Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Haha!kuna jamaa angu ana kisehem kutea copy na ku print...bac kuna jamaa kila baada ya mwez anakuja na kubadilisha tu figure na kuhamishia nyingine..kumbe jamaa anaombea msaada wa kujenga msikit huko singida ....huwa anazunguka sana Tz hii hadi viziwani huko...ila hakuna mchango anaopeleka zaid ya kufanya mahemezi ya familia yake tu....naona kwa ss iv kafanya kama ndo kaz yake
 
Nakuunga mkono asilimia mia moja braza. Mimi hapa nina deni la 500,000(Laki tano) nilipledge kwenye harambee. Nashauri utaratibu wa win win situation utafutwe ili waumini wasipungue kanisani kwa ajili ya michango. Ukienda kwenye Makanisa ya walokole ndo balaa.
 
Na Yale Maelfu kumi kumi unayoyaacha pale kaunta ya baa Kila wiki,mbona huyalalamikii.
 
Sema tunaweza kuchukia kutoa kanisani ila kwenye mambo mengine ya kawaida tunatoa bila kujiuliza
1.betting
2.kuhonga
3.bia,soda ,vilevi mbali mbali
4.kulipia kuangalia mipira
5.kwenda beach na kuspend hela
Mungu anatuhurumia sana kwa rehema zake ila binadamu sisi ni wabinafsi sana
 
Naupongeza Uongozi mzima wa Kanisa kubwa Bora ambalo mwanzilishi wake ni Kristo mwenyewe. Kanisa Katoliki Jimbo la Dsm kwa Kuwa nimeshuhudia mchango wenu pale mlipotuchangia parokia yetu kununua mali ilokuwa ikiuzwa kwa zaidi ya milioni 200.
Ahsante.
 
Wewe hama kanisa, dini au achana na dini kabisa. Haya ni malalamiko yasiyokuwa na msingi
 
Wangekuwa wanajenga hata hospital watu watibiwe bure ili kurudisha shukran wao kila siku michango na haiishi jamani
 

Hehehehe wizi kabisa
 

Ni wezi kabisa yaan kanisa halimisaidii muumini
 
Ndio Mjue Mnapigwa
 

Ehee na wenyewe wanawafaidisha nin?
 

Huendi kanisan kisa sadaka? Unahofia macho ya watu? Sio nzuri, Mungu akijua huna sadaka inatosha, lakin usiache enda Ibadan kisa sadaka, Hapo unakuwa hutoi sadaka cz utakuwa unafuata taratibu za ibada. Sadaka inatolewa kwasbb unampenda Mungu, (Moyo wa kupenda) lakin ukitoa kama taratibu za Ibada utalalamika Kila siku. Nenda Kaabudu usibaki nyumbani
 
Kama hujui mimi nilikuwq mnistrant mpiga chetezo ila hawa RC wamekuwa wazinguzi sana wahitaji unachanga tena na wakati sadaka ya pili ilikuwa ni kwenda kuwaona wahitaji in short hawa ma padre nao wamestuka wana familia tunalisha familia zao
Kuwa ministrant sio hoja.Kama wewe hutaki kutoa sisi wengine tutamtolea MUNGU maana kuna baraka nyingi ktk kutoa.
 
Kila mtu anataka atoe ili apate makanisa wao wanapokea na kujinemeesha wao Tu ingekuwa waumini wao wanalipa Ada pungufu kwenye mashule Yao au vyuoni au kwenye mahosspitali Yao wala wasingekuwa wanaumia ivi shule tunajenga pamoja na bado tunazidi kuiudumia Ila Ada kubwa kuliko kawaida gharama za hospital ndyo usiseme kwann watu wasilalamike
 
Pole sana.
Mimi nakuwa mkali sana kwa hawa viongozi wa dini wakina na haya mambo.
Kuna siku wale vijana wanajifanya wajuaji wameitisha kikao eti tutengeneze mfuko wa kusaidia maisha ya Mchungaji, hapo kumbuka ana fungu la kumi na mengineyo...niliwatolea uvivu, nikawaambia Yesu mwenyewe alikua seremala ili aishi,mchungaji atafute chanzo cha mapato.nadhani walimwambia maana upendo ulikata.
 
kweli dunia imekwisha!!
yaani muumini wa kanisa unalalamika kutoa sadaka?!
hujui umuhimu wa sadaka kwako binafsi na kwa familia yako?!

Elimu inahitajika juu ya Kutoa Sadaka ktk nyumba za ibada.
Hatulalamiki sadaka,Bali michango.

Watumishi wanaishi maisha ya anasa na pesa zetu.

Bora turudi old school, tunapeleka mazao na mifugo tunachinja na kuchoma moshi upande mbinguni. Sasa mapesa yote wanayaita sadaka wanaweka kwenye acc zao .
 
Mh ingekuwa hivyo basi pia wachamungu wa kweli wangekuwa wengi lakini tunaona watu wanadini ila bado wanafanya na mambo yenye kusababisha kwenda motoni.

Hilo unalizungumziaje?
dini imekuwa ni ya kutakatishia pesa,kujikomba na kujitafutia sifa mbele za watu
 
5. Washirika kwenda kusaidia kazi za mchungaji, iwe kilimo,ujenzi n.k

6. Nowadays, michango ya kuwanunulia wachungaji magari...ila sisi wanatuwekea mikono wakituombea tupate magari wakat wao wanachangisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…