Kuna kiongozi mwenye Mamlaka Simiyu anatishia vijana wanaopinga mawazo yake

Kuna kiongozi mwenye Mamlaka Simiyu anatishia vijana wanaopinga mawazo yake

KwetuKwanza

Senior Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
127
Reaction score
245
Habari za Muda huu ndugu zangu na wanafamilia wa NYANZA FM COMMUNITY!?

Binafisi najua mko salama Kwa asilimia kubwa na niseme poleni kwa wenye changamoto mbalimbali zinazo wakabili.

Nimesoma maandiko na comment za watu wote humu kuanzia Jana asubuhi. Nishukuru na niwapongeze nyote mlioweza kushiriki mijadala migumu na Ile myepesi katika group hili la nyanza fm.

Kwanini nimeamua kuandika andiko hili!?👇

Ndugu na wanafamilia wa nyanza nataka kunena machache sana. Najua magroup haya yamekuwa na watu mbalimbali tunaojuana na tusiojuana. Pekee tunakuwa tumeunganishwa na group hili.


Binafisi Jana Muda wa saa mbili asubuhi niligundua Kuna jambo linaenda kutokea mbele ya chatting zilizo kuwa zikiendelea kwa sababu mzaha ulichukuwa sehemu kubwa kuliko seriousness.

Niwakumbushe ndugu zangu wanagroup binafisi kwenye Simu yangu nina magroup zaidi ya 50. Kuna magroup ninayochat kwa vitu sensitive TU. Na Kuna magroup ya kurefresh mind.

Kitu pekee kilichonishangaza Kuna mtu anachat kwa mzaha na kejeri na kutegesha ajibiwe na watu walio serious akijibiwa kulingana na alichoandika anachukia na anatoa maelekezo ya watu kuwindwa na hata kukamatwa kuwa wamemvunjia heshima. Halloooooh!!!!! Kwanini watu tunataka kutukuzwa utafikiri wao ni Waumbaji!!? Kuna vijana watatu wamewekewa mitego tayari ya kuwindwa na hata kukamatwa (sitegemei lolote litokee) kisa ni kumvunjia heshima kiongozi mwenzangu. Hii si sawa tunapaswa kujua humu watu hujibiwa kutokana na alichoandika ukiandika smart utajibiwa smart na ukiandika ujinga utajibiwa ujinga kama ulivyoandika.

Na kukinzana Mawazo na mitazamo sio dhambi hata kidogo ukitaka kila unalolisema wewe tulikubali sote huo utakuwa ni udhaifu mkubwa na utakuwa huna sifa hata punje la kuwa kiongozi Bora. Utakuwa Bora kiongozi tu.

Sifa hizi ukizikosa kama kiongozi ujue hufai hata ujumbe wa nyumba kumi.

1. Uvumilivu,
2.utu
3.uadirifu
4.kushaurika
5.kutokujikuza
6.kutodharau
7.kutokuwa na kiburi.
Hivi ni Moja ya vitu muhimu kwa kiongozi akivikosa vinavyoweza kumfanya angukoa la kiongozi yeyote duniani.

Kufikia kuandika hili nimepata taarifa za Karibu kuwa vijana hao watatu wanawindwa kukamatwa jambo ambalo si sawa hata kidogo. Viongozi tunaotaka tuogopwe sio kwa kukamatana na wanaokinzana na wewe, Wala wasio kushabikia kwenye vitu vya hovyo. Kitu pekee Cha kukuogopa ni kufanya vitu vikubwa kwenye eneo lako la utawala hata yesu hakuongopwa kisa ni Mtoto wa Mungu walimwogopa na kumheshimu kwa vitendo vikubwa vya uponyaji na kusaidia wenye changamoto.

Natamani tufanye mambo mazito sisi kama viongozi si mambo ya hovyo kama kutishia watu, na kunyima watu uhuru katika magroup ya kijamii, sisi tuna nafasi ya kufanya wabaya wetu wawe marafiki na sio kuwaadhibu ama kuwafunga maana hatutoweza kuwamaliza wasiotaka kutusifia na kukinzana nasi.

My take,
Kwa vile Kila taarifa tunayo dhidi ya vijana wasio tuunga mkono viongozi. Ni Bora kuachana na mpango wa kutaka kushinda jambo kwa ubaya .

Nishauri sisi viongozi wenye umri Mdogo, tunapaswa kufanya mageuzi makubwa kutoka kwenye mifumo ya kibeberu na kuja kwenye mifumo rafiki dhidi ya vijana Wenzetu.

Kwa sababu Bado tunasafari ndeeefu ya maisha hata kama utakuwa umeahidiwa uwaziri, ubunge tusitumie Nguvu ya kuumiza wengine ili kesho Yetu iwe njema. Hili litashindwa kwa asilimia kubwa na mikono yetu itakuwa imenuka udhalimu na damu za watu.

Usimkamate au kumtengenezea kesi MTU na usiendelee na hii tabia siku moja utaondoka kwa fedheha kubwa na hutokuja kuamini haya maneno.

#Mungu ibariki Tanzania,
#Mungu ibariki Simiyu,
#Mungu ibariki Bariadi.✍️

# Mwana kondoo ameshinda........🙏
 
Back
Top Bottom