na familia yenye watoto kadhaa, baba Bora ni yule anayesikiliza Kila mtoto hata kama mtoto mmojawapo anaonekana kana kwamba ni mkorofi au mjinga mjinga hivi, ila usimpuuze katika madai yake

Sasa, tuna viongozi na chama ambao hawapendi na hawataki kusikiliza wanaolalamika na kudai haki zao, ni CCM na viongozi wake

Kwao Kila anayelalamika ni gaidi au katumwa na mabeberu

Siku tukija kujua sote kwamba, viongozi wapo ili kutekeleza wajibu wao kwa wananchi, huu u CCM na UChadema utajifia na tutakuwa na viongozi Bora wenye uchungu na nchi Yao

Nyinyi watu wa CCM mmchangia kwa asilimia zote kuwagawa,kufukarisha wananchi na Kila migogoro mmeleta nyinyi

Na bahati mbaya kabisa, mna sikio la kufa, huko tuendako msipobadirika, hamnatakuwa salama nyinyi na watoto wenu

Bora umeanza kung'amua mapema
 
1 Watu wanapochochewa kuchukiana kwa misingi ya makundi, maeneo, itikadi au maslahi badala ya kuunganishwa na haki na uzalendo.
8. Umaskini na mateso kutumiwa kuwatawala watu.
Huduma muhimu zinapokosekana, fursa zinapopatikana kwa upendeleo, au wananchi wanapolazimika kutoa rushwa ili kupata huduma wanazostahili.
9. Ukweli kuzamishwa na propaganda.
Uongo unaporudiwa mpaka kuaminika, ushahidi unapopuuzwa na watu wanaohoji mamlaka wanaposhambuliwa badala ya kujibiwa hoja zao.
10. Wananchi kukata tamaa na kuacha kudai haki.
Hii ni dalili inayostahili kuangaliwa kwa makini: watu wanapoamini kwamba kupinga ufisadi, kutetea haki au kushiriki katika masuala ya umma hakutabadilisha chochote.
Umeiweka kama shairi flani safi nimependa uandishi wake
 
 
Haki na ukweli yanabaki kama maneno yenye kubeba maana ya haki na ukweli ila kwenye uhalisia hivyo vutu havipo ..Kiufupi , sisi wote ni wachafu ndio maana leo unadai haki yako huku unaenda kuvunja duka la mtu , hapo nawe umeharibu haki ya mwingine.

So , we tulia fanya kazi zako hata huko mnapopasifia wameua watoto kwa mabomu ila hawataki kuguswa ..Hkuna haki wal ukweli , ukweli uliopo ni lile jambo ambalo unapenda kulisikia kutokana unavyoamini ila neno ''ukweli'' linabaki kama neno ila sio uhalisia.​
 
Back
Top Bottom