Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Shukurani kwa ufafanuzi.....Ni Marehemu wa aina gani anastahili kuongozwa na Padri ama Askofu, na huyu anaeongozwa na Katekesta sifa zake ni zipi.?
Oh!!!,swali zuri sana Mkuu.Ktk Kanisa Katoliki Kuna muongozo wa Ibada ya mazishi uliotokana na Sheria ya Kanisa;Ambapo Marehemu yeyote ambaye aliishi ktk ushirika na Kanisa na MUNGU anapaswa kupewa Heshima ya kuzikwa kwa Misa Takatifu itakayoongozwa na padre au Askofu,lkn ktk mazingira ambayo padre au Askofu hayupo karibu basi Katekista anaweza kumzika mtu huyo kwa ibada maalumu ya mazishi ambayo itazingatia vipengele vyote muhimu vya Ibada ya mazishi ya Mkristo aliyeshirikiana vema na Kanisa.Sasa unawezaje kutofautisha Ibada iliyoongozwa na Katekista kwa Marehemu aliyekuwa mshirika mzuri wa Kanisa na yule ambaye hakuwa mshirika mzuri wa Kanisa??,Jibu ni fupi,yule aliyekuwa mshirika mzuri wa Kanisa ibada itafuata vipengele vyote muhimu, wakati yule ambaye hakuwa mshirika mzuri ibada itakuwa fupi sana,inaweza kusaliwa sala chache tu na Kisha kumzika,na hapa huwa inaangaliwa pia juu ya ndugu za Marehemu kwa nia ya kuwafariji na kuwaasa wasiwe km ndugu yao, Ndio maana km Marehemu hakushiriki ktk Mambo ya Kanisa na ndugu zake pia,uwezekano wa kukosa kabisa mazishi ni mkubwa, anaweza kuzikwa tu km mbwa au mzoga na Serikali au jamii yake.


Kimsingi Kanisa Katoliki halimtengi mtu,Bali mtu mwenyewe kwa akili zake timamu ndio anajitenga na Kanisa (Excommunication).

Muda si mrefu nitaweka hapa muongozo wa mazishi ktk Kanisa Katoliki.Kaa mkao wa kula.
 
Ibada ya misa ya mazishi inafanyika kanisani, nyumbani au hata uwanjani kama Taifa au Kalimjee, ila ibada ya mazishi makaburini makatekista wamekaimishwa kufanya ibada ya mazishi makaburi na ile siyo misa.

Wewe ni mkatoliki au mkristo wa wapi hujui vitu vidogo kama hivi?
 
Ndg hilo la sadaka mara7,na hiyo ten kwa buku2 labda lipo kwenu tu.Kwetu kuna sadaka ya kwanza na ya2 kwajili ya ujenz wa nyumba ya mapadre na uzio.Mkiona mambo hayaridhishi chukueni hatua kwa kufata utaratibu wa kanisa.
 
Achana nae mkuu huyo ni wale waumini kondoo haswa ambao kila akisemacho padre hata cha kipuuzi wanakunja mikono na kuitika ndio baba.

Hatukatai mchango ila iwe na mantiki na kusiwepo vikwazo kwa wasio na uwe zoo wa kuchangia viwango vinavyoweka.
Hiyo phrase ya Roma locuta causa finita ni udikteta wa hali ya juu wa viongozi wa kanisa Halafu wanatuletea eti kanisa la kisinodi.
 
Yaan jana nimepewa bahasha ya zaka.
Bado michango kedekede.
Naupenda mno ukatoliki lakini ni muda mrefu sana sijaenda. Nilienda jana kwqkua tu nasimamia ubatizo

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Restrictions unajipa wewe mwenyewe.Nyie watu wa ajabu sana,ujitenge mwenyewe halafu useme eti umewekewa restrictions!!!, Halafu kusema eti unawapa watu umungu,hivi wewe ungekuwepo enzi zile za Anania na mkewe Safira jinsi walivyokufa kisa kusema uongo mbele ya mtume Petro ungesemaje sasa??. Wakati ule sheria zilikuwa kali sana tofauti na sasa.Hebu Tafakari mwenyewe eneo ni la kwako umeliuza haya ukasema ngoja nijiwekee kahela kadogo na kanako baki ndio nipeleke Kanisani lkn mwisho wa siku unakufa,je,ungeweza? Km sadaka tu inakutoa jasho hadi kulia lia kwenye mitandao ya kijamii.Ukristo wa siku hizi ni wa kupenda dezo.
 
