Kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba?

Kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba?

Hizo taarifa mpe yeye kwamba umeachana nae sio anakusubiri kumbe wewe hauna mpango hence kuwazibia wenzako...

Haya mambo ni ya pande mbili, mutual consent bila wote kuwa na utayari bora muache leo kuliko kesho...
 
Wana JamiiForums hope mko poa kabisa

Naomba kuuliza hili maana linanitesa sana. Mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nimemlipia mahari na nikamvalisha pete.

Ila mimi baada ya kuona haeleweki nikampotezea. Swali ni kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba.
Ni nini ambacho hakieleweki? Tuanzie hapo Kwanza
 
Wana JamiiForums hope mko poa kabisa

Naomba kuuliza hili maana linanitesa sana. Mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nimemlipia mahari na nikamvalisha pete.

Ila mimi baada ya kuona haeleweki nikampotezea. Swali ni kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba.
Kwa context yako naamini unaamini mambo ya kiroho zaidi. Kwanza omba uvunje huo muungano wenu tayari halafu tuma mshenga aende huko akadai mahari irudishwe hata kama hawatarudisha yote watoe fedha kidogo ili kuvunja huo muungano uliokwisha kufanyika. Kiroho inaweza kukuzuia usioe au ukioa usidumu na mwenza wako maana unakua unamilikiwa na mtu mwingine tayari.
 
Kama uliweza kupima ukaona anakufaa ukalipa mahari, halafu ukapima tena ukaona hakufai kabla ya kumuoa, basi unauwezo Mkubwa wa kupima mwenyewe madhara ya kumuacha sababu wewe ndio unajua subject matters. Huku utapigishwa ramli tu
 
Huyu ni msumbufu, muacheni msipomjibu ataondoka mwenyewe. Ndiyo mtu anayemiliki ID's nyingi JF. Nyingi zimepigwa Ban na kila leo anaanzisha mpya. Huyu ndiyo yule huwa anadislike kila comment. Kipensili huyu...
Mpumbavu sana huyo kijana basi...
 
Back
Top Bottom