Kuna Manabii wa uongo, je Manabii wa kweli ni wepi?

Kuna Manabii wa uongo, je Manabii wa kweli ni wepi?

Mungu akusaidie.

Roho mtakatifu ni ROHO wa YESU kristo. Ukimpokea Yesu, utapokea zawadi ya Roho mtakatifu. Anaishi ndani ya WATAKATIFU
Mungu hawezi nisaidia kitu.
apo bado umehubiri kulingna na dini yako ilivyokukuza , ungekuzwa na nyingne ungesema tofauti pia ,kwa hiyo bado haujasema.
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Kama kuna jambo ambalo lilikuwa likiniwazisha ni namna ya kumjua Nabii wa uongo na wa kweli.

Nilisikia habari hizi kutoka katika mahubiri kanisani tokea nilipokuwa mdogo.

Kifupi habari hizi ziliniitisha maana sikuwa najua ya kuwajua Manabii.

Nikakua bado nilisikia tu niendelea kusikia habari za kuja Manabii wa uongo.

Mpaka sasa bado nazisikia habari hizi za Manabii wa uongo.

Watu wanasema Manabii wa uongo tu, je hakuna Nabii wa kweli?

Kama yupo ni yupi?

Wamemjuaje huyo Nabii ni wa kweli?

Biblia inasema neno 1Yohana 4:1
Wapenzi msiamini Kila roho, bali zijaribuni hizo roho, bali ziketoka kwa Mungu

Mathayo 7:15
Jihadharini na Manabii wa uongo, watu wanaowajiq wamevaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu

Mwl Mwakujonga Rabbon
Dada angu Donatila
1. Nabii wa kweli kwanza huwez kumkuta anajiita nabii
2. Nabii wa kweli huwa wanahubiri tuu na kuwasihi watu kutubu na kumrudia mungu, then akiondoka ndo utakuta watu waanza kumwita nabii, wale manabii wote wa zamani wakina Isaya, Jeremiah, Elia wote hawakujiita manabii, watu ndo waliowaita manabii.
3. Nabii wa kweli hatumii miujiza kuaminisha watu kwamba yeye ni nabii, nabii huwasihi watu kumrudia mungu kwa kufanya toba na kusoma neno la mungu(biblia) kama njia pekee ya kumjua mungu.
4. Nabii wa kweli hajilimbikizii mali(sadaka za watu), manabii kama Eliya, ezekieli na Isaya walikuwa watoaji wa zaka na sadaka, tena Paulo aliwasihi watumishi wa mungu kufanya kazi za mikono ili waweze kujikimu, yeye mwenyew Paulo alifanya kazi ili asiwategemee, kwa Paulo alikuwa anaona ni vibaya sana unapowahubiria watu then ukimaliza unawaomba nauli au hela ya kula.
5. Utawatambua kwa maneno wanayoongea na jinsi wanavohubiri, pima kile mtu anachoongea...je, kinaendana na neno la mungu? Je, kina ukweli wowote kuhusu Sheria za mungu? Je, kina sisitiza upendo kwa mungu na upendo baina yetu??

Itaendelea....
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Kama kuna jambo ambalo lilikuwa likiniwazisha ni namna ya kumjua Nabii wa uongo na wa kweli.

Nilisikia habari hizi kutoka katika mahubiri kanisani tokea nilipokuwa mdogo.

Kifupi habari hizi ziliniitisha maana sikuwa najua ya kuwajua Manabii.

Nikakua bado nilisikia tu niendelea kusikia habari za kuja Manabii wa uongo.

Mpaka sasa bado nazisikia habari hizi za Manabii wa uongo.

Watu wanasema Manabii wa uongo tu, je hakuna Nabii wa kweli?

Kama yupo ni yupi?

Wamemjuaje huyo Nabii ni wa kweli?

Biblia inasema neno 1Yohana 4:1
Wapenzi msiamini Kila roho, bali zijaribuni hizo roho, bali ziketoka kwa Mungu

Mathayo 7:15
Jihadharini na Manabii wa uongo, watu wanaowajiq wamevaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu

Mwl Mwakujonga Rabbon
Manabii wote ni wa uongo, wanazidiana uongo tu.

Ukishasema kuwa wewe ni nabii wa Mungu, katika ulimwengu ambao Mungu hayupo wewe tayari ni nabii wa uongo.

Ama kwa kujua na kupanga hadaa, ama kwa kutojua na kuamini uongo wako mwenyewe.
 
Mpaka sasa sinapata Jibu la watu huku ndani...
 
Quran imeletwa baada ya Yesu kufufuka, hivyo ni nafundisho wa uongo ya kupotosha.
Qur an sio INJILI na Injili sio zaburi na Zaburi sio Taurati

Injili ya uwongo ni hiyo inayo ruhusu ushoga kanisani na kuwa singizia Manabii uzinzi
 
Nabii maana yake ni binadamu anayepokea ufunuo kutoka Kwa Mungu

Manabii watatu wa mwisho Kwa mujibu wa Quran ni
1) Yohana mbatizaji
2) Yesu
3) Muhammad
 
Back
Top Bottom