Mshangazi mdogomdogo
Member
- Sep 23, 2024
- 64
- 43
Kuna Maafisa ambao walikuwa wakishirikiana na Uongozi wa Serikali za Mtaa kuchimba mashimbo hayo kwa ajili ya kile walichoeleza kuwa wanaweka Kalavati, lakini sasa ni zaidi ya mwezi hakuna kinachoendelea.
Wamechimba wametuachia mashimo ambayo ni hatarishi kwetu, watumiaji wengine wanaopita hapo na hasa Watoto, kwani jirani nae neo hilo kuna Shule.
Hivyo, Wanafunzi wengi wamekuwa wakipita hapo, na sasa hivi ambapo kuna mvua zinanyesha, mashimo yanakuwa hatari zaidi.
Tunaomba wanaohusika waje wamalizie kazi waliyoianza, wamesababisha limekuwa eneo hatarishi.