Kuna kila dalili Samia Suluhu atakuwa Rais wa muhula mmoja pekee, dalili hizo ni hizi...

Kuna kila dalili Samia Suluhu atakuwa Rais wa muhula mmoja pekee, dalili hizo ni hizi...

Mtachonga sana, mtatabiri sana lakini nchi haiwekwi rehani kwa Wazungu.
 
Ni wapi Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan alishatangaza kuwa alikuwa na nia ya kuwa Rais wa Tanzania au hata baada ya Kuokota hivi Embe Dodo na kuwa Rais amesema kuwa ameshaionja Asali Tamu ya Ikulu na Urais hivyo baada ya 2025 angependa kuendelea kuwa Rais?

Ukipitia Threads za Watu ( baadhi ) hapa JF na hasa Ujengaji wao pia wa Hoja utagundua ya kwamba Elimu ya Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni imezalisha na inaendelea Kuzalisha Watu Wapuuzi ( Mahayawani ) wa Kifikra watupu tu. Tunachojua ni Kuzusha 24/7.
Kwa Historian inavyoonyesha Marais wanaopokea wale wanaoishia njiani hupiga miaka 10, tazama Zanzibar

Na hata hivyo kuutaka Urais sio dhambi, ndio cheo cha juu kabisa cha siasa na kila mwanasiasa anatamani mungu ambariki siku moja
Usiwe kiazi kama unaona una akili sana kuliko level za JF basi ungeondoka kwenda kwenye wenye akili wenzako
 
Sasa kwani tatizo ni nini? Kwani katiba inasema kuwa kila raisi ni lazima aongeze mihula miwili au inasema kuwa raisi anatakiwa kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano? Ninavyofahamu mimi ni kuwa Raisi anapochaguliwa anatakiwa kuongoza kwa miaka mitano, na anaruhusiwa kugombea urais kwa mihula miwili. Hii haimaanishi kuwa ni lazima aongoze kwa mihula miwili.
Namaanisha kuwa 2025 CCM hawatampa ile automatic endorsement kuwa mgombea wao kwa awamu ya 2
 
Atajua mwenyewe! Na wasipo pandisha tena madaraja wafanyakazi mwaka huu kwa sababu zao za hovyo hovyo! Za kununua ndege na kumuenzi yule dikteta uchwara, vita itaanza upya. Kwa sasa tunamvutia kasi.
umedeliver mtaaalam au unataka tu kila mwaka madaraja yapandeee wakati mpango kazi wako tu hapo na opars kila mwaka mapengo na humit target.madalaja yasubili tu kwa sasa tunajenga nchi.
pambana kwanza kukamilisha mpango kazi na uwe na malengo yanayopimika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Obviously, atakuwa Rais wa muhula mmoja.

Binafsi sina tatizo na mama huyu. Nina mwamini na kwamba ktk kipindi hiki kilichobaki atafanya vizuri na kurekebisha mengi yaliyoharibiwa na Mwendazake.

Ni kwa sababu pia, wanawake kote duniani waliowahi na wanaongoza mataifa yao, hawana historia ya uongozi wa kibabe na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Hopefully, Mungu kamleta kwa muda mfupi tu ili kupoza makovu na maumivu yaliyosababishwa na uongozi hatari wa mwendazake ambaye kama angeendelea kuwepo, angelipeleka shimoni taifa hili zuri.

However, sababu kuu zitakazomfanya awe Rais wa muhula mmoja si uwezo wake binafsi, la hasha bali ni;

å Tukumbuke kuwa ameukwaa Urais si kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kwa sbb ya takwa la kikatiba, kwamba, Rais kafa na yeye ni VP na katiba inasema yakitokea mazingira haya, basi VP moja kwa moja anaapishwa kuwa Rais. Ndiyo maana kulikuwa na struggle za chini chini za kutaka kumzuia asiwe Rais kwa baadhi ya wahafidhina kulitumia Jeshi litwae madaraka ya uongozi wa taifa hili.

å Hoja ya Utanganyika na Uzanzibari. Hii ndiyo ishu kubwa kabisa. Hata mimi nakataa kabisa Tanganyika kuwa na Rais Mzanzibari. Tunataka Rais wa JMT siku zote na mara zote awe ni Mtanganyika kwa sababu Tanganyika ndiyo JMT na JMT ndiyo Tanganyika...

Tanganyika haiwezi kutawaliwa/kuongozwa na Raia wa taifa jingine. Huu ni udhaifu mkubwa wa Muungano huu wenye utata mwanzo mwisho.

