Kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba?

Kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba?

obby robby

New Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
2
Reaction score
3
Wana JamiiForums hope mko poa kabisa

Naomba kuuliza hili maana linanitesa sana. Mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nimemlipia mahari na nikamvalisha pete.

Ila mimi baada ya kuona haeleweki nikampotezea. Swali ni kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba.
 
Na kamwe kamwe usije kubali ukalishwe na ndugu sijui wapambe wakushauri sijui ndoa yenu ni baraka au aanze kujiliza Liza Mwanamke.. ooh nisamehe tusamehane..

Usirudi nyuma .. kwenye maamuzi..

Mwanamke ndiye anayetaka ndoa kuliko mwanaume remember that . Wanawake wapo wengi sana
 
Wana JamiiForums hope mko poa kabisa

Naomba kuuliza hili maana linanitesa sana. Mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nimemlipia mahari na nikamvalisha pete.

Ila mimi baada ya kuona aeleweki nikampotezea Swali ni kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba.
Utaingia hasara ya muda na pesa tu ambayo umetumia ukiwa nae. Lakin in the long run hakuna madhara
 
Hakuna madhara...ni haki Yako kudai...ila lazim uwe na sababu za msingi ..
Hata asipokuwa na sababu za msingi .. yeye ni mwanaume muda wowote anaweza amua aache maana yeye ni mwanaume na ndiye alienda kutoa mahari/li
 
Wana JamiiForums hope mko poa kabisa

Naomba kuuliza hili maana linanitesa sana. Mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nimemlipia mahari na nikamvalisha pete.

Ila mimi baada ya kuona aeleweki nikampotezea Swali ni kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba.
We piga chini
 
Ndio yapo utaishia kupiga NYETO hayo ndio madhara yenyewe
 
Chochote unachokifanya kama kitamuumiza mtu hisia zake kuna madhara.

Mfano, umelipa mahari, na umemvisha pete ya uchumba. Hayo yote umewashirikisha ndugu zake na ndugu zako bila kusahau marafiki na majirani zenu. Lengo likiwa ni kufunga ndoa.

Sasa usipomuoa huyo mchumba wako utawaumiza zaidi kihisia wazazi wake na ndugu zake. Pia yeye mwenyewe utamuumiza kihisia sababu wapo watakao mdhihaki kwa kutolewa mahari na kuachwa kabla hata ya ndoa.

Machozi na manung'uniko ya watu unaowaumiza kwa namna moja ama nyingine huwa hayakuachi salama.

Kuna kitu wazungu wanaita "divine retribution", lazima itakupata kama wewe ndiye mwenye hatia hata kama sio leo, ipo siku yatakupata.

Amini nakwambia kuna Wanawake machozi yao yana mikosi sana.

Na ndiyo maana mnaambiwa kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale, tafakari kwa kina. Ulipaswa kutafakari kabla ya kutoa mahari na kumvisha pete ya uchumba.
 
Madhara yapo unaweza ukawa Mwanachama wa kudumu wa Chaputa
 
Back
Top Bottom