cnx
Member
- Apr 26, 2021
- 6
- 6
Naomba mamlaka husika kuchunguza malalamiko kuhusu utaratibu wa usajili kwenye mfumo wa NaPA kwa waombaji wa mikopo ya elimu ya juu katika Wilaya ya Sengerema, Mwanza.
Kuna malalamiko kwamba mtendaji mmoja wa wilaya anawataka wanafunzi wanaohitaji kusajiliwa kwenye mfumo wa NaPA kutoa fedha kwa madai kuwa ni za nauli na bando la intaneti ili kukamilisha usajili wao.
Iwapo madai haya ni ya kweli, inazua maswali kuhusu utaratibu huo. Je, Serikali haikutenga bajeti ya kugharamia huduma hizi hadi wanafunzi waombwe kuchangia fedha hizo? Aidha, kama malipo hayo ni halali, kwa nini yasiwe na utaratibu rasmi, kama kutumia control number au njia nyingine ya malipo ya Serikali, badala ya kukusanywa moja kwa moja?
Binafsi nililazimika kutoa fedha hizo ili mdogo wangu asajiliwe kwa kuwa nilikuwa nazo. Hata hivyo, najiuliza kama malipo hayo yalikuwa halali au la. Hofu yangu ni kwamba wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kutoa fedha hizo wanaweza kushindwa kusajiliwa kwenye mfumo wa naPA, jambo ambalo linaweza kuwanyima fursa ya kuomba mkopo wa elimu ya juu na hivyo kuathiri ndoto zao za kuendelea na masomo.
Tunaomba mamlaka husika zitoe ufafanuzi kuhusu suala hili na, ikiwa kuna ukiukwaji wa taratibu, zichukue hatua stahiki ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapata huduma kwa usawa bila kutozwa fedha zisizo rasmi.