Hizi ndizo push factors zinazoweza kwa 100% kumfanya huyu mama amalizie hii miaka minne na kisha asirudi tena. Na ofcoz better iwe hivyo!
fungu la kukosa ... waswahel wanassem kisebu sebu na kiroho papo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo gang la mwendazake wanampotosha kuendeleaa na maono ya mtu wao ni kumpoteza mama aisee, na Tena ikiwezekana miradi yenye hasara ka ndege sijui bwawa fyekelea mbali, mama aje na kipaumbele chake Cha kuinua uchumi na sector binafsi ili iajiri watu wengi, kuna swala la masilahi ya watumishi Basi Mei mosi hii awape kicheko Cha kuwapoza wafanyakazi ili kuanza na mwanzo mzuri na kupataa reception nzuri ya uongozi wake, so aje na kitu cha kukonga nyoyo za wananchi na kamwe asi dance beat za mwendazake atapotea.
Pia hao ccm wanaoimba beat za mwenda zake ni kuonywa Mara moja kuacha akishakuwa mwenyekiti, Sasa wimbo inakuwa ni awamu ya Samia pia aruhusu mikutano ya siasa na hao wabunge waliopewa ubunge waambiwe kabisa this time utapambana na upinzani na ukishindwa no mbeleko inakula kwako, so ccm wakiachiwa kupambanaa na upinzani huko majimboni watasahau power struggle kwa mama enemy atakuwa upinzani sio ccm wao kwa wao Kama walivo relax
Kabisa May Day aongezee mishahara! Atembelee nyota yake. Walioajiriwa serikalini waondokewe na machungu.
Asipotoshwe. Kuna waliokuwa hawamtaki awe Raisi, so watatumia kila mbinu ya fitina na unafiki wa kisiasa bora tu aonekane bogus.
Ajitenge yeye ni tofauti na mwendazake.

Itapendeza sana kama atairudisha sekta binafsi ishamiri, na kurudisha ajira mitaani.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Pili anaonekana hana ujasiri wa kulivunja baraza la mawaziri, japo kuna utata kuhusu katiba kama inataka ama haija lazimisha, lakini Samia ana discretion ya kuvunja baraza la mawaziri na ikajengwa hoja tu kuwa uamuzi wake ni sahihi, hii itamfanya aweke watu wake ambao ambao ni watiifu kwake na hata kama atabakisha wale wa Magufuli pia sio mbaya kwa kuwa pia anaend
Mlipenda Magufuli age,lakini hamkujiandaa na maisha baada ya Magufuli
Kwa sasa mmegeuka wapiga ramli na washauri waelekezi
Mtu hata wiki hajamaliza ofisini,ushaanza kutabiri atakua Rais wa Muhula mmoja!
 
Mlipenda Magufuli age,lakini hamkujiandaa na maisha baada ya Magufuli
Kwa sasa mmegeuka wapiga ramli na washauri waelekezi
Mtu hata wiki hajamaliza ofisini,ushaanza kutabiri atakua Rais wa Muhula mmoja!
Nijiandae na maisha baada ya Magufuli kwa sababu gani sasa, wakati awepo asiwepo habadili chochote kwenye maisha yangu binafsi..hizi ni opinion tu mzee kama zinakukera sepa tu, JF ni jukwaa huru
 
Kisiasa mama Samia anatakiwa aegemee Kwa Magufuli, hlo kundi Lina mtaji kisiasa. Akienda upande mwingine wa Twitter, atapitia wakat mgumu sana.
Hakuna kitu mkuu, wenye mtaji wa kisiasa ni wapi? Ni Hawa ambao hata kwenye majimbo yao hawana mvuto , ambao ata kufanya mikutano kwenye majimbo wanaogopa, ? Kumbuka wale wenye mvuto wa kisiasa 95% ni wale waliachwa kwenye kura za maoni, japo walikua washindi Sasa hao unafikili walikua kwenye kundi la jpm? Leo pole pole, BASHIRU anaushawishi kwenye chama kuliko mzee kinana,makamba ,Nape, nk na je waweza sema hii ilikua team jpm,?
Cha msingi mama ni kusimama ,apige kazi , weka tume huru, then apange Tim nzuri kwenye chama twende kwenye uchaguzi ,mazuri yake ndo yatampa kura za kutosha kushinda, au kushindwa kutokana na ubora wa sera za kila chama
 
Nnilikuwa najiuliza hili swali nikawa sina uhakika, ila kwa sasa kutokana na mambo yanavyoenda inaonekana wazi kuwa huyu mama atakuwa Rais kwa muhula mmoja tu.

Kwanza kabisa siasa sio Sayansi, haina exact jibu, upo upande ambao unaweza kutengeneza hoja Samia akawa rais wa vipindi viwili na pia upo upande unaweza kutengeneza hoja pia Samia akawa Rais wa muhula mmoja tu na waote wakaonekana sahahihi.

Samia Suluhu kama ana nafasi kubwa ya ku influence na kutengeneza hoja apewe mihula miwili lakini naona hilo ni ngumu kwa sababu hizi.

