Chochote unachokifanya kama kitamuumiza mtu hisia zake kuna madhara.
Mfano, umelipa mahari, na umemvisha pete ya uchumba. Hayo yote umewashirikisha ndugu zake na ndugu zako bila kusahau marafiki na majirani zenu. Lengo likiwa ni kufunga ndoa.
Sasa usipomuoa huyo mchumba wako utawaumiza zaidi kihisia wazazi wake na ndugu zake. Pia yeye mwenyewe utamuumiza kihisia sababu wapo watakao mdhihaki kwa kutolewa mahari na kuachwa kabla hata ya ndoa.
Machozi na manung'uniko ya watu unaowaumiza kwa namna moja ama nyingine huwa hayakuachi salama.
Kuna kitu wazungu wanaita "divine retribution", lazima itakupata kama wewe ndiye mwenye hatia hata kama sio leo, ipo siku yatakupata.
Amini nakwambia kuna Wanawake machozi yao yana mikosi sana.
Na ndiyo maana mnaambiwa kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale, tafakari kwa kina. Ulipaswa kutafakari kabla ya kutoa mahari na kumvisha pete ya uchumba.