Kuna kitu kinakosekana Simba sc

kombaME

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
2,115
Reaction score
2,818
Simba ni timu yenye wachezaji wakubwa na wazoefu wa ligi lakin wengi wao ni kama sijui hawana morali, utaona wanavyoenda kukaba ni kama tayari wana goli 5, hakuna ule uharaka katika kutengeneza nafasi.

Simba hii sio ya kushindwa kuifunga yanga ambayo haina Kamusoko, Tambwe wala Naroub, huku simba ikiwa imetimia kabisa.

Something is missing, ni tofauti kabisa na vile mashabiki walivyoibeba simba kwenye vichwa vyao, mashabiki wa simba daima huwa wanatarajia makubwa na ni tofauti na kile wanachokipresent simba uwanjan, ukimsikiliza Manara utaona hilo, simba imebebwa kwa ukubwa sana vichwani vya wanasimba lakin performance yao uwanjani haifiki hata 50% ya kile ambacho wanasimba wanavyofikiri juu ya timu yao.

Tuseme either mfumo wa Mwalimu au something else kinawafanya washindwe kuperform kwa kadri wanavyotarajiwa simba kufanya wakiwa uwanjanj..

Naweza kusema,simba wako fiti psychologically kuliko technically, psychologically wapo relaxed na ndicho ambacho atleast kinawasaidia kupata matokeo, but performance yao hakika huwezi kuiona bill 1.3 hata kidogo.
 
Timu inakosa muunganiko.
Mwalimu ameshindwa kuwa inspire,kuwapa mbinu za ushindi,anashindwa kuwatumia wachezaji.
Kama alivyoshindwa kumtumia Ajib na akaruhusu aondoke.
Nashangaa Simba Kwa nini wameshindwa kumuamini Mayanja,kumkabidhi timu?
Mayanja ni zaidi ya Omog.
 
Tatizo la simba ni bla bla na mikwala mbuzi mingi, sitashangaa kama na msimu huu wataukosa ubingwa, yaani ni mwendo wa maujanja ujanja tuu yanayo kuja kuwa cost mwishon
 
Shabiki ana majukumu mawili tu
1.kushangilia na
2.kuzomea

mtu hata draft hujui kucheza,leo unajifanya kocha

wabongo tuheshimu taaluma za watu
 
Hujiulizi kwanini mara nyingi timu inapokuwa pungufu huwa ngumu au hushinda?
 
simba kama njombe mji tu sema manara anaikuza sana na washabiki wana amini ubingwa wao. sitashangaa wakienda FIFA tena
 
simba tulikosea kumuacha Ajib aende amin nakwambia boko simba si saizi yake na huyo gyan tuliambiwa ni hatariiio yuko wapi???
 
simba tulikosea kumuacha Ajib aende amin nakwambia boko simba si saizi yake na huyo gyan tuliambiwa ni hatariiio yuko wapi???
Ajibu alikataa kusaini Simba Sports Club, kwa sababu alichukia kuwekwa benchi au kuanzia benchi.
Mkude naye alitaka kuondoka kwa kukataa kukaa benchi.
Mimi nasema, chini ya kocha Amog, ubingwa wa ligi ya VPL tutausikia kwa jirani tu.
Amog hana jipya lolote zaidi ya kulinda ajira yake.
Azam walikatisha mkataba wake baada ya kuona hana kitu cha maana katika kazi yake ya ukocha.
Mimi naisubiri Simba ya baada ya Amog kuondoka.
 
simba kama njombe mji tu sema manara anaikuza sana na washabiki wana amini ubingwa wao. sitashangaa wakienda FIFA tena
Bingwa wao wa kuandika barua hewa FIFA yupo Keko
 
hat hivyo we ukiangalia kuna wa kumuweka benchi ajibu pale... haya tujulishe huyu gyan tuliyeambiwa ni hatari yu wapi
 
Simba wanaponzwa na kuwapa uongozi wajanjawajanja wanawachezea akili na wenyewe wanakubali wanaaminishwa wamesaini kwa 2B,Gyan bonge la striker wakati anawekwa benchi had na Luizio hapo inapigwa 10%,wamesaini wachezaji ili kufurahisha washabiki tu sikuona kama Niyonzima alikua anahitajika kwa Simba yenye Muzamiru,Ndemla,Mo Ibra,Ajib,Kotei na Mkude ila Rage alishawaita Mbumbumbu acha waburuzwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…