Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kule Buza kanisa la Anglican lilikuwa na mamia ya heka, wamepiga mpaka basi, nadhani ndio kilichomng'owa Askofu Mokiwa na sasa Askofu mkuu wa Zanzibar Michael Hafidh anaundiwa zengwe ili ang'olewe, maana Anglican Zanzibar ina vitega uchumi vya maana na vya kitalii.
Mmh.. ...

Kwa huyu ndugu ... ... Ni Bora apumzike ...
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
Kwa utafiti nliyoufanya, kanisa lenye maadili na linalosimamia misingi ya Bible na Kristo wa kweli ni kanisa la kisabato, haya mengine ni business oriented.
 
Naupongeza Uongozi mzima wa Kanisa kubwa Bora ambalo mwanzilishi wake ni Kristo mwenyewe. Kanisa Katoliki Jimbo la Dsm kwa Kuwa nimeshuhudia mchango wenu pale mlipotuchangia parokia yetu kununua mali ilokuwa ikiuzwa kwa zaidi ya milioni 200.
Ahsante.
Parokia gani
 
Nadhani mtoa mada bado uko enzi za wafadhili wa kanisa. Kwasasa kanisa linajiendesha,kama ufadhili unapatikana kwa bahati sana. Hivyo usipotoa unasababisha anguko la kanisa. Tutoe,tujenge vyakwetu. Wakati wakufanyiwa haupo tena.
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
@matol fwara kweli wewe😆😆😆 ....umenichekesha!

Sie Walutheli siku hizi Matangazo wakati wa Ibada 98% yanavinasaba vya kuchangia hela!

60% ya mida wa ibada watumishi wataongelea na kuhubiri pesa tu!

Ni only 5% ya ibada ya nyimbo za TUMWIMBIE BWANA za kitabuni tu ndio huimbwa kwa wote kanisani, asilimia iliyobaki ni nakwaya tu ya kila namna wanacheza kama Mfalme Daudi alivyomwangukia mke wa Uria akiwa myoni anaoga! (Watoto wetu hawajui hata nyimbo tatu tu za kitabuni)

Inaudhi sana. Yani unatoka nyumbanj walau ukapate neno la faraja kanisani, huko unakutana na wachungani wajasiriamali wanakukamua mpaka dah!
 
Makanisa yote mkuu kitakacho kuokoa ni imani yako

Hakuna aendae kwa baba bila kupitia mimi
 
Kwa utafiti nliyoufanya, kanisa lenye maadili na linalosimamia misingi ya Bible na Kristo wa kweli ni kanisa la kisabato, haya mengine ni business oriented.
Wazee wa hesabu sio wakristo!

Hamjawahi kuwa wakristo ninyi ni part ya waislam!
 
Nadhani mtoa mada bado uko enzi za wafadhili wa kanisa. Kwasasa kanisa linajiendesha,kama ufadhili unapatikana kwa bahati sana. Hivyo usipotoa unasababisha anguko la kanisa. Tutoe,tujenge vyakwetu. Wakati wakufanyiwa haupo tena.
Ni wapi niliposema watu wasitowe sadaka na matoleo? Unaelewa lakini kinacholalamikiwa hapa ni nini?
 
Mkuu pengine Kanisa Katoliki limechelewa sana kuwaamsha waumini wake.
Kwanza Mungu anatenda, tena kwa uwezo mkubwa sana.
Miujiza yake huwezi kuion kwa macho, lakini ipo n inafanya kazi.
Sisi waluteri tuna simamia katika kitabu cha

Haggai 1: 1-14

1Katika mwaka wa pili wa Dario mfalme, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake Hagai nabii, kusema,
2 Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya Bwana.
3 Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,
4 Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?
5 Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
6 Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka.
7 Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
8 Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana.
9 Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake.
10 Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake.
11 Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono.
12 Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hayo mabaki yote ya watu, wakaitii sauti ya Bwana, Mungu wao, na maneno ya Hagai nabii, kama Bwana, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za Bwana.
13 Ndipo Hagai mjumbe wa Bwana, katika ujumbe wa Bwana, akawaambia watu, akisema, Mimi nipo pamoja nanyi, asema Bwana.

14 Bwana akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya Bwana wa majeshi, Mungu wao;

Mkuu katika Neno hilitoka kwenye Biblia, waluteri wengi wame barikiwa kwa kutii amri ya Bwana kumjengea Kanisa la kumuabudu.
Nasema hivi maana nami baraka hii nimeipata over the 25 years ambazo nilishiriki kujenga nyumba ya Bwana.
Nikwambie kitu, dunia hii kati ya wafia dini na wafuasi wa shetani ni wafuasi wa shetani ndio wenye mafanikio nadhani ndio huko kubalikiwa usemako.

Hii dunia uchumi mkubwa unamilikiwa na mashoga na wamebarikiwa mno.

Verse kama hizi endeleeni kuzitumia kuwalaghai maskini ili muendelee kuwapora hata hicho kidogo walichonacho.
 
Kwa kweli michango na sadaka zinakimbiza watu makanisani. Tena wakifahamu ni muajiriwa au unakipato kikubwa bahasha inakuja ikiwa imeandikwa jina lako kufadhili shughuli za kanisa. Hatari kwa kweli
 
@matol fwara kweli wewe[emoji38][emoji38][emoji38] ....umenichekesha!

Sie Walutheli siku hizi Matangazo wakati wa Ibada 98% yanavinasaba vya kuchangia hela!

60% ya mida wa ibada watumishi wataongelea na kuhubiri pesa tu!

Ni only 5% ya ibada ya nyimbo za TUMWIMBIE BWANA za kitabuni tu ndio huimbwa kwa wote kanisani, asilimia iliyobaki ni nakwaya tu ya kila namna wanacheza kama Mfalme Daudi alivyomwangukia mke wa Uria akiwa myoni anaoga! (Watoto wetu hawajui hata nyimbo tatu tu za kitabuni)

Inaudhi sana. Yani unatoka nyumbanj walau ukapate neno la faraja kanisani, huko unakutana na wachungani wajasiriamali wanakukamua mpaka dah!
[emoji23][emoji23][emoji1787] Pigweni kwani mlilazimishwa kwenda huko
 
Back
Top Bottom