Panctuality
JF-Expert Member
- Jun 11, 2019
- 1,160
- 1,748
Mtume Mudy anafufuka lini....يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ وَكَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ ﴿١٩﴾
19. Anatoa kilichohai kutokana na kilichokufa, na Anatoa kilichokufa kutokana na kilichohai, na Anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na hivyo ndivyo mtakavyotolewa (kufufuliwa).
Suurat Ar Rum
Kifo ni ni mwisho wa kila kitu hakuna cha maisha mengine wala niniKuna maisha baada ya kufa, au tukifa ndiyo mwisho wa kila kitu?
Hili ni swali ambalo limekuwa likiwagawa watu kwa karne nyingi. Wapo wanaoamini kuwa kifo ni mwisho wa kila kitu, hakuna fahamu wala maisha mengine. Wengine wanaamini kuwa kifo ni mlango wa kuingia katika maisha mengine, ambako matendo ya duniani yanaendelea kuwa na maana.
Sasa hebu tufikiri.
Kama tukifa ndiyo mwisho wa kila kitu, je, kuna sababu ya kujinyima sana? Je, tuishi kwa kutumia na kufurahia mali zetu kadiri tuwezavyo kwa sababu baada ya kifo hakuna tena nafasi nyingine?
Lakini kama kweli kuna maisha baada ya kifo, je, si busara kuishi kwa tahadhari? Tuilinde miili yetu, tusiiharibu kwa makusudi, na tufe tukiwa na nguvu na afya kadiri inavyowezekana, kwa imani kwamba huenda kuna safari nyingine inayotuhitaji baada ya maisha haya.
Wewe unaamini nini? Je, kifo ni mwisho wa kila kitu, au ni mwanzo wa maisha mengine? Na kwa nini unaamini hivyo?
Perspective nzuri sana hiiMi nadhani baada ya kufa kila kitu kinakuwa kimeishia hapo. Hata kama kutakuwa na kitu kinaendelea baada ya kifo kinakuwa hakina uelewa wako uliyekufa maana unakuwa hautambui chochote.
Huenda pia unapokufa unahamishwa kabisa katika dunia hii na kupelekwa kwenye mojawapo ya vitu vilivyoko angani iwe nyota,sayari,galaxy, metroids nk na kuanzisha maisha mengine ukiwa katika hali nyingine kabisa ila likiumbe ambalo linaweza kuishi kwa namna nyingine inawekana ukaishi kwa Kula vumbi au vyovyote vile ambavyo nature itaamua juu yako.
Maana huenda hata huko kwenye sayari za mbali au kwenye universe ambazo tunaamini hakuna viumbe huenda vipo ila vinaishi katika form nyingine kabisa, haiwezekani Mungu au nature iwe na likitu kama sayari ya Jupiter ambayo ni kubwa karibu mara 130 au zaidi halafu kusiwe na chochote kinachokaa huko tatizo sisi binadamu tunafikiri ili uishi ni lazima ule chakula na kunywa maji tu huenda Kuna maisha yanayowezesha kuishi hata kwenye joto la centigrade 5000 na ukaishi bila shida.
Pia kwenye maisha mi naamini hatufi tu accidentally bali kuna viumbe vinavyotuvuna bila sisi kujua ni kama ambavyo wewe unaweza kumpangia mbuzi huyu tutamla kesho andaeni visu na huyo mbuzi anasikia na wala hawi na wasiwasi wowote juu ya ulichompangia.
Muhimu nadhani maisha ni hayahaya tu ukiwa vizuri economically Kula maisha na wenzangu na Mimi huenda maisha yako mazuri yamepangwa kwenye sayari nyingine huko maana kama unaambiwa galaxy yetu tu Ina terrestrial bodies zaidi ya bilioni moja na Kuna galaxy zingine zaidi ya billion moja kweli Bado unaamini Kuna kuchomwa moto baadaye sidhani kwa kweli. Haya majanga yanayotokea ni katika kuji balance tu kwa dunia yetu na wala huenda hayana uhusiano na dhambi yoyote
Achana na imani hembu jibu kiuhalisiaيُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ وَكَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ ﴿١٩﴾
19. Anatoa kilichohai kutokana na kilichokufa, na Anatoa kilichokufa kutokana na kilichohai, na Anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na hivyo ndivyo mtakavyotolewa (kufufuliwa).
Suurat Ar Rum
"Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala." 1 Wakorintho 15:20
"Na kama Kristo hakufufuka, basi kuhubiri kwetu ni bure, na imani yenu nayo ni bure." 1 Wakorintho 15:14
"Hupandwa katika uharibifu, hufufuliwa katika kutokuharibika... hupandwa mwili wa asili, hufufuliwa mwili wa roho." 1 Wakorintho 15:42-44
"Maana twajua ya kuwa nyumba yetu ya hapa duniani, maskani hii ya hema, ikivunjwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu... la milele mbinguni." 2 Wakorintho 5:1
"Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida... Natamani kuondoka nikakae na Kristo, maana ni hali iliyo bora zaidi." Wafilipi 1:21-23
"Tuna ujasiri, naam, twapendezwa zaidi kukuwako mbali na mwili, na kukuwako nyumbani kwa Bwana." 2 Wakorintho 5:8
"Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo; ili kila mtu apokee..." 2 Wakorintho 5:10
"Mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu." Warumi 6:23