Huna lolote ulijuwalo, wakati Galileo anasema dunia ni duara nyinyi wahafidhina wa Vaticano si ndio mlimbishia na kusema dumia ni bapa huyu anakufuru?

Kiko wapi sasa Vaticano inakuja kumuomba radhi mtu ameshafariki miaka kibao baada ya kuijuwa kweli na kuishi kumpa heshima ya maktaba Vaticano ya Galileo Archives?

Wewe hakuna unalolijuwa katika kanisa hili kaa kimya.

Hivi Unajuwa baada ya recession iliyotekea miaka hiyo Vaticano ikaanzisha dhua na kutunga cheti cha maondoleo ya dhambi ambacho kilikuwa kinanunuliwa kwa pesa nyingi leo ndio mnadanganywa kwamba ni kitubio? Unayajuwa haya?
 

Ndg hilo la sadaka mara7,na hiyo ten kwa buku2 labda lipo kwenu tu.Kwetu kuna sadaka ya kwanza na ya2 kwajili ya ujenz wa nyumba ya mapadre na uzio.Mkiona mambo hayaridhishi chukueni hatua kwa kufata utaratibu wa kanisa.
Mkuu.Kwenye jumuiya haupewagi bahasha zozote halafu kuiwasilisha ni jpili kanisani(tofauti na ile tulioizoea ya zaka).Baada ya hyo sadaka ya pili ndo zinaanza kutajwa hzo bahasha ulzochukua kwny jumuia(hizi ndizo zimebeba uzi wa mleta mada)
 
Sikumbuki last time nimehudhuria jumuiya lini. Zaidi naonaga unafiki tu baina ya waumini. Yaan last week junuiya ilikua kwetu lakini i couldnt attend. Siwezi unafiki kwakweli. Kwanini nikasali na najua hatuko vizuri baina yangu na some people?

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Napokea ushauri, huku nikiendelea kuamini kuwa wajinga ndio waliwao.
Mimi ni Mjinga Namba moja,kwa Mambo yahusuyo MUNGU,acha Mimi niitwe Mjinga au vyovyote vile ili mradi wewe umerizika kuwa umenitukana, Kiufupi Tukana hadi roho yako ijisikie vizuri.
 
Hakuna mwenye hati miliki ya kuabudu wala ya ukristo wala ya ukatoliki.
Katafute historia ya kanisa, kanisa haliongozwi na watakatifu, RC ilishawahi kuwa na mapapa wahuni kupindukia, lakini waumini wakakomaa kuwatoa madarakani.
Hivyo tunao wajibu wa kukataa na kukemea pale kanisa linapotaka kujigeuza la kibiashara.

Sijui kama unafahamu kwamba Martin Luther alienguliwa (excommunicated) kwa kupinga kitubio kuuzwa kama bidhaa ili ipatikane pesa ya ujenzi wa St Peter's basilica

Haiwezekani Leo muumini hana uwezo lakini anaambiwa kama hujachangia kitu fulani ( vingine anasa) huwez kupata huduma fulani.
 
Mimi angalau Paroko wetu wa zamani nilimkubari sana maana alikuwa na utaratibu wa kuja vijiwe vyetu mtaani kututembelea kwenye mapub ajuwe tunaishi vipi kondoo wake na anazungusha round mpaka anaondoka hataki mumpe yeye offer anasema yeye ndio amewafuata mtaani ana ela yake.

