Kuna kitu kina nguvu katika urembo na uzuri wa mwanamke.

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Siamini eti ni mihemuko ya kihisia ndio inatufanya tu babaike na urembo wa mwanamke maana hata mwanamke mrembo anatamaniwa hadi na mwanamke mwenzake.


Tangu hii dunia ianze tumeona jinsi mwanamke mrembo alivyowadondosha watu wazito na mataifa mazito. Hakuna mwanamke mrembo masikini hapa duniani. Ushawishi wa urembo wake utamfanya afikie viwango ambvyo siivyo vya taaluma yake na amavyo visivyokuwa vya haki yake.


Mwenyewe hapo umempangia mchepuko na kumfungulia biashara. Ni kitu ulichokifanya ambacho hukutegemea kukifanya maishani mwako lakini ulipokutana na energy kali kutoka kwa uzuri wa huyo hawala basi ukatuliza ubabe wako woote.


Uzuri mkali wa mwanamke ni nyota yenye sumaku kali. Wanawake wazuri wametumika kuwakamata waharifu, kufanya utapeli na kufanya mitego mingi iliotengeneza manufaa kwao na kwa wanaowatumia


Nyie angalieni miji midogo mnayoishi alafu muangalie wale pisi kali ambazo mliwahi kuzijua. Mtagundua zimeamia miji mikubwa yenye fursa kubwa na yenye mabwana wenye bank accounts nene.


There is something powerful kutoka kwa mwanamke mzuri. Biashara zinategemea muonekane wao katika matangazo, huko insta watu wanatangaza maduka yao kupitia mabinti warembo, mabenki wanawatumia kwenye reception na mabaa na lounges ndio usiseme.
 
PICHA MOJA TU INATOSHA UMEWEKA NYINGI
 
Jibu lako liko kule mwanzoni mwa mada yako.uko kwingine umepiga tu porojo.Nikwambie sasa kua hakuna mwanamke ambaye sio mrembo.Wanawake wote duniani ni warembo ila sio wanawake wote duniani ni wazuri.Kinachotusumbua ni hizo hisia.Hisia ndizo zinazofanya uthaminishe kitu.Ndo maana wewe ambaye hisia zako zimetekwa kwake kwa mwingine niwakawaida sana,au ukishakaa naye hisia zikamzoea utamwona wa kawaida.Mwanaume kaumbiwa udhaifu kwa mwanamke.kwahiyo tunamwangalia mwanamke kwa macho ya udhaifu wetu wa ndani.udhaifu unaowasha hisia na tamaa.Tamaa ikishakokea hapo ndipo shida inapoanzia.Tamaa itakufanya ufanye chochote na wanawake warembo ambao ni wajanja kwasababu wanajua udhaifu wetu wamekua wakiutumia vizuri kujineemesha.
 
ulipokosea n uliposema hakuna mwanamke Mrembo alafu maskini...Embu tembelea Kondoa...karatu...hanang uone mabint warembo wapo tu wanachunga mbuzi
 
Your browser is not able to display this video.


She is a full package, thick and beauty 😍.
 
Kama vitabu vya dini tu vinakubali kuna wanawake wameumbika vzr sana kuliko wenzao we unabisha na siasa za kila mwanamke mrembo!!!!
 
Nimeipenda philosophy yako,umetoa majibu karibu yote ya maswali ya ,mtoa ,mada. Ila inahitaji utulivu wa msoma kukuelewa kwani umetumia constructs kujenga deep philosophy yako e.g urembo na uzuri, tamaa na hisia.kuangalia mwanamke kwa mcho ya udhaifu, tamaa inakufanya ufanye chochote. Hii imetulia nategemea utakuwa na background ya physchologia kwa mpangilio mzuri wa kimantiki
 
kuna energy fulani inayojizalisha ndani yetu hasa kupitia hisia,maneno/kauli,miguso nk uzuri ni kitu cha fasta na haraka kuwepo na kutoka ila kuna nguvu ya maneno na vitendo ndiyo inayobomoa tawala au heshima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…