Kuna mambo watu hawayaelewi kuhusu Mungu

Hivi Mungu wetu waafrika jina lake ni lipi, ikiwa Mungu wa Israel ni Yahweh, Arabs ni Allah, Huko Asia kuna Krishna, Shangdi na wengine wengi?
Binadamu wote tumeumbwa na Mungu. Hao wengine wanaoabudiwa ni Watu waliojikengeusha tu kuabudu Miungu ya Majini kutoka katika Viumbe wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho cheo kina maana kwako unayeamini hivyo,ukikutana na wale wanao mwabudu Mungu Buddha kwao ndio Mungu muweza wa yote.

Sio kosa kudhani hivyo ikiwa ndio uwezo wao wa Akili ulipofikia.

Ni Kama mtoto akiwa mdogo anadhani Baba yake anaweza kupiga Dunia nzima ilhali Baba yake Kwa wengine ni Fala tuu, asiye na lolote.

Au hata kwenye nchi wapo watu wenye Uelewa mdogo wanafikiri Rais ndiye the Top lakini kumbe Hali iko tofauti Kwa Rais mwenyewe anavyojiona
 
Kwa sababu wanamuabudu asiyestahili kuabudiwa ambaye sio Mungu MUWEZA WA YOTE
Kwa nini wewe udhanie ya kwamba Mungu wao astahili ila wa kwako ndio anastahili kuabudiwa?
Na kama swala ni muweza wa yote,huyo unayemsema wewe ni mambo yapi au vitu vipi ameviweza vyote?
 
Kwa nini wewe udhanie ya kwamba Mungu wao astahili ila wa kwako ndio anastahili kuabudiwa?
Na kama swala ni muweza wa yote,huyo unayemsema wewe ni mambo yapi au vitu vipi ameviweza vyote?

Mkuu hakuna sehemu niliyosema Mungu wangu au mungu wao, nilikuwa nachambua Mungu MUWEZA WA YOTE na miungu.

Mungu MUWEZA WA YOTE kafanya yote uyaonayo na wote wayafanyayo na Yale ambayo hukuyaona na ambayo hutayaona.

Wewe ukimuangalia Kama Zumaridi anastahili kuabudiwa?
 
Inawezakana nao wakakuona hivyo hivyo kuwa uwezo wako wa akili ndio unaopelekea kudhani Mungu wako ndio Mkuu kushinda wao.

Kuhusu hiyo mifano 2 ni mifano ambsyo inaweza kuthibitika hivyo MTU kukosa uelewa wa mambo hayo haimanishi hayapo.tofauti na hilo LA kwako la kusema Mungu Mkuu ndio muweza haliwezi kuthibitika bali ni imani.
 
Mkuu hoja yangu ni kuwa neno Mungu muweza,Mungu Mkuu au Mungu yoyote yule inategemeana na imani ya muhusika-wewe unayedhania kwako ni Mkuu anaweza asiwe Mkuu kwa mwingine,wewe unayemuiita miungu kwa wengine ni Mungu.

Mfano kwa wanao amini katika Mungu Buddha, kwako sie tunaye muita Allah au Mungu Muweza kwako wanawachikulia kama miungu halafu huyo Buddha ndio Mungu.Pia kama wewe unavyoona Mungu wako anaweza yote nao wanaona wa kwao pia anaweza yote na itakuwa kinyume na imani kudhania wa kwako anaweza halafu wao usiweze.

Kwa issue ya Zumaridi siwezi sema kama anastahili kuabudiwa au hastahili,sababu mie sio muumini wake ila kwa waumini wake wanaona anastahili na kwao anaweza kuwa ni Mungu.Kama ambavyo wewe unaona Mungu wako anastahili kuabudiwa nao wanaona wa kwao nao anastahili.
 

Mimi sijazungumzia Mungu wangu elewa hoja Mkuu.
Mungu wangu anawez asiwe Mungu Mkuu MUWEZA WA YOTE.

Na Mungu anayethibitika anapoteza sifa ya MUNGU MKUU muumba wa mbingu na Nchi.

Mungu hajawahi kuonekana popote pale wala hajawahi kusikika popote pale
 

Kwangu haina shida na wala siumii wala Mungu MUWEZA WA YOTE haumii wala kufurahi hata ukimuita na kumfananisha na miungu.
Ila miungu ndio inashida ikifananishwa na miungu wengine, inajisikia wivu
 
Thibitisha Mungu yupo na kwamba hizo habari za kuwapo kwa Mungu si hadithi za uongo tu walizojitungia watu.
 
Uwepo wa miungu midogo ni udhihirisho wa Mungu Mkuu MUWEZA WA YOTE
Hujathibitisha hata hao miungu wadogo wadogo wapo.

Halafu your argument is a logical non sequitur.

Uwepo wa namba ndogo ndogo hauthibitishi kuwapo kwa namba ya mwisho kupita zote.

Uwepo wa prime numbers hauthibitishi uwepo wa the highest prime number.
 
Unaamini mizimu na Mizuka Kuwa Ipo?
 
Hivi Mungu wetu waafrika jina lake ni lipi, ikiwa Mungu wa Israel ni Yahweh, Arabs ni Allah, Huko Asia kuna Krishna, Shangdi na wengine wengi?
MUNGU wa afrika alitekwa nyara anatmika huko mashariki ya mbali na magharibi ya kati pia anapewa mateso makali na kuzidi kutoboa Siri za namna ya kutongoza waja wake..
Pia anaendelea kuwapa akili na maalifa watu walio mteka wanatumia sheria na mbinu za mungu wetu katka kuitawala dunia ...
 
Binadamu wote tumeumbwa na Mungu. Hao wengine wanaoabudiwa ni Watu waliojikengeusha tu kuabudu Miungu ya Majini kutoka katika Viumbe wengine

Sent using Jamii Forums mobile app

Mungu katekwa 🤣🤣🤣 makubwa haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…