mozila firefox
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 899
- 1,761
Mimi kanishangaza kila akienda sehemu upinzani unanguvu anawambia wananchi,Wakuu heshima sana,
Kadri siku ya uchaguzi mkuu zinapokaribia nabaki najiuliza maswali kadhaa bila majibu.
Najaribu kutafakari ni eneo gani haswa CCM ilikosea ?.
Mosi,kununua wapinzani (wabunge,madiwani na viongozi wa vyama).Wananchi au ukipenda unaweza kuwaita wapiga kura hawapendi siasa za aina hiyo.
Ukinunua wabunge au madiwani yawezekana bado haujanunua wapiga kura au sababu za kuchagua upinzani bado zinakuwa pale pale !.
Pili,Style ya kutawala au kuongoza za utawala huu si rafiki au wapiga kura hawazipendi.Hivi siasa za kutumbua tumbua fukuza fukuza mara vyeti feki bado si jawabu la kupendwa ? !.Labda tuseme kulikuwa na uonevu,kukiuka sheria na taratibu za ajira au vyote kwa pamoja.
Tatu, Matumizi ya kupiliza ya vyombo vya habari kusifiwa na majivuno.TBC chini ya Dr Ryoba ilipitiliza kusifu kila jambo mara ndege,Reli,Vyeti feki lakini Makonda hausiki na ukaguzi.Barabara hata ya Kilometer 2 mtu atasifiwa kuanzia asubuhi hadi jioni kuanzia Jumatatu hadi Jumatatu nyingine ni mwendo wa kumsifu mtu mmoja ungefikiri kujenga Daraja au Kivuko ni Hispano kumbe ni wajibu wake tena kazi yenyewe kaiomba kwa kampeni na ahadi luluki.
Nne,Unasema pekee yako miaka mitano wengine wakisema shida (Kesi,Vifungo,misukosuko....)Nauliza WaTanzania wamechoka na siasa za aina hii !.
Tano,Ujenzi wa Flyover Dar una faida zipi kwa mkaazi wa Dongobesh au Tarakea mkulima wa ndizi au mkulima wa Ngogwe Lushoto.Naamini kila eneo la nchi yetu lina mahitaji yake ya msingi kutokana na mazingira yake.
Sita,Watawala wetu walifika mahali wakajiona hapo walipo walifika wenyewe si wananchi /wapiga kura.Kauli zao maamuzi yao mengi yalilenga kuwanufaisha wao wenyewe eg kupitisha sheria za kuwajengea nyumba MaRais wastaafu,Sheria za mafao yao na matibabu yao zipo vizuri kweli kweli wakati wafanyakazi sheria za mafao yao kila mara wanatengenezewa sheria za kuwakandamiza eg sheria ya kujitoa na kikokoteo.Sheria za kinga ya kutoshitakiwa hata wakifanya makosa ya aina gani !.
Mwisho nadhani watawala hawakujiandaa kukumbana na uchaguzi wenye ushindani wa kiwango hiki tunachokiona sasa.Walifikiri kumnunua Silinde,Lijualikali,Nassari ...... watakuwa wamemaliza kila kitu sasa wamekutana na uungwaji mkono wa kiwango cha kutisha kutoka kwa mgombea wa CHADEMA.
Tangu mfumo wa siasa wa vyama vingi kuanzishwa tumewaona wagombea walioleta kashi kashi za kutisha.Mwaka huu 2020 tumeanza kuona dalili mbaya kwa baadhi ya mikoa ambayo chaguzi za nyuma walikuwa wakiunga mkono CCM.Mkoa ya Rukwa,Sumbawanga,Katavi,Simiyu,Ruvuma,Lindi na Mtwara ni ngome ya CCM kwa muda mrefu lakini tumeshuhudia katika uchaguzi huu wananchi wa mikoa hiyo wakibadilika na hivyo kuiweka CCM katika wakati mgumu.
"msinichanganyie magunzi, ukichagua mpinzani sileti maendeleo"
Ndugu zangu JF members hivi Jiwe hiki kiburi anakitoa wapi wakat sisi wananchi ndio mabosi wake na ndio walipa kodi wa nchi hii?
Mbona kiburi hiki hatukukiona kwa JK, Mkapa RIP, Mzee Mwinyi na Mwl RIP?
Hivi Jiwe ni raia mwenzetu kweli? Yaani usipeleke maji na barabara Singida kwa Watanzania wenzako kisa wamemchagua mpinzani?