Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Suala la sadaka na zaka kwa karne hii naona inamantiki Sana kama utaitumia sadaka yako na zaka yako kusaidia wahitaji na wasiojiweza kuliko kutoa kwenye makanisa ambayo Sasa yamegeuka biashara. There are a lot of needy people out there wanahitaji msaada.
 
Ajabu Sasa ya wakristo, ulieleta hii mada Ni muumini mwenzao, lakini utashangaa wataanza kushambulia Waislamu na uislamu, jamaa Ni mazuzu!!
 
Labda huko unakoishi wewe...

Huku kwetu Ni Yale Yale .. pesa za misaada..za yatima..za sadaka ..zinapigwa vibaya na ugomvi usiokwisha wa kugombea uongozi wa misikiti .. ..

Binadam ndiye bilisi...wa mwanzo...
Sawa ila hatujafiki kutozika mtu kisa hakuwa mchangiaji sadaka msikitini au huko unapokaa wewe imetokea
 
Ukisema kiongozi wa Parokia kwamba anaweza kunipa majibu unakosea.
Unafahamu fika kwamba mambo ya kanisa ni up - bottom
Hiyo halmashauri walei inapokea maelekezo toka kwa paroko, wajibu wao ni kugawana majukumu ya utekekelezaji.

Halafu sina haja ya kumuuliza kiongozi au paroko kwasababu ilitangazwa kanisani sababu ni haina hadhi. Kwahiyo suala ni status sio uhitaji.
 
Utaratibu ambao sikubaliani nao ni huu wa usipotoa, basi hupewi huduma kama ubatizo na ndoa. Hili jambo kipindi cha nyuma halikuepo, sijui nani alianzisha. Sikuhizi kutoa sio moyo, ni kulazimisha.
 
Shukurani kwa ufafanuzi.....Ni Marehemu wa aina gani anastahili kuongozwa na Padri ama Askofu, na huyu anaeongozwa na Katekesta sifa zake ni zipi.?
Huduma ya Mazishi/Kuzika (kwa Wakatoliki) inaweza kuongozwa na MTU YEYOTE MKRISTU MKATOLIKI aliyepata kibali /idhinishwa kutoka kwa uongozi Mahalia kuendesha shughuli hiyo.. Lakini Huduma hiyo inapohusisha kuwepo kwa Misa Takatifu ni LAZIMA awe ni Padre au Askofu kwa kuzingatia Uzito/Sensitivity ya Shughuli yenyewe. e.g. Tukio limegusa vipi Jamii husika mathalan akifariki kiongozi mtu maarufu/Mwenye Heshima ya kipekee kiimani, Mzee, Mtu mzima mwenye familia n.k.n.k
Kama shughuli yenyewe itahusu Ibada tu ya Mazishi hiyo inaweza/ itaendeshwa na Katekista au Mtu aliyeidhinishwa na Uongozi Mahalia.
Kama hakuna Katekista, Uongozi (Padre kiongozi) Mahalia humwidhinisha mtu wa kusimamia na kuongoza shughuli hiyo kwa kuzingatia Uadilifu wake, Mcha Mungu (Bidii katika mambo ya Sala/ Kanisa) na anao Uwezo au Uzoefu katika shughuli hiyo.
Naomba kusahihishwa au marekebisho
 
Utaratibu ambao sikubaliani nao ni huu wa usipotoa, basi hupewi huduma kama ubatizo na ndoa. Hili jambo kipindi cha nyuma halikuepo, sijui nani alianzisha. Sikuhizi kutoa sio moyo, ni kulazimisha.
Hama Kanisa.
 
Basi km huoni haja acha kulalamika sasa.
 
Sawa. Nimekuelewa. Uko sahihi sana. Najipa nafasi kwanza. Nitakwenda pasi na shaka

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Nakazia hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…