Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ama kweli siasa sio uadui, na hakuna uadui wa kudumu kwenye siasa..
Wabobevu na manguli wa siasa za Tanazania wameamua kujitosa na kuchukua hatua za kuingilia kati ugomvi wa kisiasa na kutuliza vita ya maneno, kashafa na tuhuma za kisiasa baina ya F. Mbowe mwenyekiti wa chadema taifa na Mch.Msigwa kada wa ccm, ili kupata suluhu na muafaka nje ya mahakama..
'Hawa ni watu wanao fahamiana na kuheshimiana sana mpaka kwenye familia zao. Wamefanya kazi za siasa na kupitia changamoto nyingi sana wakiwa pamoja, tena kwa muda mrefu sana. Si sawa siasa hizi za kuchafuana zikaachwa zikaendelea kuharibu udugu, urafiki na siasa za nchi kirahisi hivi, na sisi wazee walezi tupo tunatazama tu, hapana, hilo haliwezekani. Tutachukua hatua. Tukishindwa basi, lakini naamini tutaweza, mtupe nafasi na muda kidogo tu. Mimi na wazee wenzangu tutawaita tuzungumze nao, na bila shaka yaliyopo mahakamani yataondolewa'..
Miongoni mwa wazee nguli wa siasa za Tanzania aliyejitosa kutuliza uhasama wa wangwana hao wa kisiasa alidokeza kwa kifupi bila kutaka kuongeza chochote..
Je, manguli hao watafanikiwa kuwaleta pamoja na kutuliza joto kali sana la kisiasa lililofikia hatua za kisheria mahakama na kurejesha urafiki na maelewano baina ya wangwana hawa wawili, walioheshimiana na kufanya kazi pamoja kwa muda mrefu, licha ya kutofautiana mirengo ya kisiasa kwasasa?
Una maoni gani?
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina