Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

mchungaji atakula madhabahuni, kila madhabahu lazima uihudumie kwa sadaka mkuu, iwe ni kwa damu, nyama, nafaka, maziwa, pesa au kafara ya mtu. tafuta fundisho la mwakasege juu ya sadaka litakutoa gizani
 
Basi km huoni haja acha kulalamika sasa.
Katekista nimesema sioni haja ya kuuliza maana jibu limetolewa, nina haki ya kulalamikia jibu lililotolewa kwasababu ni anasa kwa makasisi huku wakiwakamua waamini ambao wengine hata kodi za nyumba ni shida achilia mbali kumiliki nyumba.

Makasisi waache ulafi na anasa, ni wajibu wetu kuwakemea maana walikuka kiapo mbele za Mungu na mbele za waamini (sisi)
 
Tangu niliposikia askofu kwenye maongezi yake eti kutoka mwanza kwenda musoma hawezi kupanda gari ila ndege tu ndipo nilijichokea mimi
Je, Alifafanua ni kwa nini? Huenda anamatatizo ya kiafya au labda nauli ya ndege ni ndogo zaidi ukilinganisha na ile ya Ndege au pengine ikiwa kuna kitu cha Haraka/Dharura kubwa mno. Lakini kama ni vinginevyo, basi alijikweza au alikuwa anapasha-pasha/anachangamsha (Energiser)mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea..
 
mchungaji atakula madhabahuni, kila madhabahu lazima uihudumie kwa sadaka mkuu, iwe ni kwa damu, nyama, nafaka, maziwa, pesa au kafara ya mtu. tafuta fundisho la mwakasege juu ya sadaka litakutoa gizani
AMINA
 
Aisee m mpaka nashangaa hasaaa

Yni kikubwa wanachokukhofisha kanisani ni kua ukifa hawatokuzika hili haliingii akilini kabisaa sasa mtu akishakufa ata kumstiri tu mpaka utoe pesa ! dah kwa kweli inauma

Katika Uislamu tumeharakizwa kuzika tena Muislamu akifa.sehemu yyte ile ni jambo la kawaida tu hilo na mtu atazikwa vizuri tuu

M nawashauri watu tusomeni hizi dini mbili hlf tutaona ukweli ulipo bila hata ya kumurika kwa tochi
Mkuu umenikumbusha kuna siku nimeudhuria mazishi sehemu asa misa imefanyika baadae mda wa sadaka mimi nkajipinda nkatoa sadaka yangu nzuri tu nikijua inaenda kuwasaidia wafiwa,ngachoka!naambiwa sadaka anaondoka nayo padri!
 
Siku hizi mamilooo, usipotoa ni kosa kwani wanaangalia registaa, hivyo huduma za kikanisa kama vile ubatizo, ndoa nk haupati.
Kwani watoto wasipobatizwa wanakwama wapi mi kuna mguso ninao kuwa haya ma dini wanatutishia MUNGU ili watukamue.Siku hizi ukikwama na ukaenda church kuomba msaada wa hata chakula hawakupi ila wao wakati wa mavuno wanachagua eti mpuka kuanzia debe mbili as if tulisaidiana hela za mbolea
 
Mkuu umenikumbusha kuna siku nimeudhuria mazishi sehemu asa misa imefanyika baadae mda wa sadaka mimi nkajipinda nkatoa sadaka yangu nzuri tu nikijua inaenda kuwasaidia wafiwa,ngachoka!naambiwa sadaka anaondoka nayo padri!
Huo ni utaratibu wa Kawaida Mzee.Sadaka ya ibada au Misa ya Mazishi inatakiwa aondoke nayo mwadhimishaji kwaajili ya kwenda kumuombea misa ya wafu huyo Marehemu, rejea 2Wamakabayo 12:38-44.
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
Milele Amina mkatoliki mhenga mwenzangu,


Umeandika hoja moja muhimu ambayo kama huna mihemuko ya dini utaona ni kiasi gani ukristo wetu unatoka kwenye imani.

Binafsi huwa nashangaa na jinsi polepole tunavyokuwa brainshwashed kuwa kutoa kuwa direct relationship na kuingia mbinguni au luwa mkristo bora. Naamini kubwa la kupata kwenye misa ni mahubiri, maelekezo yatakayonifanya niwe mkatoliki mkristo bora then niwe mtu mwema na nisaidie kwa kadri ninavyoguswa.

Leo hii tuna michango hii ambayo inaandikwa majina na ukikosa kila mtu anakutolea macho; sadaka, tuna zaka , tuna tegemeza jimbo, wawata, uwaka, utoto mtakatifu , viwawa, mavuno ( hii tunayo kwetu), shukrani ya mwaka ( tunayo kwetu), bahasha ya mtoto Yesu krismas, bahasha ya pasaka, mapaju jumuia ikihudumu kila familia elf 10, ujenzi wa kanisa ( letu tunachangaga ujenzi since 2005 _ 17 yrs back) na halijaisha.

