Kuna kila dalili nchi ikarudi mfumo wa chama kimoja: Ikitokea hivyo ni faida kwa nani?

Kuna kila dalili nchi ikarudi mfumo wa chama kimoja: Ikitokea hivyo ni faida kwa nani?

Nime refer bandiko lako la 2017..Lakini P. Kwa mtazamo wako unafikiri magufuli akifanikiwa kuuwa upinzani ifikapo 2020 Ndio njia bora ya kuweza kutuletea maendeleo? Na je hiyo Ndio njia pekee anayoiona ya kumuenzi Mwalimu Nyerere aliyependekeza kuwepo na vyama vya upinzani? Na je ni nini faida ya kuwa na vyama vya upinzani kwa maendeleo? Na ni hasara gani pia hivi vyama kuwepo nchini?
Nia ya Magu ni kukiua Chadema tu
 
Magazeti ?
Anayejua bill yoyote iliyopelekwa bungeni ikagonga mwamba sababu ya uwepo wa wapinzani au hoja binafsi iliyopelekwa na upinzani ikapita azitaje.

Upinzani usiodhibiti bunge ni sawa na kuwa kwenye chama kimoja tu.

Hizo RICHMOND sijui ESCROW kiuhalisia huwa ni minyukano ya ndani ya CCM kuelekea chaguzi na hao unaodai wanaibua huwa wanatumika tu kama loudspeakers kwa hiyo hata wasipokuwepo kuna platforms nyingi tu kama magazeti.

Kingine ni kwamba kifo cha chama kimoja hupaswi kukihusisha na kifo cha vyama vyote.

Chama Kikuu kikifa kinatoa nafasi kwa wengine wenye fikra mbadala ya kufanya siasa katika mazingira haya kuibuka tena wengi watakuwa haohao wasiopewa nafasi kwenye hicho chama kinachojifia.

Mtazamo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio ndio mahubiri yenu kila siku?,nafikiri mtafarijika sana,kama mliombea corona ije na ikaja (technically)

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunahubiri ukweli na wananchi mliowajaza uoga wa kuuwawa na green guard wanajua

Ndio maana mkafunga mikutano ya Vyama vya upinzani kwa uoga Corona imekuja kuwasaidia nyie ili mpate sababu ya kuzudi kuzuia Mikutano ya Siasa na sasa plan yenu ni kwenda kwenye uchaguzi bila ya kampeni ndio mnayopanga ila mtaumbuka vibaya
 
Hizo scandals aina ya RICHMOND zisizohusu mhimili uliojichimbia zaidi hata sasa magazeti yanatumika mbona!

Gazeti la Jamhuri na lile la Musiba yanatumika na yatatumika sana tu kuibua madudu ya team pinzani kuelekea 2025 kama yatakuwepo.
 
1. Hatuwezi kusema ni faida kwa Rais kwani kikatiba atamaliza muda wake na kupsha mwingine.
2. Serikali itapata ahueni ya bajeti, ruzuku za vyama vingine hazitakuwepo- hapa kuna hoja
3. Vyama vya siasa vitazua migogoro ya kikatiba na serikali, na huenda baadae vikapoteza uelekeo kwa viongozi wake wakuu kupata makesi lukuki.
4. Baadhi ya wananchi hasa walio wengi hawatapata ukweli wa hali halisi ya serikali , ikikumbukwa kashfa za richmond, escrow, nk ziliibuliwa na vyama pinzani.
Tuchambue zaidi hoja hii kwa manufaa ya wengi.

