Kuna kila dalili wachambuzi Wasafi FM wamemchoka Maulid Kitenge

Unaona Simba wapo sahihi kwa hili au umeandika ili ujaze page tu
 
Fabrizio Romano huwa anasema, wachezaji wamegombana na kocha?
Mara kagere ampiga kichwa kocha Sven?
Hivi hizi ni tetesi au lengo kuu ni kuwatoa watu mchezoni? Hasa katika ardhi yetu ya Tanzania ambapo kila kitu ni mtandaoni.
Mkuu,
Kuhusu hilo la mchezaji kugombana na kocha ni mara ngapi umewahi kusikia tetesi juu ya jose mourinho kugombana na wachezaji wake??? Mfano ndani ya chelsea 2016 ilisemekana kulikuwa na mgohoro..juzi lampard kaondoka lkn inasemekana kulikuwa na mgogoro..tetesi zipo..hazikwepeki..watu wenye weledi wanajua jinsi gani ya ku deal na tetesi

Iwe simba iwe yanga tetesi hazikwepeki..cha muhimu ni jinsi ya ku deal nazo lkn si kutishia waandishi wa habari
 
Wewe unawaza kama mm.. sioni cha kuwatoa mate wale jamaa.

Tetesi za kitenge zisitupotezee muda.
 
Watamchokaje wakati yeye ndo boss wao na ndo aliopambana kuwaleta wachambuzi pale redion?
 
Umeandika kama nilivyosikia.. Kongole Mkuu
 
Kitenge hajawahi kuipenda Simba...

Kitenge na Haji wanajuana hao, mambo yao waachieni wenyewe...
 
Sasa huo ndo mpira wa Yanga miaka yote. Its our philosophy. Na wachezaji wenyewe ndo hao hao...kwa sasa wachezaji wa maana hawazidi 4 wachezaji ndo uwezo wao. Huku kocha wa ngapi tunafukuza.
 
Naifananisha yanga na binti aliyekuwa anaringa ujanan akitaka kiolewa na wenye pesa matokeo yake kaishia kuwa single mother na uzee ndio huo unapiga hodi anabak kuringia uzur wa ujanani kumbe umr ushamtupa

[emoji23][emoji23][emoji23] mfanano umekaa vyema sana huu
 
Nyie huyo kanjibay wenu anajua nn kuhusu soka litimu lenu linashakua la familia ya mo
Ulishawahi kuona Mo anasafiri kwenda kufuata mchezaji nje ya nchi? Ulishawahi kuona Mo amebebwa juu juu kwenye kiti eti amewezesha usajili? Ulishawahi kuona washabiki wa Simba wanashangilia usajili badala ya ushindi?
 
Wewe unawaza kama mm.. sioni cha kuwatoa mate wale jamaa.

Tetesi za kitenge zisitupotezee muda.
Kitenge kwenye taarifa yake hakusema Tetesi, yeye ameandika kama shahidi namba moja.

Hii ni mbaya sana, kwasababu hakuna sehemu amesema chanzo cha habari, lazima kuwe na mashaka kwenye taarifa yake.

Hivyo huenda nia yake ni kuleta taharuki Simba SC, kwahivyo lazima apewe Onyo Kali Sana!
 
Anachofanya mo simba anatofauti gani na hao gsm tuacheni unafki watanzania,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…