Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,355
- 14,408
Oh!!!,swali zuri sana Mkuu.Ktk Kanisa Katoliki Kuna muongozo wa Ibada ya mazishi uliotokana na Sheria ya Kanisa;Ambapo Marehemu yeyote ambaye aliishi ktk ushirika na Kanisa na MUNGU anapaswa kupewa Heshima ya kuzikwa kwa Misa Takatifu itakayoongozwa na padre au Askofu,lkn ktk mazingira ambayo padre au Askofu hayupo karibu basi Katekista anaweza kumzika mtu huyo kwa ibada maalumu ya mazishi ambayo itazingatia vipengele vyote muhimu vya Ibada ya mazishi ya Mkristo aliyeshirikiana vema na Kanisa.Sasa unawezaje kutofautisha Ibada iliyoongozwa na Katekista kwa Marehemu aliyekuwa mshirika mzuri wa Kanisa na yule ambaye hakuwa mshirika mzuri wa Kanisa??,Jibu ni fupi,yule aliyekuwa mshirika mzuri wa Kanisa ibada itafuata vipengele vyote muhimu, wakati yule ambaye hakuwa mshirika mzuri ibada itakuwa fupi sana,inaweza kusaliwa sala chache tu na Kisha kumzika,na hapa huwa inaangaliwa pia juu ya ndugu za Marehemu kwa nia ya kuwafariji na kuwaasa wasiwe km ndugu yao, Ndio maana km Marehemu hakushiriki ktk Mambo ya Kanisa na ndugu zake pia,uwezekano wa kukosa kabisa mazishi ni mkubwa, anaweza kuzikwa tu km mbwa au mzoga na Serikali au jamii yake.Shukurani kwa ufafanuzi.....Ni Marehemu wa aina gani anastahili kuongozwa na Padri ama Askofu, na huyu anaeongozwa na Katekesta sifa zake ni zipi.?
Kimsingi Kanisa Katoliki halimtengi mtu,Bali mtu mwenyewe kwa akili zake timamu ndio anajitenga na Kanisa (Excommunication).
Muda si mrefu nitaweka hapa muongozo wa mazishi ktk Kanisa Katoliki.Kaa mkao wa kula.