Hakuna kitu kama hicho hizo ni ndoto hawana pesa hawana jeuri nje ya kutegemea mabeberu kuishi kumbuka wamevuruga vyanzo vya ndani kwa ujuaji,walidhani wakisomesha watu namba wao watabaki salama.Aliyepewa kapewa hawezi pokonywa na mwanadamu mpitaji.
Pili hiki ni kizazi kipya kina global vision sio kile kilichopita ambacho nyerere alizifungia akili zao kwenye box ili awatawale
 
China ni chama kimoja na sasa ndio baba lao, angalia walivyoidhibiti corona, linganisha na nchi za Marekani na Ulaya, utaona chama kimoja ni faida,
Mbona Africa imeshindwa kwani vyama vingi vimeanza lini
 
1. Hatuwezi kusema ni faida kwa Rais kwani kikatiba atamaliza muda wake na kupsha mwingine.
2. Serikali itapata ahueni ya bajeti, ruzuku za vyama vingine hazitakuwepo- hapa kuna hoja
3. Vyama vya siasa vitazua migogoro ya kikatiba na serikali, na huenda baadae vikapoteza uelekeo kwa viongozi wake wakuu kupata makesi lukuki.
4. Baadhi ya wananchi hasa walio wengi hawatapata ukweli wa hali halisi ya serikali , ikikumbukwa kashfa za richmond, escrow, nk ziliibuliwa na vyama pinzani.
Tuchambue zaidi hoja hii kwa manufaa ya wengi.
Ni vema tupeleke katiba ya kurudisha chama kimoja.Hii katiba tuliyo nayo tunaikiuka kila kukicha.Je ni kwa faida ya wananchi wote au watu wachache?
 
Utarejesha vipi huu mfumo wakati katiba inasema ni nchi yenye kufuata mfumo wa vyama vingi?
Katiba yetu ilishapindishwa kwa mambo kadhaa na hayahojiki. Mfano; katiba inasema (ibara.......) Nchi yetu itafuata Siasa ya Ujamaa naKujitegemea ,na hili linahusu zaidi misingi mikuu ya Uchumi? Je, hali iko vile?
 
Duh...!, just do makes you happy, hupewi ban.
Huo ndio ukweli wenyewe, pole sana kwasababu ni ukweli mchungu ila ndio ukweli wenyewe.
P
Kama ni ukweli hauwezi kukaa na uongo hata siku mmoja kama upo kwa ajiri ya maslahi yako Kama samu mahela cypian musiba na akina lemetumuzi pambana utafika tu wakati ndio utasema tutaelewena tu
 
Watu kushindwa kuwa na sera na mikakati bora inayoweza kuchochea maendeleo sasa naona ni muda wa kutafuta visingizio.

Wanashindwa kuelewa kuwa toka mwaka 1965 hadi 1995 nchi ilikuwa chini ya chama kimoja (de jure one party state), pia wanashindwa kuelewa kuwa toka 1995 hadi sasa nchi imekuwa ni (de facto one party state i.e. multi party state in disguise)..

Kama chini ya hiyo mifumo maendeleo bado hayajapatikana, basi hayatapatikana kabisa hata tuki-switch to Monarchy. In fact, hatujawa na Multi Party Democracy ktk nchi hii na kilichopo ni Multi Party System in Disguise.
 
Huo mfumo wa Chama kimoja ni sawa na kuamka ukakuta nje hakupo! Hiyo democracy mkiivunja mtakua wageni wanani?
 
Watu kushindwa kuwa na sera na mikakati bora inayoweza kuchochea maendeleo sasa naona ni muda wa kutafuta visingizio.

Wanashindwa kuelewa kuwa toka mwaka 1965 hadi 1995 nchi ilikuwa chini ya chama kimoja (de jure one party state), pia wanashindwa kuelewa kuwa toka 1995 hadi sasa nchi imekuwa ni (de facto one party state i.e. multi party state in disguise)..

Kama chini ya hiyo mifumo maendeleo bado hayajapatikana, basi hayatapatikana kabisa hata tuki-switch to Monarchy. In fact, hatujawa na Multi Party Democracy ktk nchi hii na kilichopo ni Multi Party System in Disguise.
Ni nini kifanyike ili tuwe na real multiparty state? Funguka tafadhali.
 
Back
Top Bottom