Jumuia tuna mchangonwa familia kila mwezi , sadaka ya jumuia jumamosi .

Hizi ni fixed ila kuna zile adhock askofu anatembelea tumpe zawadi, gari la mapadri , nk nk


Sawa kanisa linategemezwa na waamini but come on tusiwe vipofu hivi to what extent??? Mbona kanisa hili halitoi kwa waamini? Na bado hakunaga usawa hata msemeje hakuna usawa - uwe na mgonjwa anataka sacrament ya wagonjwa utapita mlolongo huo balala. Hao wanaoniita makatekista ndio wakwanza kuwa warasimu .
Nimewahi kuomba mtoto ninaemlea miaka 6 agongewe muhuri tu alitaka kijiunga seminari dah nilienda pale parokiani mara 4 , nikaulizwa mambo yasiyihusiana na issue husika ( je namlea kivipi, je yuko kwenye sensa ya waamini na nimemtolea mchango wake - hamtaamini ila it was pathetic nilimjibu katekista na padre vubaya sana kuwa kama issue ni muhuri naweza kuchongesha ila kwa kujali ukristo wa mtoto nimefuata taratibu.

In short viongozi hawa wakatoliki wasioobadilika wajue wao ndio kikwazo kikuu na sababu ya waamini kukimbia kanisa na andiko linasema ole wake anaesababisha makwako kwa wengine.

Kuna siku jumuia yetu ilikuwa na zamu yanusafi na jumapili yake kupeleka mapaji ...hii ya mapaji nayo imekuja miaka hii ya 2000 zamani haikuwepo ; wasio wakatoliki mapaji ni kama mayai,sabuni, mahitaji ya kutumia mapadre ina week ( najiulizaga kama tunatoa sadaka iendeshe nyumba ya mapadre mapaji ya nini ila ndio kwa ufinyu wetu ukiuliza unaambiwa una lucifer kichwani) now back to the story, katekista akatuma ujumbe kuwa mapaji tunayopelela yawe ya aina fulani sabuni, mayai nk , nilitafakari sana tumefikia hapa mapadre au katekista anachagua sio mbaya sawa ila alikuwa aki dictate na brand za margarine, cooking oil. Tukumbuke kanisa ni kimbilio la wanyonge je wale wahitaji kanisa lina give back vipi kwao. Miaka 2 nyuma tulikuwa na harambee ya kununua gari la mapadre waumini wakasema tununue Rav4 ,mapadre walikataa wakataka navara tukasema jamani parokia iko mjini na inahudumia wanaparokia kwanini hawataki rav4 - we never won na prado lilinunuliwa. I can go on and on ila tuna tatizo kubwa sana kanisani.

Hiinya kupangiana sasa zaka ,eti nijaze form na mshahara wangu ndio naona mpya kanisa, who brough us here ? Nijaze napata laki 2 ,so kanisa linadai elf 20 bila kujali nina mama mkwe, wategemezi, watoto ,nk nk . Wanasema fungu la 10 ni strickt asimilia wanasahau tuna operate in a complete different environment ya tozo kila pahala.

Binafsi naipenda sana imani yangu ila nakwazwa sana na behavior ambazo zinaonekana ni strategy kuwba kuanzia juu hadi chini. Inakera zaidi wanapoogopesha waamini kuwa kutoa ni tiketi ya ukristo bora ,kuzikwa ni ishara njema , watasema ooh marehemu alilipenda kanisa ,what nonsense?? Bora waseme marehemu alisaidia majirani hata kama alikuwa mpagani.

Uzi huu usomwe na makasisi warekebike ,wanatukwaza kwa. Kwa kiwango cha juu sana. Kizazincha vijana chipukizi kinakuja na reasoning power na wasipoangalia watakosa waamini.

Sijui tunashun
 
Je, Alifafanua ni kwa nini? Huenda anamatatizo ya kiafya au labda nauli ya ndege ni ndogo zaidi ukilinganisha na ile ya Ndege au pengine ikiwa kuna kitu cha Haraka/Dharura kubwa mno. Lakini kama ni vinginevyo, basi alijikweza au alikuwa anapasha-pasha/anachangamsha (Energiser)mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea..
No!no!hana hadhi ya kupanda gari
 
Huo ni utaratibu wa Kawaida Mzee.Sadaka ya ibada au Misa ya Mazishi inatakiwa aondoke nayo mwadhimishaji kwaajili ya kwenda kumuombea misa ya wafu huyo Marehemu, rejea 2Wamakabayo 12:38-44.
Hichi ni kitabu gani tena maana najua vilikuwepo vitabu 66 hiyo wakabayo imetokea agano gani tena,turudi kwenye mada hiyo sadaka anaondoka nayo padri inaenda jimboni ama?
 
Back
Top Bottom