Kuna kila dalili wachambuzi Wasafi FM wamemchoka Maulid Kitenge

Kuna kila dalili wachambuzi Wasafi FM wamemchoka Maulid Kitenge

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Kumekuwapo na sakata siku mbili hizi kati ya msemaji wa Simba, Haji Manara na mtangazaji wa Wasafi FM, Maulid Kitenge.

Hii ni baada ya Kitenge kupost kwenye page zake kwamba kuna ugomvi kati ya Morrison na kocha wake Gomes, na ndio maana Morrison aliachwa Dar safari ya Khartoum, madai ambayo Manara aliyakanusha na kumuonya Kitenge aache uzushi.

Leo katika kipindi cha michezo asubuhi, amehojiwa CEO wa Simba, akakanusha kuwapo ugomvi huo na akadai ni waandishi tu wanaotafuta followers kwenye pages zao ndio wanazusha hilo. Pia akahojiwa kocha Gomes kama ana ugomvi na kwa nini alimuacha Dar, akasema taarifa hizo si za kweli na Morrison ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ambaye atawasaidia sana Simba, na akasema alimuacha Dar kwa sababu za matatizo ya kifamilia.

Pamoja na ufafanuzi huo wa CEO na kocha mwenyewe, lakini bado Kitenge akawa anamlazimisha Zingizi aongelee ugomvi ili kuhalalisha habari yake ya mitandaoni, na wakati wakizungumza hayo, wachambuzi wengine wa soka akina Musa, Ambangile nk waliamua kupiga kimya kuwaachia Kitenge na Zingizi wakifarijiana kuwa CEO na kocha wamekanusha tu ila kuna habari wao wanazo, hadi ikafikia hatua ya Ambangile kuvunja ukimya na kuanzisha habari nyingine mpya.

Kitendo cha wachambuzi wenye akili zao kuamua kukalia kimya ushawishi wa Kitenge ili wasiwaamini CEO na Gomes kimenifanya nipate picha kuwa huenda waliona watajiondolea heshima kujadili kitu ambacho kimeshakanushwa, tena mmoja wa wakanushaji nihuyo huyo Gomes anayehusishwa na ugomvi!

Hongera Musa Kawambwa, George Ambangile na wachambuzi wote mliokuwapo studio kwa kumuachia Kitenge alibebe zigo lake, wala asiwasumbue, mpeni makavu!
 
Mikia kitenge anawanyoosha kwel kwel na bado
Huu ndo Ujinga wetu Yanga. Yaani tunaamini Team ambayo inaongoza kwenye Group CAF inanyooshwa na Mwandishi wa habari ambaye anaongea Upuuzi tu Daily?

Badala ya kuangalia team yetu inavyoyumba na kupoteza mwelekeo... sisi aliyeturoga atakuwa LUC EYMAEL . Jana tumepoteza points 2 na kumfukuza kocha na tunaacha ku concetrate kwenye mambo yetu tunalazimisha ya SImba. sisi akili tulipotezea wapi?
 
Huu ndo Ujinga wetu Yanga. Yaani tunaamini Team ambayo inaongoza kwenye Group CAF inanyooshwa na Mwandishi wa habari ambaye anaongea Upuuzi tu Daily? Badala ya kuangalia team yetu inavyoyumba na kupoteza mwelekeo... sisi aliyeturoga atakuwa LUC EYMAEL . Jana tumepoteza points 2 na kumfukuza kocha na tunaacha ku concetrate kwenye mambo yetu tunalazimisha ya SImba. sisi akili tulipotezea wapi?
Mkuu sisi yanga Kuna shida mahali mashabiki huku mitaan wanatia kinyaa wamesahau ya timu yao wapo na kitenge wakija kushtuka yanga itakuwa Kama Azam TU yaan jina kubwa ufanisi n hovyo

Naifananisha yanga na binti aliyekuwa anaringa ujanan akitaka kiolewa na wenye pesa matokeo yake kaishia kuwa single mother na uzee ndio huo unapiga hodi anabak kuringia uzur wa ujanani kumbe umr ushamtupa
 
Sio kweli mkuu bali ni hivi..kitenge amewameza wale madogo mle ndani yaan jambo analo tqka yeye ndilo lizungumziwe ukibishana nae itakupasa ukae kimya tu.

Na shida ya kitenge ni Unanzi wa kuipenda yanga. Binafssi nilimsikiliza shafii dauda leo ktk Hili game shafii alipasua JIPU leo na ule ndio ukweli. Shafii amesemaa wazi kabisaa wadhamini wale wa herufi tatu ndio shida maana wao ndio wana ratibu kila kitu ktk club ile na shafii alisema wazi ata maamuzi ya kumfukuza kocha M/kiti wa club na Makamu wake wote hawakuwepo.

Lwambano akaongezea akasema ndani ya club ya utopolo kuna wajanja wachache ambao wanaendesha maisha yao kupitia club ile wamejificha kwa mgongo wa mdhamini wa herufi tatu

Sasa kuamini hili binafsi huwa najiuliza iv ina kuwaje sponsor anaingia ktk vikao vya kuongoza club tena wao sio main sponsor mbona wale michezo pesa hawa play part kama mdhamini wa herufi 3
 
Huu ndo Ujinga wetu Yanga. Yaani tunaamini Team ambayo inaongoza kwenye Group CAF inanyooshwa na Mwandishi wa habari ambaye anaongea Upuuzi tu Daily? Badala ya kuangalia team yetu inavyoyumba na kupoteza mwelekeo... sisi aliyeturoga atakuwa LUC EYMAEL . Jana tumepoteza points 2 na kumfukuza kocha na tunaacha ku concetrate kwenye mambo yetu tunalazimisha ya SImba. sisi akili tulipotezea wapi?
Kwa kutambua ujinga wenu mkuu NAOMBA wewe nikutoe huko.

Wewe ni mwelevu ila upo kwenye kundi la wajinga.
 
Kitenge alikosea kitu kimoja toka mwanzo, aliacha unazi wake kwa Yanga ukue sana matokeo yake sasa hivi kila atakachosema kuhusu Simba hakuna atakaemuamini tena, ni rahisi sana mtu wa sampuli yake kutunga uongo ili awafurahishe wale wa kundi lake, na hiyo TV yake ya KitengeTv itatazamwa na utopolo wenzake pekee, sitaki hata kujua ina nembo ya aina gani.
 
Yaani kitenge amewafanya uto wajifiche kwenye kichaka chao cha kuombea/kusemea mabaya simba Ili mradi ubovu wa Timu yao usionekane
Kwakifupi kijora na Yanga yake wanasafari ndefu sana
 
Hata kama ugomvi upo, hawawezi kukiri kwenye media. Huo ndio uhalisia
 
Back
Top Bottom