Katika utekelezaji wa mpango huu
, Serikali imefanya makubwa yanayoonekana katika sekta mbalimbali za uchumi wetu. Ufanisi huu umedhihirisha kuwa MAMA ni kiongozi bora, mchapakazi, mwaminifu, mbunifu, muadilifu, mzalendo na mwenye nia na maono makubwa ya kuleta ustawi wa Taifa na maendeleo ya watanzania.
Haya Makubwa ni yepi hayo?
Shabaha na Malengo ya Bajeti 12. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2024/25, Serikali ililenga kufikia malengo na shabaha za uchumi na bajeti ambapo, mwaka 2024 Pato halisi la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 5.5 ikilinganishwa na lengo la asilimia 5.4.
Suali hapa imekuaje Uchumi umeporomoka kutoka kati ya asilimia 6 na 7 ya kati ya mwaka 2015 na 2020 hadi sasa kwenye asilimia 5.5 na hata lengo bado kuwa chini la asilimia 5.4
Hususan kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi za nje na zinazouzwa nje ya nchi ili kuongeza ajira na kuboresha mgawanyo wa vipato kwa watanzania. Kutokana na utekelezaji wa sera hizo, nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa ilipungua kufikia dola za Marekani milioni 5,157.2 mwaka 2024 kutoka dola za Marekani milioni 6,032.3 mwaka 2023.
Suali hapa ni je, ni bidhaa zipi zaingizwa nchini na pia ni bidhaa zipi zauzwa nje ya nchi?
Pili, je kipato cha mtanzania leo ni kiasi gani kwa mtu mmojammoja?
Mapato na Matumizi
Mwenendo wa Mapato 13. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2024/25, Serikali ilipanga kukusanya jumla ya shilingi trilioni 50.29 kutoka katika vyanzo vya ndani na nje. Hadi Mei 2025, kiasi cha shilingi trilioni 45.07 kimekusanywa, sawa na asilimia 89.6 ya lengo la mwaka.
Wakati Matumizi
Mwenendo wa Matumizi 21.
Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaliyoidhinishwa na Bunge lako Tukufu kwa mwaka 2024/25 ni shilingi trilioni 50.29 ambapo shilingi trilioni 33.75 ni matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 16.54 ni matumizi ya maendeleo. Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025, ridhaa ya matumizi iliyotolewa ilikuwa shilingi trilioni 42.90, sawa na asilimia 85.3 ya lengo la mwaka.
Sasa, hapa inakuwaje mapato yawa sawa na matumizi yaani yakusanywa trilioni 50.29 na matumizi ni trilioni 42?
Na hapa:
22. Mheshimiwa Spika, kati ya kiasi hicho, ridhaa ya matumizi ya shilingi trilioni 30.63, sawa na asilimia 90.8 ya lengo la mwaka ilikuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Aidha, ridhaa ya matumizi ya shilingi trilioni 15.74, sawa na asilimia 95.1 ya lengo la mwaka ilitolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Ridhaa ya matumizi ya maendeleo inajumuisha kiasi cha shilingi trilioni 3.47 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo ambacho kilipelekwa moja kwa moja kwenye utekelezaji wa miradi (D-Fund).
Kwa maana hiyo serikali yatumia pesa yote inoipata katika mapato yake. Je hiyo ndo sababu serikali yakopa sana pesa nje?
Tukumbuke ni lazima serikali iwe yaangalia mapato na matumizi yake.
23. Mheshimiwa Spika, baadhi ya maeneo yaliyopelekewa fedha katika kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025 ni pamoja na: ugharamiaji wa deni la Serikali shilingi trilioni 11.16; ugharamiaji wa mishahara ya watumishi wa umma shilingi trilioni 10.27; na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 shilingi bilioni 741.5. Aidha, kwa kutambua mchango wa wakandarasi, wazabuni na watoa huduma katika kujenga Taifa, Serikali imeendelea kulipa madeni yaliyohakikiwa ambapo kiasi cha shilingi trilioni 1.01 kimelipwa. Ulipaji wa madeni haya umesaidia kulinda mitaji na kuchochea shughuli za kiuchumi nchini.
Kwanza hapa inakuwaje serikali ya CCM yajitengea fedha za walipa kodi shilingi bilioni 741.5 kwa ajili ya uchaguzi ambao tiyari CCM wenyewe wamejiandaa kushinda?
Kwanini CCM isiwe na vyanzo vyake vya mapato?
27. Mheshimiwa Spika, Machi 2025, kampuni ya Moody’s Investors Service ilifanya zoezi la mapitio ya kwanza ya tathmini ya nchi kukopesheka katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa mwaka 2025. Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, kampuni hiyo ilichapisha matokeo ambayo yameendelea kuiweka Tanzania katika daraja la B1 kama ilivyokuwa kwa matokeo ya mwisho ya mwaka 2024. Aidha, kampuni nyingine kubwa ya Fitch Ratings inaendelea na mapitio ya kwanza kwa mwaka 2025 na inatarajia kuchapisha matokeo hivi karibuni. Kampuni hiyo ilichapisha matokeo ya mapitio ya mwisho Desemba 2024, ambapo iliiweka Tanzania katika daraja la B+.
Hapo kwanza, hizi ratings za B1 na B+ hutolewa kwa wakopaji ambao kwa vyovyote vile wataindia kwenye default yaani kushindwa kulipa deni kwa wakati sahihi.
Credit: Image by Sabrina Jiang © Investopedia 2020
Ukiangalia hilo jedwali hapo juu ni wazi kwamba Watanzania wataendelea kulipa deni endelevu kwasababu kila mara twaingia kwenye High Risk.
Sasa, kwanini Tanzania yajiingiza kuendelea kukopa huko nje jambo ambalo hata spik awa zamani Job Ndugai alishauri tujitafakari?
Naomba wataalam wa uchumi tusaidiane mie nataka kuelewa.