Kuna kila dalili Samia Suluhu atakuwa Rais wa muhula mmoja pekee, dalili hizo ni hizi...

Kisiasa mama Samia anatakiwa aegemee Kwa Magufuli, hlo kundi Lina mtaji kisiasa. Akienda upande mwingine wa Twitter, atapitia wakat mgumu sana.
Na ameshaanza kupita mule mule....wale ndio watakaoafiki bungeni muwa awe mgombea wa URaisi pekee
 
Hii ya chombo cha habari inafikirisha haiwezekani kila siku mkawa mnatuliza na ngonjera kama vile aliekuja hajacover nafasi iliowazi, hawa wanavyotangaza utadhani aliyefariki ndio aliyeinunua Tanzania kutoka kwa waingereza na wanataka tujiulize baada ya mmiliki kuondoka nani atasukuma gurudumu? Hawa watu waache uchonganishi Raisi Mama Samia anatutosha.... Na tulimsubiri sana kwa miaka 6!
 
Kuhusu TBC nadhani wanatekeleza ile dhana ya kwamba tupo katika 21 days za kuomboleza. Baada ya hapo tutawashangaa
 

Wapiga ramli wa kigiriki mbona mnafeli mapema? Shida kubwa tuliyonayo tunataka Baadhi ya watu tunaowapenda ndio wawe viongozi wakubwa nchini. So far hilo linaonekana gumu. Mshaanza kusema one term...wakati hakuna anayejua miezi miwili kuanzia sasa covid itaanzisha mashambulizi gani
 
Subiri amalize siku 100 kwanza. Hata ingekuwa ni wewe, within a week uvunje baraza la mawazir, uchague wengine, uchague makamu, upokee Report ya CAG, Ukague hazina etc..huwezi haya mambo hufanywa bila kukurupuka.
 
Maombolezo ni siku 21,je zimeshakwisha.....?! Mbona walimwengu hamna dogo....
 
Ndugu, uRais ni kama lango 1 kubwa hivi ambalo Mungu anataka kupitishia baraka zake kwa wamchao na pia shetani anataka kupitishia maovu yake kwa wanao msujudia. Hilo lango linagombewa na falme 2, sasa unatakiwa wewe binafsi kumwomba Mungu wako amlinde Rais ili shetani na mawakala wake wasiweze kuzuhiya au kuchelewesha mahitaji yako yanapotakiwa kupita ktk lango hilo, Ni muhimu sana kumwombea Rais ili shetani asimtumie kuzuia baraka zako na za watoto wako. Hii ni muhimu zaidi kuliko unavyo waza.
 
Wewe hebu acha maneno yako ya kukosa heshima. Nani aliyekwambia zanzibar ni inchi....?!

Nani kakwambia mama samia kuwapo hapo katika uongozi ni kosa au ni kunajisi jamuhuri ya muungano?!

Tanganyika na zanzibar vilijifia kifo cha amani na utulivu kwasasa tunatanzania......

Muungano una faida sana na tija kijamii kuliko udhaniavyo......
 
Ana 14 actually sababu hii awamu kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi ni ya magufuri si yake yeye.....
 
Hakuna hoja ya kuthibitusha kuwa atakuwa rais wa muhula mmoja

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Umeandika sana lakini hoja zako ni dhaifu mno.
 
Maombolezo hayajaisha ndo maana wanaongelea Magufuli kila wakati. Subiri yakiisha ndiyo utoe mawazo haya uliyotoa.
 
Atajua mwenyewe! Na wasipo pandisha tena madaraja wafanyakazi mwaka huu kwa sababu zao za hovyo hovyo! Za kununua ndege na kumuenzi yule dikteta uchwara, vita itaanza upya. Kwa sasa tunamvutia kasi.
Wafanyakazi wa serikali hatufiki 500,000. Na kati yetu asilimia 80 tulishapandishwa mishahara na vyeo tunapandishwa kama kawaida. Nyie endeleeni na propaganda zenu eti mishahara haipandi wakati hata ajira hamna.
 
Kwa katiba hii ya 1977 mtu akiapishwa kuwa raisi anaweza kufanya lolote hata kuwa raisi wa milele hivyo mama samia kuongoza awamu moja labda ni ubinadamu wake tu. Naona wtz bado hatujajifunza jiwe angetunyoosha pia Mungu ametupa nafasi ya kujtathmini kabla ya Moto
 
Watajuana wenyewe regime mpya na yatima (MATAGA) Binafsi ningependa tusiwe na serikali ya CCM kuanzia hata sasa!
 
Hivi mnakomaa na makundi makundi ni lini kulikua na makundi?
 
Kiukweli hata mimi ningependa amalizie hii ngwe iliyobakia,then tuendelee na utaratibu wetu 2025,mindset yake na mipango yake ilikuwa imejielekeza mpaka 2025 asijilazimishe kwenda mpaka 2030,ingawa simpangii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…