Uchaguzi 2020 Kuna mahali CCM ilikosea?

Mimi kanishangaza kila akienda sehemu upinzani unanguvu anawambia wananchi,

"msinichanganyie magunzi, ukichagua mpinzani sileti maendeleo"

Ndugu zangu JF members hivi Jiwe hiki kiburi anakitoa wapi wakat sisi wananchi ndio mabosi wake na ndio walipa kodi wa nchi hii?

Mbona kiburi hiki hatukukiona kwa JK, Mkapa RIP, Mzee Mwinyi na Mwl RIP?

Hivi Jiwe ni raia mwenzetu kweli? Yaani usipeleke maji na barabara Singida kwa Watanzania wenzako kisa wamemchagua mpinzani?
 

Kuna clips ya Kikwete wakati huo ni Mwenyekiti na Rais wa JMT aliwaambia CCM hawezi kutumia police kujibu hoja za wapinzani.

Ni wajibu wa Kinana,Nape na Mawaziri kujibu hoja za wapinzani,utawala imekuwa ni kazi ya police,mahakama,TRA na Uhamiaji kujibu hoja kwa namna ya kutisha,kuadhibu,kupotezwa na kubambikiwa kesi za kutakatisha fedha.
 
Kuna Watawala 3 Duniani ambao sikuwahi kudhania wangetoka madarakani niliomba uhai niwashuhudie Wakitolewa Madarakani nao ni Sadam Hussein, Mobutu Sese Seko na Omar Al Bashir! Kweli nikashuhudia! Naamini nitashuhudia CCM ikitoka madarakani siku moja pia
 
Rukwa,Sumbawanga,Katavi,Simiyu,Ruvuma,Lindi na Mtwara ni ngome ya CCM kwa muda mrefu lakini tumeshuhudia katika uchaguzi huu wananchi wa mikoa hiyo wakibadilika na hivyo kuiweka CCM katika wakati mgumu.
Mkuu uchaguzi unafanyika 28/10/2020!!! Mabadiliko gani unazungumzia !!!
 
Wewe tangu lini ukawa unafuatilia ya CCM? Endelea kula tende tu hapo Arusha, mwaka huu tunakwenda kuwatia adabu kwa majivuno yenu na njama ambazo mmekuwa mnataka kuzitumia kuchafua uhuru na haki za Watanzania. Huyo kibaraka wenu tutamrudisha fasta Belgium. Hao Belgium waliweza DRC (Congo) waambie Tanzania hawawezi sisi ndio Baba lao.
 

Hoja nzito majibu mepesi,huu si uungwana unanikumbusha kipindi Mtangazaji maarufu nchini Kenya “Huu si ungwana”
 
Rejea kauli ya Zitto, "tumekabidhi nchi kwa washamba"

Watu wanaoamini wao ndio wametumwa na Mungu kutuokoa (nikiondoka sijui kama kuna mwingine ataweza kufanya haya)

Watu wanaoamini kuwa wao peke yao ndio wenye uchungu na nchi yetu (msiwasikilize hao wanaotumiwa na mabeberu)

Watu wanaoamini kuwa wanajua kila kitu hawaihataji kujifunza wala kushauriwa (wastaafu wanawashwa washwa)

Watu wanaoamini kuwa nguvu ndio suluhisho la kila tatizo (tutapeleka JKT wakabangue korosho hata kwa meno)

Watu wasiotaka mijadala wala kuhojiwa kuhusu matendo yao (mimi sipangiwi cha kufanaya)

Inshort CCM wametuletea mtu ambae hata wenyewe wameshindwa kumdhibiti, ndio katufikisha hapa
 
Majigambo, matusi, mbwembwe zote mwisho tarehe 28

Kuanzia tarehe 29 tukutane hapa kupeana pole na pongezi😁😁😁😁😁

Maendeleo hayana vyama
 
Team ya CCM ikiongozwa na Dr Bashitu imetepeta sana,Polepole hajui aseme nini na lipi la kunyamaza.

Mpaka leo Nadhani Polepole kafikisha press conference 50 ambazo hazina impact yoyote kwa wapiga kura zaidi ya kumfurahisha aliyemteua.
 
 
Mimi maoni yangu ni haya:
1: Uongozi unapoingia madarakani ni muhimu kutekeleza Sera ambazo chama kimekuandikia/kuandalia kinyume na hapo utaweka mawazo yako binafsi utapishana na kipaumbele cha wananchi
2:Uongozi ni utumishi wa watu siyo Mali binafsi
3: Maendeleo ya nchi ni mwendelezo wa Yale ambayo watangulizi wako waliweza
4:Wananchi ni Watu wenye akili timamu,mawazo,maono,fikra na matarajio,ukiwafanya kuwa kama watoto wasiojua lolote ni kosa
5:Uteuzi wa viongozi mbali mbali uzingatie vetting na sifa stahiki,ukichukua tu hotels ni rahisi kuharibu Taifa
6: Kupokea ushauri sahihi ni Jambo muhimu
7: Uongozi usichuliwe kama ni Alfa na omega,mtawala anaweza Fanya chochote kwa raia wake ni kosa
8:Katika uongozi Utu,haki,uhuru na faraja ni jambo muhimu
9: Matatizo ya nchi yatatuliwe kwa kufuata kipaumbele cha wananchi,mfano:Jengo zuri la Ofisi si Bora Kuliko maji kwa wananchi,mbolea kwa wakulima,madawa hospital nk.
10:Wananchi hujisikia fahari pale ambapo maswala makubwa yanapata majibu na serikali,mfano,mtu kapotea,kauawa,serikali isiposhirikiana na raia ni Rosario
11: Maamuzi ya raia ya heshimiwe,mfano utanunuaje wapinzani kwa hela nyingi wakati watu hawana barabara,hosipitali nk
Yangu ni hayo wengine wanaweza ongeza
 

Huwezi kubadilisha Watanzania kwa kulazimisha. Haiwezekani na haitawesekana
 
Passive resistance...kwa mwenyekigoda.
Mjanja yeye, Bashite, Slowslow, na Kalamaganda, so wamewaachia wasomi na wajuvi zaidi waendelee.

Nileeeteeni.....................................
Nileteeeeeeni..........................................
Nileteeeeeeeeeeeeni...............................

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…