Kiukweli nilimkubali sana paroko huyu kwa sasa amehamishiwa parokia nyingine miongoni mwa parokia zetu.
 
Hakuna anaelia kutoa sadaka ndg katekista, ninachopinga ni michango yenye uelekeo wa anasa na kuwaumiza bure waamini.

Nimekupa mfano wa parokia yangu Kinyerezi, nyumba ya mapadre ipo tulionunua sh 400M haina miaka 10.
Sasa wamekuja upya na mchango wa kujenga nyumba ya ghorofa eti ile haina hadhi.
Wewe unaona ni sahihi? Hao waumini wanaishi nyumba za namna gani?
 
Nakazia[emoji106]
Aisee m mpaka nashangaa hasaaa

Yni kikubwa wanachokukhofisha kanisani ni kua ukifa hawatokuzika hili haliingii akilini kabisaa sasa mtu akishakufa ata kumstiri tu mpaka utoe pesa ! dah kwa kweli inauma

Katika Uislamu tumeharakizwa kuzika tena Muislamu akifa.sehemu yyte ile ni jambo la kawaida tu hilo na mtu atazikwa vizuri tuu

M nawashauri watu tusomeni hizi dini mbili hlf tutaona ukweli ulipo bila hata ya kumurika kwa tochi
 
Umenena vyema kuhusu kutoa ulichonacho ili kuwezesha mambo yafanyike. Very nice. Lakini malalamiko yanakuja pale inapokuwa ni too much e.g. Idadi ya aina za sadaka; au Kutoa(Sadaka/Majitoleo) kwa kuzingatia vigezo i.e unapangiwa kiasi cha kutoa!
Ikumbukwe kwamba Sadaka ni ile itolewayo ndani ya Misa Takatifu ambayo ni moja tu - ile inayopelekwa na inawekwa chini mbele ya Altare/Madhabahuni kabla ya sala ya Utangulizi inayoanza na maneno "Salini ndugu ili sadaka yangu na yenu ikubaliwe....."
Hiyo mingine ni Michango na sio Sadaka. Sadaka haijawahi kuwekewa viwango na watu hawajawahi kulalamikia Sadaka.
Kwa hiyo kinacholalamikiwa ni Michango. Michango inalalamikiwa kwamba imekuwa ni mingi. Waumini Wakatoliki hawakatai au kulalamikia uwepo wa michango la hasha bali ni Idadi ya michango kuwa ni mingi e.g. kuna Mchango wa maendeleo ya Parokia, Mchango Zaka, MchangoTegemeza Jimbo, Mchango tegemeza Nyumba ya Mapadre, Mchango Vipaji, Michango midogo-midogo e.g.Bahasha ya Pasaka/Krismasi,Kampeni ya Kwaresima,Pango la Mtoto Yesu, Kuombea marehemu(Novemba) n.k. michango yote hiyo ni endelevu i.e. Inajirudia kila mwaka. Ipo michango mingine ya Dharura e.g. Ujenzi wa Cathedral, kumshika mkono Frater/Shemasi/Katekista akienda masomoni au kuhama,Kupokea Ugeni fulani, matengenezo ya gari, ununuzi wa kifaa au vifaa muhimu e.g. kinanda /generator n.k. hayo ndo yanalalamikiwa kutokana na kutokuwa na Annual Budget na Vipaumbele.
Naomba niishie hapo kwanza. Samahani kama nimemkwaza Mkatoliki mwenzangu.
 
Hiyo sio njia sahihi ya kushughulikia migogoro baina yako na jirani yako.Yesu alitoa muongozo wa namna ya kushughulikia migogoro hiyo ktk Mt.18:15-17, imeandikwa hivi.[emoji116][emoji116][emoji116]


Mathayo 18:15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
Mathayo 18:16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
Mathayo 18:17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.


Kwa hiyo,usiache kwenda kusali jumuiya au Kanisani kwa visingizio vya kitoto vya eti fulani amenikwaza au fulani na fulani hatuelewani.Huu ni ushauri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…