Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Itazame hali yake kwa jicho la kiroho utagundua kitu
Akalewa sifa , akapotea. Sasa ndo anatumbukia shimoni kabisa. La sivyo, abadilike na kujiona ni mtu mzima.Ameshasemwa sana kwa ubaya ameshaandikwa sana kwa ubaya ameshakuwa na kashfa nyingi...ni wakati sasa wa kumwangalia kwa jicho la tatu.
Hatuwezi kumweka kwenye kundi la malaika wa kifo kwakuwa wapenzi wake wengi bado wako hai. Ni binti mwenye nyota kali ya mafanikio kwake na kwa wapenzi wake pia na nyota yake hii ilichanua mapema kabisa hata akapata mafanikio mengi kwa muda mfupi na akiwa bado mdogo.
Nyota yake bado inawaka lakini imechezewa imefanyiwa kitu kibaya Wema wa bahati sasa ni wema wa mikosi nuksi na balaa.
Habari zake za kuandikwa kila siku kwa mabaya zimemfanya achukiwe na wengi bila kufikiri zaidi..nilikuwa mmojawapo na nikasema ni utoto akikua ataacha...mabinti wengi wamepitia hiki kipindi hata hapa JF tunao.
Wema amejijengea maadui wengi kuliko marafiki, Wema amekuwa centre ya habari kwa lolote afanyalo au linalomtokea iwe kwa ubaya au kwa wema
Lakini hebu tujirudi na kujitafakari upya...
Tabia ya Wema ya sasa ina mahusiano ya karibu na makuzi yake na hasa malezi ya mama! Je tuna la kujifunza hapa?? Tukumbuke na sisi ni wazazi.
Wema wa sasa anaporomoka kuanzia mwili shepu mahusiano nk nk...wengine wengi wamepitia haya lakini yakapita yakaisha, ya Wema hayaishi kila uchao tatizo liko wapi? Je haters wake wamefanya yao kwenye ulimwengu wa giza?
Wema anahitaji faraja ya kila mmoja sasa, kila dakika na kila sekunde pamoja na mapungufu yake yote lakini bado ni binadamu kama sisi mwenye hisia maumivu na roho ya nyama.
ASAIDIWE!
hivi wema ana matako makubwaNi kumpa Wema promoshen ya bure tu. Wanaume wengi tuna ugonjwa wa kupenda matako makubwa. Hakuna kitu kilichoharibika hapo, ingawa ni picha ya kutengenezwa.
Bi Kidude alishafariki, unataka tumjadili vipi sasa?Kinachomuweka wema juu ndio hicho ulichofanya mshana... Unamuandikia wema uzi???? Si bora tumdiscus bibi kidude
PMkuu Paskali first page nimeona like yako nikajikuta nafika mpaka page ya 7 si kwa kuifutlia hii
Mkuu
mshana jr,
you have a point, na kiukweli nimeguswa!, huyu dada 'has powers', she uses her powers and misuses them kwa kujijua au bila kujijua!, she needs help na sio ridicule!.
Mungu amsaidie!.
Paskali
Kwa wasiojua kuhusu powers, karibuni mnitembelee mitaa hii
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila kujiua!.
thread la hasha bali nijue maoni yako kuhusu huyu binti...I lost my time kupekua pages na sijaona comment yako zaidi ya ma likes tu! For god sake weka maoni yako hapa