A
Anonymous
Guest
Mara kadhaa nimeona na nimesikia stori za baadhi ya maafisa wa LATRA, hasa jijini Dar es Salaam, wanavyotekeleza majukumu yao ya kuwakamata madereva wa bodaboda na Bajaj.
Kinachonishangaza ni kuona baadhi ya maafisa hao wakiwa katika operesheni za ukaguzi na ukamataji bila kuvaa sare au mavazi yanayowatambulisha wazi kuwa ni maafisa wa LATRA.
Hali hii inaweza kuleta mkanganyiko kwa wananchi na hata kuwaweka maafisa wenyewe katika hatari wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Nimesikia mara kadhaa kuhusu matukio ya baadhi ya maafisa hao kuingia katika vurugu na madereva wa bodaboda au hata kupigwa wakati wa ukamataji. Hali hii inaonyesha kuwa namna ya utekelezaji wa operesheni hizo inahitaji kuangaliwa upya ili kuhakikisha usalama wa pande zote mbili.
Pia kuna malalamiko kutoka kwa baadhi ya madereva kuwa wakati mwingine wanapokamatwa hawapewi Control Number bali jamaa wanataka malipo rasmi.
LATRA ina wajibu wa kusimamia sheria na kuhakikisha usalama pamoja na nidhamu katika usafiri wa umma, lakini utekelezaji wa majukumu hayo unapaswa kufanyika kwa kufuata taratibu zinazoeleweka na zinazolinda pande zote.
Nadhani ni vema LATRA ikatoa ufafanuzi kuhusu utaratibu unaotumika kwa maafisa wake wanapofanya ukaguzi na ukamataji, hususan kuhusu mavazi ya maafisa, namna ya kuwakamata madereva na utaratibu wa malipo ya makosa.