technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,706
- 52,355
Sitaki kutaja majina ila tetesi zilizopo ni kuwa
1 : Mkuu wa taasisi nyeti ya Serikali mmoja ataondolewa
2: Mawaziri wa baadhi ya wizara kupanguliwa.
Ni kutokana na mkuu analalamika mambo hayaendi kama anavyotaka yaende.
My take: pole yenu mtakaopatwa na mtikisiko.
Stay tuned
1 : Mkuu wa taasisi nyeti ya Serikali mmoja ataondolewa
2: Mawaziri wa baadhi ya wizara kupanguliwa.
Ni kutokana na mkuu analalamika mambo hayaendi kama anavyotaka yaende.
My take: pole yenu mtakaopatwa na mtikisiko.
Stay tuned
Kuna habari zimetapakaa hapa mjini kuwa Rais Makufuri anatarajia kupangua Baraza la Mawaziri siku yoyote kuanzia sasa.
Imeelezwa sababu za Rais kupangua Baraza hilo ni kuwafuta kazi baadhi ya mawaziri ambao wameshindwa kwenda na kasi ya Hapa Kazi Tu hivyo ameona bora awabwage baadhi ya mawaziri mizigo badala ya kuendelea kuing'ang'ania kuwabeba.
Hii itakuwa ni mara ya pili Rais kuwafuta kazi mawaziri tangu alipomfuta kazi Waziri Charles Kitwanga kwa sababu ya kulewa akiwa kazini. Mtangulizi wake Rais Kikwete alibadili Baraza la Mawaziri zaidi ya mara 8 kwa sababu mbalimbali zikiwemo kashfa maarufu za Richmond, Operesheni Tokomeza na Escrow.
Tusubiri tuone ni kina nani watakaopitiwa na panga hili la Makufuri na nani watapenya kwenye tundu la sindano. Kuna kila dalili kwamba kuna baadhi ya mawazi watafutwa kazi kwa sababu ya ama kumdanganya rais au kutojituma ipasavyo kwenye nafasi zao. Je, unaweza kutabiri nani atakuwa wa kwanza kupitiwa na panga hili?
Nawasilisha