Kuna kila dalili nchi ikarudi mfumo wa chama kimoja: Ikitokea hivyo ni faida kwa nani?

Ungekuwa correct kama ungeondoa maneno: "in disguise".
 
ikitokea hivyo tuombe Mungu tu aepushe wasiibuke mbadala wa vyama vya siasa - vikundi dizaini ya Alshabab, Bokoharam, nk.

Mungu apishe mbali CCM isibaki peke yake maana hali hiyo inaweza kupelekea kusambaratishwa kwa CCM yenyewe kwa mkono wa kibedui wa kina Bokoharam!!
 
Jiwe anahangaika kweli na vitu visivyo na faida yoyote kwa nchi,anaua upinzani ukimuuliza faida yake,hakuna zaidi ya hasara,kabomolea watu majumba,katumbua watu,kapeleka jeshi kununua korosho ukimuuliza faida yake hakuna.
 
Ni nini kifanyike ili tuwe na real multiparty state? Funguka tafadhali.
Lazima tuwe na katiba mpya itakayotenganisha kabisa mamlaka ya mihimili yote ktk nchi na itakayokuwa juu ya kila mtu (Supremacy of the Constitution).

Katiba itakayoweka mechanism ya Checks and Balances na pia ku-guarantee uhuru na haki mbali mbali za kiraia ambazo hazitolewi na katiba ya sasa na vile vile itakayotatua namna tume huru ya uchaguzi itakavyoweza kupatikana.
 
Ingependeza ukashauri pia hatua au njia za kupata hiyo katiba mpya.
 
China ni chama kimoja na sasa ndio baba lao, angalia walivyoidhibiti corona, linganisha na nchi za Marekani na Ulaya, utaona chama kimoja ni faida,
CHINA chama kimoja LAKIN mfumo wa uendeshshaji ni tofaut KAMATI KUU NDIO INA MENO KILA KUTU rais ni msimamizi tu wa yaliyoamuliwa na KAMATI kuu ya chama. Kwetu raisi ndio ana MENO wengine ni viazi tu ndio ss tunaferi hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingependeza ukashauri pia hatua au njia za kupata hiyo katiba mpya.
Watalaam wa katiba (Constitutional Lawyers) ndio waandaye hiyo rasimu ya katiba na hao watalaam tunao humu nchini, wanasiasa wapigwe kabisa marufuku kushiriki kuiandaa kwa sababu ambazo zinajulikana.

Zoezi la kuiandaa haiwezi kuchukua zaidi ya mwezi moja kwani haiwezi kuwa "Unique" kwamba ni ya kipekee duniani, wata-rely on templates na kufanya marekebisho pale inapobidi ili kukidhi mazingira ya Tanzania.

Pia ile ya Waryoba inaweza ikatumiwa kama rejea pale inapobidi. Kimsingi Tanganyika Law Society inaweza ikatumiwa vizuri kuiandaa hiyo rasimu na rais asihusike na hii katiba kwani katiba sio mali ya rais bali ni matakwa ya namna wananchi wanataka waongozwe.
 
Asante. Unao uzoefu wowote wa ama nchi jirani waliofanikiwa kwa staili hiyo bila kuhusisha vyama wala serikali husika (Raisi). Mfano Kenya,Zambia hata Malawi Vyama ndo vili- spearhead mabadiliko ya katiba zao.
 
Asante. Unao uzoefu wowote wa ama nchi jirani waliofanikiwa kwa staili hiyo bila kuhusisha vyama wala serikali husika (Raisi). Mfano Kenya,Zambia hata Malawi Vyama ndo vili- spearhead mabadiliko ya katiba zao.
Vyama vinaachia wataalam wanatengeneza rasimu, Kenya walifanya hivyo na sio wanasiasa.
Kuhusisha wanasiasa ndio kulikopelekea katiba yetu isipatikane hadi leo na rais akihusika ndio kabisaa haiwezekani kwani ni interested party.
 
Ikitoke hivyo wao wenyewe kwa wenyewe wataanza kuhujumiana na kuuana kwa kuogombea madaraka ya vyeo
 
Vyama vinaachia wataalam wanatengeneza rasimu, Kenya walifanya hivyo na sio wanasiasa.
Kuhusisha wanasiasa ndio kulikopelekea katiba yetu isipatikane hadi leo na rais akihusika ndio kabisaa haiwezekani kwani ni interested party.
Asante. Kwa mazingira na hali ya kisiasa inavyoendelea hapa nchini, unafikiri hili wazo lako linawezaje kuakisiwa na shughuli zikaanza? Unadhani TLS wanaweza kuanza bila platform na whistleblower(s)?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…