Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Hili sio bandiko la kila mtu, ni bandiko la wale tuu wenye jicho la 3 na sikio la tatu.
Leo Rais Samia, akiwahutubia maofisa ugani, Ikulu ya Chamwino, kuna kitu Rais Samia amekisema kuhusu uchaguzi mkuu wa 2025, pale aliposema atarejea lini Kizimkazi. Rais Samia ameuzungumzia uchaguzi wa 2025 not expressly but impliedly
Juzi kati nilipandisha bandiko humu nikiuliza kuhusu Wasaidizi wa Rais Samia kama wanamsaidia kwa kumwambia ukweli Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..?
Kauli hiyo ya Rais Samia sio tuu ina maana kubwa sana kwa uchaguzi wa 2025 tuu, bali ni kauli ya uthibitisho bado kuna wasaidizi wa rais, ambao hawamwambii Rais Samia ushauri wa ukweli kuhusu mambo mbalimbali ukiwemo urais wa 2025.
Mimi ni miongoni mwa watu wanaounga mkono urais wa JMT 2025, twende na mwanamke Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Nimewasisitiza watu wenye uwezo wa kusaidia, wasaidie, kwa kumshauri Rais Samia ushauri wa ukweli wa urais wa 2025.
Mimi pia ni miongoni mwa watu hao wenye uwezo wa kusaidia, na nimeisha saidia kwa kutoa ushauri wangu kusaidia taifa langu.
Kwa upande wa CCM nimeeashauri katika bandiko la sauti HII
Na kwa upinzani pia nimewashauri Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli 2025, Iachane na Urais, Ujikite Serikali za Mitaa, Ubunge na Udiwani, Urais labda 2030!
Kauli hiyo inaonyesha Rais Samia tayari ameisha hakikishiwa na watu wake, kuwa 2025 rais ni yeye, hii maana yake ni rais wetu wa 2025 tayari tunaye, yupo na ameisha chaguliwa, (amechaguliwa na nani?), hivyo siku ya uchaguzi ni kumthibitisha tuu!.
Hivyo nashauri, wale wenzetu ambao ni Presidential hopefuls wa urais wa JMT kwa uchaguzi Mkuu wa 2025, nawashauri save your time and money, rais wa JMT 2025, tayari tunaye!, zoezi la upigaji kura za urais uchaguzi wa 2025, sio kumchagua rais bali kukamilisha tuu taratibu za takwa la kikatiba kuwa uchaguzi ni kila baada ya miaka 5, hivyo hata kama rais tayari tunaye, bado tutapiga tuu kura sio kumchagua rais bali kutimiza tuu takwa la kikatiba la kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano hata kama uchaguzi huo sio uchaguzi, bali ni igizo tuu la uchaguzi kumthibisha tuu rais aliyepo!. Swali kama hili pia nililiuliza kabla ya uchaguzi wa 2020 Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Tena nimewasikia watani zangu fulani wakisemezana kumsimamisha jembe lao, jibaba la shoka na shujaa wao, nawashauri wamsimamishe mgombea mwanamke, wanawake ndio wapambane, maana jibaba dume la shoka kushindwa na mwanamke, si ni itakuwa ni aibu sana?. Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!
Nawatakia Jumamosi Njema
Paskali