Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Mimi ni Mjinga Namba moja,kwa Mambo yahusuyo MUNGU,acha Mimi niitwe Mjinga au vyovyote vile ili mradi wewe umerizika kuwa umenitukana, Kiufupi Tukana hadi roho yako ijisikie vizuri.
Mbona mnapenda kumsingizia Mungu kwenye ulafi wenu?

Mungu hausiki katika hili, huu ni UAMSHO wa kukataa kutumia jina la mungu kubariki unyang'anyi na mbaya zaidi wahanga ni watu maskini ambao tegemeo lao pekee ni life after death, maisha ya duniani wameshapigwa tatu bila
 
🤣🤣🤣
 
Ni kwa nini unachaguwa verse unazozipenda wewe tu?

Tukumwagie verse za Biblia hapa kama haujakimbia kuhusu watu wanafki kama wewe? Hata shetani anayajuwa maandiko na alimjaribu Yesu kwa kutumia maandiko.
 
Umeshawahi kuwauliza Viongozi wako wa Parokia Kwanini wamechukua Maamuzi ya kujenga ghorofa badala ya nyumba mliyokuwa mmeinunua??. Inawezekana mahitaji ni makubwa kiasi Cha kudai ghorofa ijengwe.
 
Kila nikisoma comments humu ndani nazidi kupata ufumbuzi kuhusu wakristo wanavotapeliwa
 

Samahani, naomba nifahamishe, uendeshaji wa ibada au misa kikatoliki una basis 'mapokeo - maandiko' "kwamba: jinsi viongozi wanavyofanya ndivyo Yesu alivyokuwa akifanya au alivyofundisha kimatamshi na kimatendo?"

Zingatia: Utoaji sadaka ni moja ya kitendo
 

Kwa hiyo ibada inayoongozwa na Padri/Askofu na Katekesta kwa upande mwingine zinautofauti kwa sheria za Kanisa..

Kama kwa sheria ya Kanisa kuna utofauti kwa maana ya hadhi, vipi kwa upande wa imani huyo marehemu aliyeombewa na Padri /Askofu na Katekesta hadhi zao zinakuwa sawa mbele za Mungu.?
 
Mzee Matola,wewe Unaumwa ugonjwa wa Sonona,mada iliyopo mbele yetu ni juu ya Sadaka na Michango mbalimbali, Sehemu uliyoiquote ni jibu langu kwa muuliza swali kuhusu Taratibu za mazishi,sasa hbr ya Akina Galileo Galilei imekujaje hapa?,Oh!!,mara wewe Hujui kitu,kipi nisichojua kuhusu Kanisa langu Katoliki??, Sasa km kwa upeo wako umeona sijui Kwanini unaniquote na kutoa comment yako??.Anyway Jitahidi kupunguza mawazo ya chuki za kidini utaishi kwa furaha sana.
 
Ni kwa nini unachaguwa verse unazozipenda wewe tu?

Tukumwagie verse za Biblia hapa kama haujakimbia kuhusu watu wanafki kama wewe? Hata shetani anayajuwa maandiko na alimjaribu Yesu kwa kutumia maandiko.
"Kuwa kichaa sio lazima uokote makopo,hata kwenda nje ya utaratibu ni ukichaa pia".-
 
Kuna Parokia zingine Paroko anatembelea waumini majumbani mwao "kubariki" jumuia moja hadi nyingine then unampa the so called SHUKURANI.(kiwango chochote)

Ikitokea ukatoa kiasi ambacho kwa utashi wake Paroko akaona ni kidogo kutokana na hali yako ya maisha aliyoiona hapo kwako,anakataa mnaanza kupandishiana dau kama mnada wa Majembe Auction Mart.😁.

NB:Anaingia hadi ndani na ukizubaa hadi vyumbani!
 
Shida yote ya nini ndugu zangu si bora mje upande wetu waislam
Labda huko unakoishi wewe...

Huku kwetu Ni Yale Yale .. pesa za misaada..za yatima..za sadaka ..zinapigwa vibaya na ugomvi usiokwisha wa kugombea uongozi wa misikiti .. ..

Binadam ndiye bilisi...wa mwanzo...
 
Endelea kujiamsha wewe uliyelala na akili zako za kuazima.
 
Naunga mkono hoja. Hata Yes hapendi kinachoendelea Sasa kwa kutumia jina lake. Yes alikuja kuonyesha njia ya wanadamu kuishi kwa upendo ili siku moja tuwe wote mbinguni. Kuishi kwa kutokumtendea mwenzako kill ambacho hupendi yeye akutendee. Hi haihitaji pesa Wala sadaka. Sadaka mpelekee mhitaji. Mtu mwenye shida. Taasisi za kikristu yaani dini zimeanzishwa na watu wajanja kwa maslahi yao. Hao achana nao. Wewe kazania amri kuu ya Mungu UPENDO. Mpende Mungu kwa moyo wako wote na kwa akili yako yote na jirani yako kama unavyojipenda wewe. Japo Kuna watu wengine hawajipendi
 
Unapenda sana slope.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…