carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Mohamed, ametoa onyo kali kwa kiongozi mmoja anayedaiwa kuwatishia vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Nasra amesisitiza kuwa chama hakitamwogopa kiongozi huyo na kiko tayari kuchukua hatua dhidi yake.
Akizungumza kuhusu suala hilo, amesema:"Tutakughulikia na hatutakuogopa. Unataka upendwe na kila mtu? Kwani wewe umekuwa fedha?"
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa chama kitachukua hatua za kinidhamu dhidi ya mtu yeyote anayesababisha usumbufu. Halikadhalika, ametoa wito wa kukomesha tabia ya kuwatishia vijana wanapokuwa kwenye majukwaa ya chama.
Chanzo : Chief Odemba