Kuna kundi limejipanga kuliibia taifa letu kwa udi na uvumba. Watanzania tuwe macho

Kuna kundi limejipanga kuliibia taifa letu kwa udi na uvumba. Watanzania tuwe macho

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Hili kundi ni wanaCcm ambao wanajifanya wanaakili nyingi za kutuibia watanzania.

Huko nyuma wametuibaia sana kwa kila namna, kwa kukwepa kodi, kukwapua pesa za umma na kujilimbikizia mali. Hawa watu hawafai kwa udi na uvumba.

Sasa hivi ndio wanamuongoza chief wetu kwa kila namna. Kama taifa tusipotumbua macho tunakwenda kuibiwa kama vile tumelala usingizi wa pono.
 
Mtaje basi walau mmoja tuanze kudili nae ili awe mfano, vinginevo na wewe mmbea tuu
 
Mtaje basi walau mmoja tuanze kudili nae ili awe mfano, vinginevo na wewe mmbea tuu
Nadhani mada aliyotaka kuiwasilisha hapa hakujua kuwa ni nzito zaidi kuliko alivyojiandaa kuiwasilisha ili ijadiliwe kwa kina.

Lakini angalao kataja kitu, hata kama hakutaja mtu kama wewe unavyotaka afanye. Kataja kuwa ni kundi "la wanaCCM", kwa hiyo kakupa pa kuanzia. Ukitaka kujua zaidi itakulazimu uangalie huko ndani ya CCM.

Na ili nami nihesabike, ninakubaliana naye kwamba huko ndani ya CCM kuna kundi hatari linalotafuta njia za kuiuza nchi. Pamoja na kwamba yeye bado anaona kuwa kuna "chief anayeongozwa", mimi ninatofautiana naye juu ya hili nikiamini kwamba 'chief' haongozwi, chief ni sehemu ya mchezo wenyewe.
 
Hili kundi ni wanaCcm ambao wanajifanya wanaakili nyingi za kutuibia watanzania.

Huko nyuma wametuibaia sana kwa kila namna, kwa kukwepa kodi, kukwapua pesa za umma na kujilimbikizia mali. Hawa watu hawafai kwa udi na uvumba.

Sasa hivi ndio wanamuongoza chief wetu kwa kila namna. Kama taifa tusipotumbua macho tunakwenda kuibiwa kama vile tumelala usingizi wa pono.
Wataiba nini sasa
 
Mtaje basi walau mmoja tuanze kudili nae ili awe mfano, vinginevo na wewe mmbea tuu
Jk na kundi lake la wanaccm mahafidhina wanaodhani Tanzania ni mali ya ccm, na ccm ni mali yao, kwa hiyo na Tanzania ni mali yao.
 
Acha warudishe ukwasi wao maana mwendazake aliwapoka bila huruma.
 
Hepi aliyekua mkuu wa mkoa wa Iringa aliwapa makavu aliposema. Wastaafu wakae kwa kutulia, waache kuliongoza taifa.
I
Ndio maana Hapi anaishi kwa natumaini ya Mungu kwani anawajua vizuri na wanamlia timming tu
 
Wewe jamaa unahangaika kama kuku anayetaka kutaga!! Unaumwa ugonjwa wa kutokubaliana na ukweli kwamba yule jamaa yako pendwa zama zake zimeisha, sasa ni zama mpya!! Kaa kwa kutulia untill 2030, la sivyo utajipatia magonjwa ya moyo kwa ajili ya ujinga wako
 
Back
Top Bottom