PreGE2025 Kuna kitu sijaelewa. Mwaka 2020 Serikali ilitenga Bilioni 268 kugharamia Uchaguzi, mwaka huu wametenga Bilioni 741. Hili ongezeko ni la nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Dah hii nchi ina pesa sana, Acha wenye viongozi wajilundikie utajiri πŸ”₯
 
Una matatizo kama jana na habari ya mkuu wa kituo. Hizi zimetumika siyo kutenga
 
Sijaisoma (sina muda wa kampeni inayosomwa saa nzima badala ya kusomewa budget), lakini yawezekana za mwaka jana ni sehemu ya fungu la serikali na nyingine walitoa wafadhili. Mwaka huu wamesema uchaguzi unagharimiwa kwa fedha ya ndani 100%.
 
1. Population growth
2. Cost za kumanage kuanzia vifaa, posho za wasimamizi etc.
3. Technology
4.kutotegemea donors
 
Kosa kubwa ni kwa wanaharakati kuwaachia wanasiasa madai ya reform ili gharama kubwa za uchaguzi ziweze kutupatia viongozi bora .

Jambo la msingi mwaka huu lilikua ni kuzuia bunge kuvunjwa kwa kuandamana mpaka Bungeni ili kuanza kupeleka ujumbe kabla ya Oktoba .

Kuzuia bunge kuvunjwa ni rahisi zaidi kuliko kuzuia uchaguzi mwana kuzuia bunge kunawapa faida wabunge na watawala waliopo ili waendelee .
Lakini kuzuia uchaguzi kunahitaji akili kubwa sana na utayari mkubwa ili kudhibiti miji yote na pia kujua maeneo gani ya kuzuia na kujipanga kwa ajili ya kupunguza matumizi ya nguvu .
Wakina mama .
Watoto ,
Vituo vya mafuta .
Mahospitali
Maofisi ya umma
Masoko
Vituo vya uchaguzi n.k
Ni maeneo yanayohitaji kupata ulinzi sana wakati wa maandamano .
Nguvu itakayo tumika kuzuia uchaguzi ni bora ingetumika kuzuia wizi kwa kushiriki ili wandamanaji wawe wanalinda kura zao na wawe na sababu .
Jambo bora lilikua ni kuzuia bunge kuvunjwa bila reform . Hii ungepata uungwaji mkono mpaka wa viongozi wa dini maana watu wote wanataka uchaguzi ufanyike kwa Haki ili tupate viongozi bora .Lakini kuzuia uchaguzi ni tukio litakalokosa watu wengi kwa sababu maandalizi yatakuwa yameshafanyika .


Wale CCM na Wenza wao kuna mahali wanahoja kidogo insyofikirisha sana
 
Mwaka huu walimu, watendaji wa kata, vijiji, polisi watapiga pesa ndefu
 
Tamasha la udom, kusafirisha kina wena sepetu, wafupi wa mama, wasanii wa mama, waandishi wa mama, wahariri wa mama, boda za mama, n.k
Kifupi ni
 
Hali wanajua wadi No reform No Election! Walikuwa wanatutishia sasa wamejua kura zetu tunabaki nazo nyumbani zisiibiwe!
 
Wizi, wizi, wizi ndani ya wizi katika wizi na kwa wizi kiwiziwizi
 
Uchaguzi ni gharama sana.

Mwaka huu

Kata zimeongezeka

Majimbo yameongezeka.

Perdiem si zile za 2020

Bei za Petrol na Diesel si zile za 2020 Kutoka 2020 had 2025 Kuna ongezeko la karibu 70% kwenye bei za mafuta
 
We dada unawashwaga sana, mmeo kasafiri muda mrefu nn?!.
Kutwa kucha kumpigia kampeni kilaza kutoka kuzimkazi!
 
Ccm ni mafia state, na wewe kushindwa kuelewa kuwa chadema inapigania ukombozi na majambazi, hapa ni ccm, ni, kazi, ya ccm wamefsnikiwa kukufanya zwazwa!
Ukombozi wa kina Heche kutoka kwenye umaskini,Mimi nimeshajilomboa kitambo kwenye kazi na wewe fanya kap ujikomboe kutoka kwenye huo ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…