Kwanza Serikali yake bado inaitwa Serikali ya awamu ya tano, nikisikia wabunge na watu wengine wa siasa wakiongea bado wanaiita hii serikali ya awamu ya tano, hili halina jibu sahihi kama ni ya 5 au 6 lakini Samia anaweza ku influence ianze kuitwa awamu ya 6, kwa kuwa kuendelea kuitwa awamu ya 5 kunatengeneza picha kuwa anamalizia ngwe ya Magufuli na sio kuwa anaanza ya kwake.

Pili anaonekana hana ujasiri wa kulivunja baraza la mawaziri, japo kuna utata kuhusu katiba kama inataka ama haija lazimisha, lakini Samia ana discretion ya kuvunja baraza la mawaziri na ikajengwa hoja tu kuwa uamuzi wake ni sahihi, hii itamfanya aweke watu wake ambao ambao ni watiifu kwake na hata kama atabakisha wale wa Magufuli pia sio mbaya kwa kuwa pia anaendeleza miradi ya mtangulizi wake.

Tatu vyombo vya habari hasa TBC vinamfanya Samia aendelee kuwa kwenye kivuli ha Magufuli, TBC wao kutwa nzima, taarifa za habari kwa sasa ni Magufuli, hatukatai ni kuwa wanaomboleza lakini pia yapo mambo ya mama ambayo anayafanya yanatakiwa yapewe kipaumble na kuanza kupewa airtime, mfano ripoti ya CAG na maamuzi ya Samia aliyochukua yamepewa nafasi kidogo sana pale TBC, wao wanarudia hotuba za Magufuli tu, hawarudii kabisa hotub za Samia, sasa hili Rais mpya anatakiwa aliondoe endapo atataka awe rais wa mihula miwili na kuacha legacy yake na sio kuwa place holder president.
kwa nini unaangalia au kusikiliza TBC? tuanzie hapo kwanza
 
wewe kweli ni kilaza wa hatari yaani kutokuitwa awamu ya 5 au 6 ndio sbb awe wa awamu moja sijawahi kupata kuona mtu mpuuzi kama wewe

eti asipovunja baraza la mawaziri anakuwa wa awamu moja...ni dhahiri mmebinywa mapumbu mnaanza kuwehuka hovyo

kuwa wa awamu moja itategemea na performance yake pekee ndio sbb ya kuendelea au kutokuendelea na siohizo sbb mavi ulizozitoa
Mkuu kuna wengine jinsi zao hazina hayo mapumbu.Sasa hawa tuseme wamebinywa nini?
 
Katiba inamtaka na kumlazimisha Mh Rais kuongoza kutokana na matakwa yake lakini haimlazimishi kuchukua ushauri wa yeyote, ni hiari yake.

Kutokulivunja Baraza la Mawaziri ndio ujasiri wenyewe huo. Makamu wake katoka katika Baraza alilolirithi. Huu uitwe nini sasa? Zaidi ya kusema ni Mwanamke/Mwamama Jasiri kama yule Debora wa Biblia. Hakuwasikiliza nyie makuadi wa mijizi na mafisadi.
 
Ikifika 2025 atakuwa na miaka 65 ..Nani anataka raisi mzee .,.
 
Kwenye kampeni za mwaka jana mgombea aliuliza kwani yeye ana tatizo gani hadi awe Rais wa muhula mmoja? Akafanya aliyoyafanya uchaguzi ukaisha maisha yakaendelea. Mwenye pumzi yake kaichukua mwanzoni kabisa mwa mhula wa pili.
Tunasema yetu na Mungu ana yake.
 
Matukio mawili ndiyo yalikuwa yanadetermine future yake:

1. Uchaguzi wa VP(Ameshajichanganya).

2. Baraza la Mawaziri (Mtego mwingine huu).

Kingine kikubwa kuliko vyote, wanatakiwa waache kutembelea nyota ya JPM, mambo ya kusema "Tutaenzi na kuendeleza aliyoyaacha" hayafai na yanacompromise future yake.
Magufuli ana nyota gani sasa mpaka Samia atembelee nyota yake?
Samia anasimama yeye kama yeye na ndiyo maana kwenye hotuba 2 ametamka wazi kuwa namnakuu "Mimi ndiye Rais wa Tanzania mwenye jinsia ya kike".

Kwa sentensi hiyo ameweka msumari kuwa ile Jinsia ya Magufuli iliyokuwapo ndiyo tumefunga kitabu chake.
 
wtf?????

haha.jpg
 
Matukio mawili ndiyo yalikuwa yanadetermine future yake:

1. Uchaguzi wa VP(Ameshajichanganya).

2. Baraza la Mawaziri (Mtego mwingine huu).

Kingine kikubwa kuliko vyote, wanatakiwa waache kutembelea nyota ya JPM, mambo ya kusema "Tutaenzi na kuendeleza aliyoyaacha" hayafai na yanacompromise future yake.
Uchaguzi wa VP amjichanganya vipi, unadhani ange mchagua nani ambae kilamtu angesema amepatia.
 
Back
Top Bottom