Kuna maisha baada ya kifo au tukifa ndio mwisho wa kila kitu

Inategemea wewe ni nani....
Tupo dunia moja lakini kila mtu ana ulimwengu wake.....
Wengine sisi ni wana wa Mungu na wengine ni uzao wa nyoka...(si wanadamu...ingawa kimuonekano twafanana)...

>>>hiyo ni kwa kufupi>>>>>>>
 
Usiku unapolala, zile ndoto unazoziota, je? ni hiari yako mwenyewe????
Ile ni reaction tu ya ubongo kwa matukio tunayopitia pamoja na kumbukumbu halafu tofautisha kuota ndoto na kufa..kufa maana yake kwishnei hutoota ndoto hutohisi njaa hutohisi nyege halafu kuhusu ndoto sio kitu cha ajabu ukumbuke hata mahindi nayo yanaota.
 
Pongezi kwako kwa ufafanuzi mzuri
 
Hakuna cha wana wa Mungu Wala wa shetani sote ni wa Mungu ila issue ya kuchomwa moto huenda haipo. Hii dunia ina zaidi ya miaka bilioni kadhaa. Kwa mfano tuamue kutumia tu kalenda ya Sasa tuko mwaka 2026 sasa ukichukua mwaka WA kwanza mpaka mwaka 1790 hakuna hata binadamu mmoja anayeishi leo hii hata wa 1800 kamili waliopo hawafiki hata 200 dunia nzima. Unaniambiaje Kuna wakati tutachomwa moto wakati waliokufa mabilioni kwa mabilioni wametelekezwa tu hivohivo
 
Hebu uwe unatumia akili, umeambiwa humu Jf ndio kuna watu waliowahi kufufuka?
 
Jizime data uamini ngano za watu wa majahazi
Au washa 5G ule maisha
You only live once
 
Kuna maisha baada ya kifo. Maisha ya funza na wadudu wengine. Maisha ya mimea. Maishabya vidudu.
 
Hebu uwe unatumia akili, umeambiwa humu Jf ndio kuna watu waliowahi kufufuka?
Wewe unadhani ni wapi waliowahi kufufuka wapo ili nielekeze mjadala huko?
Ulipokuwa unafundishwa history na mwalimu wako, unadhani huyo mwalimu wako alikuwepo katika tukio alilokuwa anakusimulia?
Vingi vina uchunguzi na viliishawahi patiwa majibu.
Acha members watililike wewe tegesha fuvu lako empty lipate kujazwa madini parasite wa karne wewe!!!
 
Kabla ya sisi kuwa hapa je tulikuwa wapi huko?

Na kwanini hatukumbuki huko tulipokuwa
 
Kuna maisha kabla ya maisha? Unakumbuka ulikokuwa kabla ya kuzaliwa? Kulikuwa na maisha kabla ya kuzaliwa? Kwa nini kuwe na maisha baada ya kifo? Wanyama wengine je? Au sisi ni so special? Maswali ni mengi majibu ndio hakuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